Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Hii issue ni ngumu sana kung'amua kama ingekuwa rahisi basi naamini kuna watu wangeshajitosa mazima kujua ukweli. Either kwa ujiko tu au ku piga hela.
ila huwa nawaza wale outlawz wanaweza kuwa na abc's za waliomwangusha big maana kwa aina ya kifo alichokufa pac lazima jamaa wangeingia chimbo kulipa kisasi. Kama upande wa pac hawakuhusika moja kwa moja lazima outlawz kama washkaji wa karibu wa pac wangetamani kujua nani alimwangusha big.
Katika wa watu mwanzo waliamini kurejea kwa pac mimi nilikuwa mmoja wao ile tarehe ili pofika kimya nikaamini nikajua jamaa alikufa kweli.
All in all baada ya kusoma vitu vingi mitandaoni naamini all was set up kuwaondoka wote (kuwaangusha). Ukirudi nyuma jinsi hali ya east n west side zilivyokuwa unawaza hivi leo ingekuwaje. ilikuwa hatari sana. hizi habari za suge knight sijui diddy sijui Orlando ni uzushi tu.
Gavoo
 
KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO ? (4)
_______________

Inaendelea......

Kutokana na Tupac kuhitaji bosi wa Death Row, Marion 'Suge' Knight apambane kumtoa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja, Suge aliangaika huku na huko mpaka kufanikiwa kumchomoa Tupac jela.

Kiasi cha Dola Milioni 1.4 kilitolewa na Suge hivyo kufanikiwa kumtoa jela Tupac mwaka 1995, achilia mbali Dola 15,000 ambazo Suge alizitoa kumsaidia 'kishkaji' Tupac wakati akiwa jela.

Kimsingi Suge alikubali kujipukutisha fedha kwa sababu alijua kumwandika Tupac mkataba wa kumsimamia kupitia Death Row Records italipa. Knight alijua nini anafanya kwenye makubaliano hayo.

Makubaliano ya Tupac na Suge yakawa mazuri. Tupac akakubali kutengeneza albamu 3 chini ya Death Row Records lakini muda wote akihitaji Suge awe upande wake kwenye vita vyake dhidi ya Biggie.

Nyimbo ya kwanza ya Tupac kuitoa chini ya Death Row Records ikawa California Love. Kombinesheni ya Tupac, Dr Dre na Roger Troutman kwenye chorus ukawa unyama wa kufa mtu. Kwa hakika "The King was back from Jail''.

Ujio wa California love ulimtikisa kila mtu. Tupac alikuwa amejerea kuusimika upya ufalme wake uliotishiwa kuondoshwa kwa mtutu wa bunduki na vijana kutoka Pwani ya Mashariki (East Coast).

Marion Suge Knight na Tupac Shakur wakafanikiwa 'kuupika' mgogoro wa East Coast na West Coast ukapikika, mgogoro ambao chimbuko lake haswa ni chuki baina ya wasanii wawili, Notorious Big na Tupac Shakur.

Matatizo binafsi ya Biggie na Tupac yakajikuta yakirithiwa na hata wengine 'yasiyowahusu'. Wasanii wa East na West wakaonekana kuchukiana katika kiwango kilichotisha kabisa.

Wakati mgogoro huu ukikua na kuzidisha uhasama kwa wasanii, Serikali mwanzo ilionekana kama kupuuza, lakini kadiri hali ilivyozidi kuwa mbaya na viongozi walilazimika kusema chochote.

Lakini kabla ya kusema chochote, huko nyuma Tupac alikuwa ameshaingia kwenye mgogoro mara kadhaa na serikali kutokana na misimamo yake, harakati zake na maisha yake.

Nyimbo zake kupitia albamu yake ya 2Pacalypse ziliichefua sana serikali. Tupac alizungumzia zaidi Siasa, Ubaguzi na umasikini katika namna ambayo ilionekana kama kuchochea chuki kwa raia.

Mshtuko mkubwa ulitokea baada ya kijana mmoja mdogo kumpiga risasi polisi na kumuua kisha baada ya kukamatwa na kuhojiwa akathibitisha kufanya hivyo baada ya kusikiliza albamu ya Tupac iitwayo 2Pacalypse.

