Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Watu mnaenda nje ya mada na mnakuwa na mihemuko tu.Hivi unaelewa mleta mada anaongelea nini?? Yeye hajakataa kukopa au hajasema dhuluma ni mbaya - anawakomesha hawa wanaotumia app..wanao-access contacts zote kwenye simu ya mteja na wanawatumia sms watu wote kinyume na utaratibu.
Unafikiri hili suala ni sawa????


Hamna emotional yoyote hapa Mkuu Tatizo watu hatupendi UKWELI ila anachokifanya jamaa hawakomeshi hao watu ila anajikomesha yeye mwenyewe na MAISHA yake


Angelipa deni lao kwa muda waliokubaliana yasingetokea hayo yote Mkuu


Hujawahi kusikia ule msemo wa wahenga usemao


"Cha MTU mvi"

Ndio hayo yanamnukia mwenzako sasa harafu yeye anafanya kuikimbia harufu kumbe yamepakwa mwilini mwake
 
Aliekuambia kampun Yao inategemea hyo elfu ishirini uliyozulumu kujiendesha nani..???

Umepunguza kijiko Cha chai kwenye pipa la maji afu unajisifia umemaliza maji kwenye pipa...wewe ni tapeli TU kama matapeli wengine hapa unatafuta uhalali wa ujinga wako...

Hela ndogo kama hyo huwez kuikomesha kampuni yenye mtaji wa billion na zaidi...zaid unajikomesha mwenyewe kujiingiza kwenye vifungo vya nafsi usivyovijua sabb kichwan upo empty!!!

Hao unaowajibu ni waajiriwa TU kwenye hzo kampun wanatimiza wajibu wao na mwisho wa siku wanalipwa mishahara Yao..ila kampun itabaki kustaw bila kujal loss ndogo kama hzo...
kumbe inawauma eeh ?? hapo bado hamjasema 😂😂😂
 
Acha ujuaji mwingi wewe.
Benki hawawezi kukosa kukopesha kisa eti kideni cha pesa X au kisa kitangazo cha pesa X kuwa wewe tapeli.
Ukienda benki watakutajia vigezo ukitimiza wataitazama dhamana basi mkopo unaingia kwako.

Pia acha mihemko kama mtoto wa kike kiasi unamuita mwenzio mpumbavu,we unaona ni sawa kumtangaza mtu tapeli na kuvunja privacy yake!?
Hivi hujui kuwa hilo ni kosa la jinai!?
Hivi hujui hao wawili wakisimama mahakamani mtoa mada anashinda kesi na atatakiwa kulipwa fidia!?

Ujuaji mwingi kumbe dunderhead!
hiki ndio najua mimi embu mueleze uyo kwaiyo bank wakatae kunikopesa m10 kwa dhamana ya nyumba kisa nadaiwa elfu saba na pesa X 🤣🤣🤣
 
hiki ndio najua mimi embu mueleze uyo kwaiyo bank wakatar kunikopesa m10 kwa dhamana ya nyumba kisa nadaiwa elfu saba na pesa X 🤣🤣🤣
Yani nimemuona bonge fala huyo jamaa.
Alichozingua karopoka sana mineno ya ujuaji miiingiiii halafu kichwani sifuri.
Yani NBC au CRDB washindwe kukukopesha kisa deni la mkopo Fasta ama kisa mkopo Fasta kapost picha yako mtandaoni na kuandika wewe tapeli!!???
Jinga kabisa huyo.
 
Mimi mgodi Wana salamu zangu. Sidhani kama watakaa wanikopeshe Tena. Waliponipigia simu nikawaambia Mimi mwanafunzi hata ada nimekula naomba mnikopeshe Tena nilipe ada😂😂

Nilipo ona simu zinazidi Kila Leo nikawaambia sikuwalazimisha kabisa mnikopeshe Wala sikujaza form ya mkopo.
 
Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,

Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona, nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

Kweli nilichukizwa kwa kifupi nilikwazika na kughafilika sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

Usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
Aaahaaa
 
Nielekeze hiyo mkuu unafanyaje !?
Kwenye call setting katafte huko utaikuta call barring.

Ila madhara yake ni kwamba hutopigiwa simu na yeyote wala kupokea sms kutoka kwa yeyote.

Ila wewe uwezo wa kupiga na kutuma sms utakuwa nao ikiwa hivo hivo kwenye call barring.

Hivyo kama laini ndiyo hiyo tu moja unaitegemea kwa mawasiliano na watu wa muhimu sitokushauri uweke hii setting, unless laini iwe haina issue sana kwako.

Lakini pia unaweza kujaribu "call fowarding" huko huko kwenye call settings then unaenda sehemu imeandikwa "always foward" itakuomba uingize namba then utaingiza namba ambayo si ya kitanzania mfano +2555 una save.

Watu wakikupigia wataambiwa namba wanayopiga haipo, japo kwenye sms wakituma zinafika na mchart kama kawaida.

Au option nyingine unaenda playstore una down load "call blocker".

Then unaifungua unaenda kwenye setting yake kwenye "block all unkown call, private number & hidden ID number" unaweka "ON" pote pale.

Kitakachotokea ni kwamba namba yeyote ambayo utakuwa hujaisevu kwenye simu yako wewe haitakuwa na uwezo wa kukupigia (yaani namba ngeni), zita blockiwa automatically hivo hakuna fala yeyote atakae kusumbua.

Na kwenye sms setting unaenda kwenye "sparm sms" unaweka "ON" ili hata wakituma sms zao za vitisho wewe hutoziona.

Hivyo ndivyo mimi huwa nadhibiti usumbufu wa hawa mafala wanao kopesha kausha damu zao mtandaoni.
 
Mbna mnatudai na hatuwalipi na tunakopeshwa na bank acheni uboya benki wanaakili sio kama nyinyi wapumbafu..
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandao
 
Back
Top Bottom