PostGE2025 Padre Kitima: Kanisa lilionya kutofanya uchaguzi kabla ya kurekebisha kasoro za uchaguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema viongozi wa Kanisa hilo walitoa tahadhari mapema kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu hatari ya kutorekebisha kasoro za uchaguzi, akieleza kuwa walionya kuwa hali hiyo ingeweza kusababisha maafa nchini.

Akizungumza wakati wa misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025, Padre Kitima amesema Januari 8, 2024, Maaskofu walikutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM mjini Dodoma na kumweleza wasiwasi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi, wakirejea changamoto walizoziona katika chaguzi za mwaka 2019 na 2020.

Amesema katika mazungumzo hayo, kiongozi huyo wa CCM aliwaahidi kuwa masuala waliyoyawasilisha yangefanyiwa kazi ili yasijirudie, lakini baadaye walishuhudia matukio ya kutoweka na kuuawa kwa baadhi ya watu, hali iliyozidisha wasiwasi wao kuhusu usalama na mwenendo wa siasa nchini.

Amesisitiza kuwa toba ya kweli inahitaji kuondokana na kiburi na kupanda mbegu za ukweli, unyenyekevu na upendo, akieleza kuwa hayo ndiyo msingi wa msamaha na maridhiano ya kweli katika jamii.
 
waislam walionya kutoandamana...............hivyo yaani, kanisa wasitafute huruma wataenda kujibu kwa allaah waliyoyafanya.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema viongozi wa Kanisa hilo walitoa tahadhari mapema kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu hatari ya kutorekebisha kasoro za uchaguzi, akieleza kuwa walionya kuwa hali hiyo ingeweza kusababisha maafa nchini.

Akizungumza wakati wa misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025, Padre Kitima amesema Januari 8, 2024, Maaskofu walikutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM mjini Dodoma na kumweleza wasiwasi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi, wakirejea changamoto walizoziona katika chaguzi za mwaka 2019 na 2020.

Amesema katika mazungumzo hayo, kiongozi huyo wa CCM aliwaahidi kuwa masuala waliyoyawasilisha yangefanyiwa kazi ili yasijirudie, lakini baadaye walishuhudia matukio ya kutoweka na kuuawa kwa baadhi ya watu, hali iliyozidisha wasiwasi wao kuhusu usalama na mwenendo wa siasa nchini.

Amesisitiza kuwa toba ya kweli inahitaji kuondokana na kiburi na kupanda mbegu za ukweli, unyenyekevu na upendo, akieleza kuwa hayo ndiyo msingi wa msamaha na maridhiano ya kweli katika jamii.
Hili ni kanisa ambalo lilikuwa likishiriana bega kwa bega na uhalifu wa wakoloni barani Afrika, ikiwemo Tanzania. Hata sasa ni kichaka cha kujifichia majasusi, vibaraka wa Magharibi. Linafadhili usimikaji wa viongozi wenye maslahi kwa kanisa na nchi za Magharibi. Nyerere, Mkapa na Magufuli kuwa wakatoliki wote sio kitendo cha bahati mbaya tu (chance).
 
Huyu mwamba anajitahidi kujisafisha sana lakini wapi. Inabidi atubu tu, maneno yake yalisababisha madhara makubwa ambayo hakuyategemea

Laana yote ya damu za Watanzania ipo mikononi mwa watawala na CCM.
Watu wote wema walionya na kushauri kwa upendo na uzalendo mkubwa kwa Taifa letu. Wazee wenye hekima walionya na kutoa ushauri wao. Viongozi wa CHADEMA waliomba uchaguzi uahirishwe, kiongozi aliyekuwepo aendelee kuongoza, asimamie mabadiliko yatakayowezesha uchaguzi uwe wa kweli, na siyo bandia kama ambavyo ilikuwa kwenye uliotangulia. Lakini watawala na CCM, wakiwa wamejawa na roho ya shetani, wakajawa na kiburi. Badala ya kutafakari na kufanya marekebisho muhimu ili watanzania waende kwenye uchaguzi wakiwa na umoja, upendo na shauku, wakabakia kujiandaa na vitendo viovu vya kuteka watu, kuua watu, na kisha kujipachika madarakani kwa nguvu. Hawa ndiyo chanzo cha damu za watanzania zilizomwagika.
 
