Padre wa Kanisa Katoliki Italia afukuzwa baada ya kuhubiri kwamba Papa Francis ni 'Masonic' na 'Anti-pope'

Padre wa Kanisa Katoliki Italia afukuzwa baada ya kuhubiri kwamba Papa Francis ni 'Masonic' na 'Anti-pope'

Nipo deep kuliko unavyodhani mkuu,
Ungekuwa upo deep kiasi cha kuyajua mengi kunishinda ungeshanielewa pale juu nilipokwambia uombe hekima kwanza ndiyo ujadili haya mambo ya imani.

Imagine huijui hata sekunde moja ya pumzi yako lakini unathubutu kusema hapa kwamba watu fulani ni wa shetani,who are you bro?mimi nitaenda motoni unajuaje kama nitaenda motoni mzee?just kwa sababu ni Mkatoliki?umeujuaje utendaji wa Mungu?umeijuaje hekima ya Mungu ktk kuwahukumu wale waliojitahidi au kujaribu kumtafuta lakini wakawa hawapo sehemu sahihi?

Usijimilikishe wewe ukuu,Mungu ana taratibu zake siyo mimi wala wewe anayezijua itoshe kusema tusali kwa imani zetu tukingoja yajayo hakuna mwenye mamlaka ya kumuhukumu mwenzake.
 
Acha kuandika bila kufuatilia mambo. Francis alipoingia amewatoa wadhifa watu wengi waliokua wanampinga au kuonesha kumpiga, wamewekwa watu wanaitwa 'mercenaries wake' sasa hao wao ni wanatishia sana.

Tamko la vatican ni la baraza, sio la papa lkn ni baraza ambalo limejazwa watu aidha waliokengeuka tyr au waliotishwa, unategemea watapinga?
duuu vatikan haikosei ikitamka ndo ilivo ...walipinga wakina luther wakauwawa sasa s sembuse hawa wameachwa hai....mtaguso mkuu wa 2 wa vatikan unasema papa hakosei...na roma haibadiliki...ww ndo umeivamia vatikan...meng yatakuja makubwa .
 
Ila kusema kweli dunia ya leo inahitaji kujenga imani kwenye Neno na sio wote wanaoitwa watumishi wa Mungu wanafanya maagizo ya Mungu.

Kuna nyakati ni tete usipokuwa makini unadondokea shimoni maana unaongozwa na kiongozi kipofu.

Binafsi ni Mkristo ambaye niko huru, sibanwi na mapokeo ya dhehebu flani au kiongozi flani bali ninabanwa na neno la MUNGU MKUU lililo kwenye bible.

Kwa hiyo hata kiongozi wa kiimani akifanya matendo ya kishetani hata hainiumizi chochote kwa vile sina tumaini juu ya mwanadamu, ila kikubwa zingatia andiko hili,

Yohana 17:3​

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Upo sahihi sana ktk hili.
 
Kanisa na imani yetu haitayumba kwani tumelelewa kwny misingi imara..huyo papa hawezi kututeteresha..atapita na yy kama walivyopita wengine waovu na kanisa bado liko pale pale...kuna waves kwenye maisha ya imani ni jukumu letu kusimama imara...
Nitakiri imani yangu ya kanisa katoliki mpk kufa...
 
Papa benedict sijui ni nini tu kilimlazimu kujiudhuru, na ukicheki francis kasubiri benedict afe ndio afanye yake.

Kuna kardinali mmoja alisema pala benedict kpnd anajiudhuru alidhan hatoishi hata zaidi ya mwaka
Alikaa karibu miaka 10 baada ya kujiuzulu, tena akiwa na afya nzuri tu.
 
Kanisa na imani yetu haitayumba kwani tumelelewa kwny misingi imara..huyo papa hawezi kututeteresha..atapita na yy kama walivyopita wengine waovu na kanisa bado liko pale pale...kuna waves kwenye maisha ya imani ni jukumu letu kusimama imara...
Nitakiri imani yangu ya kanisa katoliki mpk kufa...
Asante sana , Let us be proud of our Catholicism.
 