Tukio hilo lilikuwa gumzo nchini Marekani. Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Bw Dan Quayle akatangaza kupigwa marufuku kwa nyimbo za Tupac kusikilizwa kwenye Jamii ya wamarekani.

Bw. Quayle alisema Tupac ni msanii asiyefaa kabisa kusikilizwa. Nyimbo zake zimejaa chuki na kuchochea uovu kwenye jamii. Akaanzisha kampeni za kuhakikisha jamii inamchukia na haipati nafasi ya kumsikiliza Tupac.

Masikini Quayle hakuwa amejua kuwa wakati anasema hayo, Tupac alikuwa ameshaiteka sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani kuliko anavyodhani. Mahojiano yake na MTV ya mwaka 1993 yamlitosha kabisa kumfanya asimjibu lolote.

"Siwezi kuitawala dunia wala siwezi kuubadilisha ulimwengu, bali nichoweza kufanya ni kutema cheche zitakazofanya bongo za watu kuibadilisha dunia"..hii ndiyo kazi yetu tunayopaswa kufanya, kuamsha mtu mwingine anayetutazama".

Tupac alikiambia kituo cha televisheni cha MTV mwaka 1993 katika moja kati ya mahojiano yake yanayoendelea kukumbukwa mpaka leo. Quayle alishindwa vibaya katika kampeni ya kumaliza Tupac, lakini inaelezwa alichangia mno kupromoti mauzo ya kazi zake bila ya yeye kujua.

Watu mashuhuri mbalimbali waliyataja maneno hayo machache ya Tupac kama maneno bora zaidi kuwahi kutolewa na mtu "asiyetegemewa" na wengi kusema hivyo. Wengi waliyatumia kama rejea kwenye maeneo yao mbalimbali.

"Inawezekana baadhi yetu tusiwe watu wa kuibadilisha dunia, lakini tunapaswa kujaribu kila wakati kushawishi mtu mwingine kuchukua hatua zitakazoweza kuibadili dunia".

Maneno haya ya Tupac hata kwangu binafsi bado yanaishi sana.!

Itaendelea........[emoji3578]

#Balozi
Kuna element ya muhimu kwenye hii story umeiacha. Kwenye Source Music Awards Suge alipopanda kwenye stage na kusema "... Anybody who wants to be a star and not worry about the executive producer be all on the record, in the video, dancing. Come to Deathrow!" Tupac alikuwa ndio kwanza anakaribia kutoka jela na beef halikuwa serious.

Za chini ya kapeti zinasema kwamba baadaye kwenye after party ya Source Awards, Suge alimfuata Puffy na kumwambia "... I was just fucking with you nigga ..." Tatizo Puffy alimaindi kinoma.

Tarehe 23 September 1995 Suge na Puffy wakiwa entourages zao walihudhuria birthday bash ya producer Jermaine Dupri iliyofanyika Platinum Club, Atlanta. Ugomvi ukatokea kwenye parking ya magari kati ya makundi hayo mawili. Katika purukushani hizo mlinzi wa Puffy, Anthony "Wolf" Jones alichomoa bastola na kupiga risasi kadhaa ambazo baadhi zilimpata mshikaji wa Suge aliyeitwa Big Jake Robles, jamaa akadanja.

Kuanzia hapo uhasama ndio ukawa mkubwa sana. Vita ikakua toka Pac vs Biggie kwenda Bad Boy vs Deathrow kwenda East Coast vs West Coast.
 
Las Vegas ipo Nevada sio Texas, story yako haipo sawa kwa asilimia kubwa sana.
Yaani watu wanaongea pumba tupu humu. Eti Tupac aliuawa na Serikali. Really? Kwa impact gani aliyokuwa nayo kuitetemesha Serikali? You are giving him too much credit. Nataka mtu aniwekee kauli au lyrics au vitendo vya Tupac ambavyo viliitetemesha Serikali mpaka itake kumuua.
 