"""LISSU,HECHE,CATHOLICS WALIONYA""

INACHEKESHA SANA,YAANI TAASISI ZINAINGILIA RATIBA ZA UCHAGUZI AMBAO UPO KIKATIBA!...

WALIPOONA HAWASIKILIZWI BAADHI WAKAJIAPIZA KUZUIA UCHAGUZI NA IKIBIDI KUASI,

YAANI UNAUZUIA MFUMO WA SEREKALI USIFANYE KAZI.
 
Hili ni kanisa ambalo lilikuwa likishiriana bega kwa bega na uhalifu wa wakoloni barani Afrika, ikiwemo Tanzania. Hata sasa ni kichaka cha kujifichia majasusi, vibaraka wa Magharibi. Linafadhili usimikaji wa viongozi wenye maslahi kwa kanisa na nchi za Magharibi. Nyerere, Mkapa na Magufuli kuwa wakatoliki wote sio kitendo cha bahati mbaya tu (chance).

Jihesabie kuwa wewe ni mwendawazimu wa kiwango cha pekee! Taja japo tukio moja ambalo Kanisa lilishirikiana na watawala wa kikoloni kuwafanyia uovu wanadamu. Nina uhakika, huna.

Kanisa ndilo lilimshauri Mwalimu Nyerere asiache kuwaongoza Watanganyika katika kuupata uhuru wao, hiyo ni baada ya Mwalimu Nyerere kuambiwa na Serikali ya kikoloni kuwa achague moja: kuacha uwalimu, aendelee na siasa, au aache siasa aendelee na siasa. Ilimchanganya sana Mwalimu Nyerere. Akiacha uwalimu, ataitunza vipi familia yake wakati kwenye TANU hana mshahara: Kanisa likamwambia kuwa lenyewe litaitinza familia yake. Familia ya Mwalimu Nyerere ikachukuliwa ni shirika la masisita la Mt. Consolata, mke na watoto wakapelekwa nyumba ya masisita Tosamaganga. Na ni shirika la watawa wa Consolata ndilo lililipia ticket ya Mwalimu Nyerere kwenda UN, huku yule mzee wa Mwanza na Dar wakichangia gharama za hotel na chakula atakapokuwepo nje ya nchi.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema viongozi wa Kanisa hilo walitoa tahadhari mapema kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu hatari ya kutorekebisha kasoro za uchaguzi, akieleza kuwa walionya kuwa hali hiyo ingeweza kusababisha maafa nchini.

Akizungumza wakati wa misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Oktoba 29, 2025, Padre Kitima amesema Januari 8, 2024, Maaskofu walikutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM mjini Dodoma na kumweleza wasiwasi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi, wakirejea changamoto walizoziona katika chaguzi za mwaka 2019 na 2020.

Amesema katika mazungumzo hayo, kiongozi huyo wa CCM aliwaahidi kuwa masuala waliyoyawasilisha yangefanyiwa kazi ili yasijirudie, lakini baadaye walishuhudia matukio ya kutoweka na kuuawa kwa baadhi ya watu, hali iliyozidisha wasiwasi wao kuhusu usalama na mwenendo wa siasa nchini.

Amesisitiza kuwa toba ya kweli inahitaji kuondokana na kiburi na kupanda mbegu za ukweli, unyenyekevu na upendo, akieleza kuwa hayo ndiyo msingi wa msamaha na maridhiano ya kweli katika jamii.
Let me confirm to you Fr.Kitima without fear of contradictions,

Uchaguzi mkuu wa TANZANIA utafanya kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kila baada ya miaka mitano bila kuzingatia onyo au ushauri wa kinafiki wa kanisa lako.

Endeleeni kuchochea na kuhamasisha chuki, uhasama, ghasia na mafarakano miongoni mwa waTanzania, huenda huo ndio wito wenu katika upadre mlio nao, lakini serikali haiwajibiki kwa kanisa katoliki pekee , bali kwa waTanzania wote bila kujali dini, rangi au makabila au makabila yao.

