Nitalijibu kwa kirefu kidogo
Ukiachana na imani ya kale ya Wamisri kwamba kumlaza marehemu kifudifudi ni dharau kubwa kuna hizi dhana hapa
1. Dhana ya mbingu na kuzimu
Imani zote zinaongelea maisha baada ya kifo na kwamba mbingu iko juu na kuzimu kuko chini ...hivyo unamlaza marehemu kuelekea kule atakakokwenda
2. Roho inapouacha mwili mawasiliano mengine yote ni kupitia jicho lionalo kwenye ulimwengu usioonekana, hapa kazi ya macho yatazamayo hukoma. ..hivyo kulaza kifudifudi ni sawa na kuliziba
3. Binadamu tumeumbwa kusimama, na ku move kuelekea mbele na si kinyume chake hatuendi kinyume nyume kwahiyo hata mawasiliano yetu ya kiroho ni ya kufunguka angani na si chini ya ardhi
4. Kuna jinsi nyingine za kumuweka marehemu kama kumsimamisha, kumkalisha kumlaza ubavu ubavu lakini kamwe si kifudifudi