Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Kisa Kafungwa na Yanga, makolo FC bwana .
 
Kamati ya Usajili yatakiwa iondolewe maana wamehusika kwa sehemu kubwa na huu upuuzi

Wasimuache Matola, huyu ndiye Nyoka kwenye Timu
Hivi huyu jamaa hana hirizi kweli?
Maana makocha hutimuliwa lkn yeye hubaki, nina wasiwasi na Matola.
 
Simba SC head coach Pablo Franco Martín has officially part ways with the Tanzanian club on a mutual agreement.

African Sports Today can confirm that Pablo is currently in negotiations with Amazulu FC 🇿🇦 and Raja Casablanca 🇲🇦 with Raja seems like the most preferred move.

Raja have offered the former Getafe coach $500,000 annual salary with other benefits while Amazulu is offering $25,000 Net monthly salary with a house, club car (with monthly fuel) and 2 business class tickets return (home) per season.
 
nabi kuanzia Sudan simba walimtaka ila alikuwa hajamaliza mkataba wake ,ile anamaliza simba wameshamchukua Gomes ,ndo maana Nabi alipofika Dar anahojiwa nawaandishi anasema Simba is the best club ,akaanza kukumbushwa upo Yanga. Hata hizi holidays alizokuwa anaenda wanasema anakwepa kurenew kwa sababu kuna ishu ya chini chini na Simba.
Mnampenda professor Nabi eeh

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
View attachment 2245636
Alitakiwa kwanza kuondoka Mtendaji mkuu(CEO) Yeye ndio chanzo cha kuporomoka kwa Simba! mengine yote ni kuficha tu udhaifu wa CEO timu haina hamasa kabisa
Yametimia, muda umeongea
 
nabi kuanzia Sudan simba walimtaka ila alikuwa hajamaliza mkataba wake ,ile anamaliza simba wameshamchukua Gomes ,ndo maana Nabi alipofika Dar anahojiwa nawaandishi anasema Simba is the best club ,akaanza kukumbushwa upo Yanga. Hata hizi holidays alizokuwa anaenda wanasema anakwepa kurenew kwa sababu kuna ishu ya chini chini na Simba.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah.
 
Back
Top Bottom