Na ni vizuri ukafahamu hili kwamba,
ni matakwa ya waTanzania wote tu ndio yatazingatiwa na na kufanyiwa kazi na serikali sikivu ya CCM ambayo ndio ina dhamana ya umma katika kuongoza nchi, lakini sio matakwa ya kinafiki ya kanisa katoliki.
By the way, who are you in this very beautiful, united and peaceful country?🐒
 
Hili ni kanisa ambalo lilikuwa likishiriana bega kwa bega na uhalifu wa wakoloni barani Afrika, ikiwemo Tanzania. Hata sasa ni kichaka cha kujifichia majasusi, vibaraka wa Magharibi. Linafadhili usimikaji wa viongozi wenye maslahi kwa kanisa na nchi za Magharibi. Nyerere, Mkapa na Magufuli kuwa wakatoliki wote sio kitendo cha bahati mbaya tu (chance).
Mimi nilijua kuwa na akili ni kuongoza mtihani darasani,badaye nilipokuwa kijana nikajua kuwa na akili ni kuwa na hera au kuwa kiongozi
Nilipokuwa mtu mzima nikajua akili haihusiani na kuongoza darasani,au pesa na vyeo akili ni busara pesa cheo bila akili ni bure na busara hupimwa na watu
 
Hili ni kanisa ambalo lilikuwa likishiriana bega kwa bega na uhalifu wa wakoloni barani Afrika, ikiwemo Tanzania. Hata sasa ni kichaka cha kujifichia majasusi, vibaraka wa Magharibi. Linafadhili usimikaji wa viongozi wenye maslahi kwa kanisa na nchi za Magharibi. Nyerere, Mkapa na Magufuli kuwa wakatoliki wote sio kitendo cha bahati mbaya tu (chance).

Ni punguani pekee anayeweza kushangaa kwa marais wengi waliopita walikuwa Wakatoliki, au kwa nini marais waislam huwa ni Wasuni. Wakatoliki ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini kuliko yote. Kwa waislam, wasuni ni wengi kuliko makundi mengine ya waislam, lakini ni wachache sana ukikinganisha na wakatoliki. Kama ungekuwa umesoma hesabu, na ukawa na uelewa na akili japo kidogo, ungefahamu kuwa probability kubwa siku zote huangukia kwenye kundi kubwa zaidi: ni sawa udondoshee punje 100 za maharage ndani ya ndoo, kati ya hizo 100, 70 ziwe nyeusi, 20 nyeupe, 10 nyekundu. Zikachanganywa, halafu ukaambiwa utumbukize mkono wake kwenye container utoe punje moja, probability kubwa zaidi ni kuwa utaibuka na punje nyeusi. Hata hiyo hujui?
 
"""LISSU,HECHE,CATHOLICS WALIONYA""

INACHEKESHA SANA,YAANI TAASISI ZINAINGILIA RATIBA ZA UCHAGUZI AMBAO UPO KIKATIBA!...

WALIPOONA HAWASIKILIZWI BAADHI WAKAJIAPIZA KUZUIA UCHAGUZI NA KIBIDI KUASI,

YAANI UNAUZUIA MFUMO WA SEREKALI USIFANYE KAZI.
ndio maana nasisitizaga sana humu jukwaani kwamba kanisa katoliki lilihusika moja kwa moja katika kupanga, kuhamisha na kuchochea kilichotokea Oct 2025. Nadhani naanza kueleweka kwa kauli hiyo ya fr.Kitima

Bado kidogo Fr. Kitima ataeleza alivyoshiriki yeye mwenyewe kibinafsi katika ghasia zile, sasaivi naona bado anajificha ficha nyuma ya kanisa, but lazima atafunguka tu as time goes 🐒
 
RC wajitafakari, wafanye toba ya kweli na waache viburi.

RC litaendelea kupokea neema toka Mungu kwa sababu halijawahi kuwa kanisa la kinafiki. Watumishi wake, wakati wote wameendelea kusimama katika kweli ya Bwana bila woga wala kujali madhira wanayotengenezewa na wauaji. Mungu wetu, ni Mungu wake, atambariki yeyote anayesimama katika haki na kweli.
 
Back
Top Bottom