Padre Titus Amigu anasema muda huu kupitia Radio Maria kuwa viongozi wakuu wa nchi wanajua wauaji ni akina nani

Padre Titus Amigu anasema muda huu kupitia Radio Maria kuwa viongozi wakuu wa nchi wanajua wauaji ni akina nani

Sikiliza Radio Maria muda huu Padre Titus Amigu anaponda viongozi wetu kwa kutowahibika ipasavyo katika kuwalinda wananchi. Anasema viongozi wetu wanawafahamu watekaji na wauaji hao.
Yuko sahihi huyo Padre, kwa sababu kauli zao hao viongozi zinathibitisha kuhusu suala hili.

Nafikiri Rais awe mwangalifu sana katika kuchagua maneno au lugha ya kuongea mbele za hadhara za Watu, asiwe anaamini kila kitu anachoambiwa na wale Watu wanaomzunguka. Sometimes anadanganywa au amekuwa akiambiwa Habari ambazo zimetiwa chumvi Sana. Awe anachuja maneno ya kuongea hadharani.
 
Tatizo kuu la serikali na jeshi la polisi ni ukosefu wa ufuatiliaji wa haraka na utoaji wa ripoti sahihi kwa wananchi.

Ripoti nyingi zinazotolewa zimejaa mashaka na kutokuaminika. Hali hii inachangia katika kuvuruga imani ya umma na kuonesha jinsi jeshi la polisi linavyokosa ufanisi na kuwa na matatizo ya kiutendaji.
 
Sikiliza Radio Maria muda huu Padre Titus Amigu anaponda viongozi wetu kwa kutowahibika ipasavyo katika kuwalinda wananchi. Anasema viongozi wetu wanawafahamu watekaji na wauaji hao.
Watafanywa kama walivyofanywa kule Congo na Tshisekedi,,,,,walijifanya kuingilia siasa za nchi ila mwisho wao kilichowakuta ni aibu
 
Yuko sahihi,kama hawajui basi hawafai kuwa pale maana waneshindwa kulinda raia wao
Kwani lazima wawajue hapo hapo si ndio maana unafanyika uchunguzi!!? Uchunguzi ndio utaleta majibu sahihi siyo propaganda za wanasiasa uchwara. Kumbuka Dr. Slaa alishasema Chadema huwa wanateka watu hata juzi Mbowe mwenyewe amesema anateka wanachama wake wasiowaaminifu kwa chama. Msikilize hapa kwenye video clip hapa chini.
 
Sikiliza Radio Maria muda huu Padre Titus Amigu anaponda viongozi wetu kwa kutowahibika ipasavyo katika kuwalinda wananchi. Anasema viongozi wetu wanawafahamu watekaji na wauaji hao.
Kwani na yeye hajjui? Kuwa kuna Padre mwenzie Geita anahusika kuteka na kuua mtoto Albino na kumkatakata viungo
 
Hii ndo raha na uzuri wa kuwa na viongozi wa dini wasomi. Ndio maana RC huwa wanatoa point sana sababu hakuna Padre ambae hajapiga shule.

Ndo maana huwez kuta Padre wa RC anatoka nje na kusema upumbavu et kila serikali duniani ina wauaji... So tuendelee kuuliwa au?
 
Ni ujinga kuwakatisha tamaa viongozi wa dini wanaohoji usalama wa wananchi. Vijana wa leo mnapata wapi akili hizi hafifu?
Kama wanatumika na mabeberu nao wembe ni ule ule,,,,DRC walishaonyesha njia na wakaufyata hizi zama sio za kuwaendekeza vibaraka wa wazungu
 
Kulijua hilo wala halihitaji D mbili isipokuwa A+ ya ujasiri wa kusema ukweli bila kumung'unya maneno.
Fr amesema kweli tupu. Rejea hotuba ya mgeni rasmi kule CCM Kalangalala Geita, CCP, katazo la kujadili utekaji bungeni. Yote haya yanafungua kodi viongozi wetu wanawajua watekaji na wanawagwaya au la.
 
Back
Top Bottom