TANZIA Padre Ireneus Mbahulira amelala usingizi wa umauti akipatiwa matibabu Hospitali ya Mugana

TANZIA Padre Ireneus Mbahulira amelala usingizi wa umauti akipatiwa matibabu Hospitali ya Mugana

Magonjwa (baadhi) ambayo pia husababisha kupumua kwa shida:
asthma, pneumonia, pneumothorax, anemia, lung cancer, inhalation injury, pulmonary embolism, anxiety, COPD, high altitude with lower oxygen levels, congestive heart failure, arrhythmia, allergic reaction, anaphylaxis, subglottic stenosis, interstitial lung disease, obesity, tuberculosis, epiglottitis, emphysema, pulmonary fibrosis, pulmonary artery hypertension, pleurisy, croup, polymyositis, Guillain-Barré syndrome, sarcoidosis, rib fracture, carbon monoxide poisoning, and aerobic exercise.

Kuna nini kila kupumua kwa shida na kifo vinahusishwa na corona? Nadhani ifike hatua tuwaachie wataalam wetu kazi ya kuthibitisha mgonjwa anaumwa nini!
 
Raha ya milele umpe "Eeeh Bwana" na Mwanga wa milele umwangazie "APUMZIKE KWA AMANI"
 
Bukoba. Padri Ireneus Mbahulira (80) wa jimbo Katoliki Bukoba amefariki dunia katika hospitali ya Mugana wilaya ya Misenyi akipatiwa matibabu.

Akizungumza jana Jumamosi Januari 23, 2021 Askofu msaidizi wa jimbo hilo, Methodius Kilaini ameieleza Mwananchi Digital kuwa kifo cha Mbahulira kimetokea Januari 22, 2021 katika hospitali ya Mugana Wilaya ya Misenyi alikokuwa amelazwa wiki moja iliyopita.
Amesema katika matibabu mbali na kuwekewa dripu kadhaa, padri huyo aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Amesema padri huyo alizaliwa mwaka 1942 na mwaka 1969 alipata daraja la upadri na alihudumu kama paroko Jimbo la Bukoba Parokia ya Buyango Wilaya ya Misenyi.

"Mwaka 2018 aliamua kurudi nyumbani ambapo alipangiwa Parokia ya Rukindo wilaya ya Muleba baadaye alihamishiwa Minziro wilaya ya Misenyi, " amesema Kilaini
Amesema mazishi yatafanyika Jumatatu Januari 25, 2021.

Source: Padri Mbahulira afariki dunia | Mwananchi
 
Ufu 14:13

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Wazungu sasa wanatumia kila njia ili kutaka kutuuzia chanjo yao ya korona. Sisi tunaendelea kuchapa kazi tukimtanguliza Mola.
 
Mpaka jana, Zimbabwe mawaziri 4 wamefariki na kuthibitishwa kuwa wamefariki kwa tatizo la Covid 19, huku wengine kadhaa wakiwa katika hali mbaya hospitalini.

Kati ya waliofariki hiyo juzi, mmoja ni Kabudi wao wa huko.
Hata huku vifo vitafika wee subiri kidogo, hasa hao wanaopokezana mike
 
R.I.P Padre lakin me nashangaa kwa baadhi ya watu kuunganisha matukio ya vifo na corona kila anayekufa now kila mtu ni corona hili jambo sio zuri na linaleta taharuki sana

Unaogopa taharuki au Corona?
 
Back
Top Bottom