Toka lini muuaji akajichunguza mwenyewe ili ajikamate. FBI ndio wahusika wakuu wa hayo yaliotokea ndomana mpaka leo unaona kesi zinapigwa danadana. We kwa akili ya haraka haraka unaona shirika kubwa la upelelezi duniani kama FBI wangeshindwa kutambua wahusika wa mauaji ya ndani tena katika traffic light barabarani sio uchochoroni?
Pumba nyingine hii hapa. Vifo vya Tupac na Biggie ni state cases, FBI anahusikaje? Au hujui kazi za FBI? Polisi kwenye hizo states, LAPD na LVPD ndio wanapaswa kufanya upelelezi. Kujibu hoja yako kwa nini kesi hazijawa solved ni kwamba wahusika wote waliopaswa kutoa ushahidi walifuata street code, DON'T TALK TO THE POLICE. Sasa watu walioshuhudia hawataki kutoa ushirikiano unafikiri Polisi anafanya nini?
 
2pac kauliwa na Orlando Anderson, inafahamika from a street perspective, Biggie kauliwa na Suge Knight in retaliation. Wala sio code ngumu ku crack. Ila watu wasiojua sasaa.
 
Kuna element ya muhimu kwenye hii story umeiacha. Kwenye Source Music Awards Suge alipopanda kwenye stage na kusema "... Anybody who wants to be a star and not worry about the executive producer be all on the record, in the video, dancing. Come to Deathrow!" Tupac alikuwa ndio kwanza anakaribia kutoka jela na beef halikuwa serious.

Za chini ya kapeti zinasema kwamba baadaye kwenye after party ya Source Awards, Suge alimfuata Puffy na kumwambia "... I was just fucking with you nigga ..." Tatizo Puffy alimaindi kinoma.

Tarehe 23 September 1995 Suge na Puffy wakiwa entourages zao walihudhuria birthday bash ya producer Jermaine Dupri iliyofanyika Platinum Club, Atlanta. Ugomvi ukatokea kwenye parking ya magari kati ya makundi hayo mawili. Katika purukushani hizo mlinzi wa Puffy, Anthony "Wolf" Jones alichomoa bastola na kupiga risasi kadhaa ambazo baadhi zilimpata mshikaji wa Suge aliyeitwa Big Jake Robles, jamaa akadanja.

Kuanzia hapo uhasama ndio ukawa mkubwa sana. Vita ikakua toka Pac vs Biggie kwenda Bad Boy vs Deathrow kwenda East Coast vs West Coast.
Haujamalizia unajua umeishia katikati
 
2pac kauliwa na Orlando Anderson, inafahamika from a street perspective, Biggie kauliwa na Suge Knight in retaliation. Wala sio code ngumu ku crack. Ila watu wasiojua sasaa.
Kila mtu anajua kilichotokea. Tatizo ni kwamba ili mtu ashitakiwe na afungwe ni lazima kuwe na mashahidi. Sasa kama kila shahidi hataki kutoa ushahidi itakuwa kazi bure. Waendesha mashtaka hawawezi kupoteza muda wao kwa kesi ambazo wanajua hawatashinda.
 
Street code ni adui wa watu weusi marekani. Dumb thing.
 
Vifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.

Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.
Very possible serikali ilihusika kifo Cha Tupac wakijua Cha big kitafuata
 
Binafsi Naamini wengi wanaomzungumzia 2Pac na Biggie hapa walikuwa mashabiki wao kabla hata hawajauawa.
Mimi ni mmoja wapo mkuu. Ndio maana imekuwa rahisi kujua mengi kuhusu rapa huyo na mwenzake Big.
 
Vifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.

Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.
Ndo nasikia leo hii, mbna mpyaaa mweeeh
 
Huyo mwamba alikuwa anawachana kinomanoma kummqe,he feared no one
Anakwambia kinyume na Mungu, hakuna binadamu ambae anaweza kumfanya yeye amuogope hapa duniani.
Alimchana hadi baba yake mzazi, baada ya dingi kujaribu kumtafuta Pac ili watumie wote pesa zake, na wakati hakuhusika na malezi yake toka utotoni hadi ukubwani.
 