Kanisa na imani yetu haitayumba kwani tumelelewa kwny misingi imara..huyo papa hawezi kututeteresha..atapita na yy kama walivyopita wengine waovu na kanisa bado liko pale pale...kuna waves kwenye maisha ya imani ni jukumu letu kusimama imara...
Nitakiri imani yangu ya kanisa katoliki mpk kufa...
Uwe unakiri imani ya Mungu ili uwe na uzima wa milele siku yako ikiwadia sio kuweka imani kwenye kanisa pekee.

Ndani ya kanisa lolote kuna sintofahamu nyini, hivyo unaweza jikuta unawekeza tumaini kwenye mapokeo yaliyowekwa na wanadamu ukasahau kuimarisha uhusiano wako binafsi na YEHOVA.

Hakuna kanisa linalompeleka mtu mbinguni bali imani thabiti iliyojengwa juu ya Neno la Mungu kupitia kwa Yesu Kristu.

Yohana 17:3​

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
 
Fr. Ramon Guidetti wa Italy amefukuzwa tar 3 January 2024 baada ya kuhubiri kwamba papa francis anakinajisi kiti cha Mtume Petro (anti-pope) na anatimiza matakwa ya wapinga Kristo.

Hio ilitokea alipokua anahubiria tarehe 31 December 2023 siku iliokua ni kumbukizi ya kifo cha Papa Benedicto wa 16. Alienda mbali zaidi na kusema kwamba Papa Benedicto ndie alikua papa wa kweli lkn huyu wa sasa ni 'Antipope and masonic jesuit'

Ikumbukwe pia wakuu kadhaa ndani ya roman catholic walitumia siku ya trh 31 ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha papa benedicto wa 16 kutoa yao ya moyoni dhidi ya uendeshaji potofu wa papa francis wakiwemo makardinali wawili waliokua karibu sana na papa benedicto wa 16

Soma zaidi hapa Italian priest excommunicated for slandering Pope Francis during Mass

Maoni yangu, mapadri, maaskofu wote wanaofukuzwa wafungue kanisa jipya ambalo litafuata kanuni za conservative catholics lkn tu lisimtambue papa kama walivyofanya orthodox, wakifungua hilo kanisa mimi nitakua muumini wa kwanza hapa Tanzania, huyu papa wa sasa 'Tumepigwa'
Fara wewe
 
Uwe unakiri imani ya Mungu ili uwe na uzima wa milele siku yako ikiwadia sio kuweka imani kwenye kanisa pekee.

Ndani ya kanisa lolote kuna sintofahamu nyini, hivyo unaweza jikuta unawekeza tumaini kwenye mapokeo yaliyowekwa na wanadamu ukasahau kuimarisha uhusiano wako binafsi na YEHOVA.

Hakuna kanisa linalompeleka mtu mbinguni bali imani thabiti iliyojengwa juu ya Neno la Mungu kupitia kwa Yesu Kristu.

Yohana 17:3​

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Sawa...
 
Maoni yangu, mapadri, maaskofu wote wanaofukuzwa wafungue kanisa jipya ambalo litafuata kanuni za conservative catholics lkn tu lisimtambue papa kama walivyofanya orthodox, wakifungua hilo kanisa mimi nitakua muumini wa kwanza hapa Tanzania, huyu papa wa sasa 'Tumepigwa'
Utakuwa hauna tofauti na waprotestant ambao kwao hata wakitofautiana mavazi wanaanzisha kanisa jipya
 
Uovu upi uliomchukiza Mungu hadi kuiteketeza dunia kwa moto zaidi ya ushoga na gharika enzi za Nuhu?
Nasisitiza, kulikuwapo Mapapa waovu zaidi ya huyu lakini walipita na kanisa likasimama. Ni kwa kuwa watu mpo wavivu tu wa kusoma
 
Mungu gan tena?? . .... ..POPE maana yake n baba mtakatifu yaan (mungu wa wakatoliki wote)...nimetoka milembe juz sjamaliza dozi
Ni kweli,kupitia maneno yako nimeiona hiyo shida waliyokupeleka nayo huko Milembe.

Mungu na akupe uponyaji wake urudi ktk hali yako ya kawaida.
 
Jamaa wameamua kumwambia kwamba hawaungi mkono hiko. Huu ndio mwanzo wa UAMSHO mpya ndani ya RC.
 
Back
Top Bottom