Wimbo unaitwa Get Money aliiba beat na Melody, huu wimbo pac alitaka kuutoa baada ya kutoka jela Ila kabla wimbo haujatoka Faith alivujisha kwa BIG na beat na Melody ilichukuliwa na Faith Evans ambae alikua anafanya ngoma na 2pac, BIG alipochukua ile Melody na beat akafanya na kundi lake jipya akaliita Junior M.A.F.I.A Ina maana yake na baada ya wimbo kutoka pac akawa amechukia maana Melody na beat ni ya kwake yeye kwa hio BIG aliiba ukiacha hivyo pac alikua na hasra alipopigwa risasi BIG alitoa wimbo unaitwa Who Shut You? Ikamuuma

Sasa baada ya BIG na Junior Mafia kutoa Get Money audio na video, pac alilalamika kua BiG kamkosea akasema isiwe kesi akaenda akafuta lyrics zoote za ile beat akatengeneza Diss Track pamoja na Crew yake yaan aliunda kundi na yeye akaliita Outlaws ambapo pindi inaundwa ilitambulika km Outlaw Immortalz yeye akiwa km Makaveli ambapo alikua anamhusudu mwanafalosofia Niccola Machiavelli akajiita pia Killuminati The Don (jina la album yake) na wengine ambao ni kundi aliloliunda wakiwa ni madikteta wa dunia, Big Marik aliejiita E.d.I Mean, na wengineo km Kastro alikua anajiita K-Dog huyu ni Fidel Castro wa Cuba, Yaki Kadafi huyu ni Gadafi wa Libya, Mutah ambae baadae alibadiri kua Napoleon, pia walitambulika km Thoro Headz and Young Thugz

Baada ya kuunda hilo kundi pac akaingia booth kutengeneza wimbo ambao hio Crew yake mwanzo hawakujua wimbo ni wa nini ndio akawaambia ni Diss Track na inaenda kumpaka Matope BiG na wale wote walio na ubia na BiG akiwemo P Diddy na Bad Boy Crew nzima pamoja na Junior Mafia

Wakatengeneza Diss Track inaitwa Hit 'Em Up hii ndio Diss Track kali ya muda wote, unaambiwa wakati Pac anaingiza vocal mic zilikua zinazima kila wakati na mmoja wa wale waliounda group ya Outlawz aliwahi kuhojiwa akasema pamoja na mic kuzima zima Pac hakuacha kurekodi na ilikua lazima arekodi hakuna wa kumzia hata producer wa ngoma nae anasema alipokua anatengeneza hio ngoma kulikua na changamoto km hizo Ila Pac hakutaka kurudi nyuma

Hatimae ngoma ikawa tayari wakatafuta watu wa Video wakashoot video baada ya hapo ikatoka kitu video & audio at the same time, na katika kava ya audio ya kwanza kabisa kwenye Tape waliweka picha ya BIG akiwa ni nguruwe kaveshwa kichwa Cha BiG na P Diddy akawekwa nyoka kaveshwa kichwa Cha P Diddy ngoma ikaachiwa

Baada ya kifo cha BiG Faith Evans aliewahi kua mke wa BiG alitoa wimbo wa kumbukumbu kwa BIG akiwa na P Diddy unaitwa I Will Be Missing You

Walale wanapostahiri uko walipo

R.I.P
Shukran kwa kutuongezea madini mkuu. Naamini yale ambayo yalikuwa hayafahamiki sasa yamefahamika kupitia comment yako.
 
KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO ? (4)
_______________

Inaendelea......

Kutokana na Tupac kuhitaji bosi wa Death Row, Marion 'Suge' Knight apambane kumtoa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja, Suge aliangaika huku na huko mpaka kufanikiwa kumchomoa Tupac jela.

Kiasi cha Dola Milioni 1.4 kilitolewa na Suge hivyo kufanikiwa kumtoa jela Tupac mwaka 1995, achilia mbali Dola 15,000 ambazo Suge alizitoa kumsaidia 'kishkaji' Tupac wakati akiwa jela.

Kimsingi Suge alikubali kujipukutisha fedha kwa sababu alijua kumwandika Tupac mkataba wa kumsimamia kupitia Death Row Records italipa. Knight alijua nini anafanya kwenye makubaliano hayo.

Makubaliano ya Tupac na Suge yakawa mazuri. Tupac akakubali kutengeneza albamu 3 chini ya Death Row Records lakini muda wote akihitaji Suge awe upande wake kwenye vita vyake dhidi ya Biggie.

Nyimbo ya kwanza ya Tupac kuitoa chini ya Death Row Records ikawa California Love. Kombinesheni ya Tupac, Dr Dre na Roger Troutman kwenye chorus ukawa unyama wa kufa mtu. Kwa hakika "The King was back from Jail''.

Ujio wa California love ulimtikisa kila mtu. Tupac alikuwa amejerea kuusimika upya ufalme wake uliotishiwa kuondoshwa kwa mtutu wa bunduki na vijana kutoka Pwani ya Mashariki (East Coast).

Marion Suge Knight na Tupac Shakur wakafanikiwa 'kuupika' mgogoro wa East Coast na West Coast ukapikika, mgogoro ambao chimbuko lake haswa ni chuki baina ya wasanii wawili, Notorious Big na Tupac Shakur.

Matatizo binafsi ya Biggie na Tupac yakajikuta yakirithiwa na hata wengine 'yasiyowahusu'. Wasanii wa East na West wakaonekana kuchukiana katika kiwango kilichotisha kabisa.

Wakati mgogoro huu ukikua na kuzidisha uhasama kwa wasanii, Serikali mwanzo ilionekana kama kupuuza, lakini kadiri hali ilivyozidi kuwa mbaya na viongozi walilazimika kusema chochote.

Lakini kabla ya kusema chochote, huko nyuma Tupac alikuwa ameshaingia kwenye mgogoro mara kadhaa na serikali kutokana na misimamo yake, harakati zake na maisha yake.

Nyimbo zake kupitia albamu yake ya 2Pacalypse ziliichefua sana serikali. Tupac alizungumzia zaidi Siasa, Ubaguzi na umasikini katika namna ambayo ilionekana kama kuchochea chuki kwa raia.

Mshtuko mkubwa ulitokea baada ya kijana mmoja mdogo kumpiga risasi polisi na kumuua kisha baada ya kukamatwa na kuhojiwa akathibitisha kufanya hivyo baada ya kusikiliza albamu ya Tupac iitwayo 2Pacalypse.

Tukio hilo lilikuwa gumzo nchini Marekani. Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Bw Dan Quayle akatangaza kupigwa marufuku kwa nyimbo za Tupac kusikilizwa kwenye Jamii ya wamarekani.

Bw. Quayle alisema Tupac ni msanii asiyefaa kabisa kusikilizwa. Nyimbo zake zimejaa chuki na kuchochea uovu kwenye jamii. Akaanzisha kampeni za kuhakikisha jamii inamchukia na haipati nafasi ya kumsikiliza Tupac.

Masikini Quayle hakuwa amejua kuwa wakati anasema hayo, Tupac alikuwa ameshaiteka sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani kuliko anavyodhani. Mahojiano yake na MTV ya mwaka 1993 yamlitosha kabisa kumfanya asimjibu lolote.

"Siwezi kuitawala dunia wala siwezi kuubadilisha ulimwengu, bali nichoweza kufanya ni kutema cheche zitakazofanya bongo za watu kuibadilisha dunia"..hii ndiyo kazi yetu tunayopaswa kufanya, kuamsha mtu mwingine anayetutazama".

Tupac alikiambia kituo cha televisheni cha MTV mwaka 1993 katika moja kati ya mahojiano yake yanayoendelea kukumbukwa mpaka leo. Quayle alishindwa vibaya katika kampeni ya kumaliza Tupac, lakini inaelezwa alichangia mno kupromoti mauzo ya kazi zake bila ya yeye kujua.

Watu mashuhuri mbalimbali waliyataja maneno hayo machache ya Tupac kama maneno bora zaidi kuwahi kutolewa na mtu "asiyetegemewa" na wengi kusema hivyo. Wengi waliyatumia kama rejea kwenye maeneo yao mbalimbali.

"Inawezekana baadhi yetu tusiwe watu wa kuibadilisha dunia, lakini tunapaswa kujaribu kila wakati kushawishi mtu mwingine kuchukua hatua zitakazoweza kuibadili dunia".

Maneno haya ya Tupac hata kwangu binafsi bado yanaishi sana.!

Itaendelea........[emoji3578]

#Balozi
Mkuu uchangiaji wako umekuwa wenye faida kwenye uzi huu. Endelea kuleta faida watu wajifunze.
 
Back
Top Bottom