Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,

Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona, nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

Kweli nilichukizwa kwa kifupi nilikwazika na kughafilika sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

Usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
Mkuu ungei reset simu ili app yao ifutike na Google account yako ifutike.
Maana kupitia Google acc yako ambayo umri allow wapate access katika simu yako wana uwezo wa kuona contacts na hadi picha zako.
Kaka reset simu wanaweza kuaibisha zaidi.
 
Kudhulumu pesa ya mtu sio ujanja

Wala kupost screenshots za wadai wako ambazo zinaonesha majibu ya kejeli ukiwavimbia wanapokuhimiza ulipe deni lao.

Guys hiyo sio right move kwa mtu ambaye ni smart.

Labda itakuwa ni ishu ya makuzi tu, ila mimi binafsi yangu siwezi kuwa na amani kabisa kudhulumu pesa ya mtu mwingine ambaye alikuwa na intention njema ya kunisaidia kwa kuniazima pesa ili niweze kutatua changamoto zangu.
Hawa watu wa mikopo ya mtandaoni washenzi mkuu.
Ikichelewa kidogo wao hawataki mazungumzo ni kukufokea na kutukana na ukizubaa washaku post we tapeli au malaya,Je hiyo ni haki!?
 
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
Hawez fahamu mamb kama hayo mtoa maada.. kichwan hamna kitu uyo yy anaona amewakomoa kumbe anajikomoa...

Lakin kwa akili za mtoa maada ataitaji mkopo wa benki ampeleke wap..hawez kuwa na mawazo ya mikopo ya benki
 
😛 😛hao branch..nilikopa 18,000 nilichukua mwaka mzima kuwalipa..looh!, meseji zao zikawa zinanijazia simu tu ...nilipoipata nikawalipa yote, ila wanasumbua haloo...usiombe ukwame uchelewe kuwalipa..utakeleka sana...hadi leo sihitaji kukopa kwa mtu😀🙁
Hapo pesa Yao ushatatulia matatizo Yako ndio wamekuwa wasumbufu..

Acha utapeli lipa pesa za watu!!
 
Kampuni imekupa mkopo kwa mfumo ambao sio physically kwa maana haukufika ofisini.

HIyo ni njia inayowapa urahisi sana matapeli kutekeleza mipango yao ya kudhulumu pesa.

Kwasababu kampuni haijui background zako kama wewe una rekodi za utapeli au ni mtu muungwana, na pia ukumbuke kampuni haijui wapi unaishi ili pengine waweze kukufuata ili hatua za huo ustaarabu zitumike.

Hivi katika mazingira hayo unadhani njia ipi ilikuwa ni sahihi kama kampuni kuifanya ili kuhakikisha watu wanarejesha pesa bila kampuni kufilisika?

Kwasababu kwenye hiyo option ya kuweka namba 3 kumbuka upo uwezekano wa tapeli kutumia namba za watu ambao hawapatikani hewani au ni namba ambazo kazisajili yeye ili tu afanikishe jambo lake naada ya hapo line zinatiwa kapuni.

Haya sasa jiweke wewe kwenye hiyo nafasi ya huyo anayekudai, umepewa namba 3 halafu zote ukipiga zimefungiwa na kuna namba nyingine unaziona utaacha kuzitumia?
Pale katika kujiunga kuna kuandika adress,na unapoipakua hiyo app ya mkopo inakutaka uweze ku allow access to contacts,files and location.
Nadhani hapo katika location unafahamu kazi yake.
Pia hao jamaa huwa hawataki kuongea wao wanaanza na fujo directly.
Yani chelewa hata masaa mawili washakufanyia unyama aisee.
 
Toka jf ianze sijawah ona mtu mpumbavu kama wewe..hvi mtu unawezaje jisifia kwa mamb ya aibu kama haya..unajisifia kudhulumu ha ha ha...sawa na mtu anajisifia kufanya zinaaa,,au kutukana ,,au ulevi..

Kiufupi hujitambui na itachukua mda sana ww kujitambua au unaweza uje kufa while mpumbavu hvo hvo..hao wameona wakae kimya labda walikosea wakamkopesha chizi ....

Ushaingizwq kwenye database ya matapeli hakuna benki ndani ya Tanzania utapewa mkopo...may be hata huo mkopo wa benk huitaji sabb upo upo TU dunian huna maono...ushakufa kifikra bado kimwili...

Wewe ni mpumbavu.
Acha ujuaji mwingi wewe.
Benki hawawezi kukosa kukopesha kisa eti kideni cha pesa X au kisa kitangazo cha pesa X kuwa wewe tapeli.
Ukienda benki watakutajia vigezo ukitimiza wataitazama dhamana basi mkopo unaingia kwako.

Pia acha mihemko kama mtoto wa kike kiasi unamuita mwenzio mpumbavu,we unaona ni sawa kumtangaza mtu tapeli na kuvunja privacy yake!?
Hivi hujui kuwa hilo ni kosa la jinai!?
Hivi hujui hao wawili wakisimama mahakamani mtoa mada anashinda kesi na atatakiwa kulipwa fidia!?

Ujuaji mwingi kumbe dunderhead!
 
Nabishana au nakujibu?
Ndiyo nadaiwa na swala la kulipa sio leo au kesho, ila uhalisia ni kwamba nimekopa nmb nikiwa nadaiwa na tigo na voda.
Na hawajawahi kuniuliza hayo madeni zaidi ya kukagua vitu vyao muhimu na mimi kupeleka nyaraka muhimu.
Basi kama ni mkopaji wa Benki kalipe huko kwenye app. Inawezekana wakati unakopa NMB basi taarifa hizo zingine hazikuwa zimefika CREDIT REFERENCE BUREAU.

Taarifa hizo zikifika Credit score zako zitashuka na utakuwa rated high risk.Benki kuu imeweka miongozo kwa mabenki nini cha kufanya kama wamepokea mteja wa mkopo ambaye ni high risk.
 
Acha uongo wewe. Unatuonaje?
Mkuu husimbishie mdau. Niongeze tu, siku hizi kampuni kubwa kidogo kabla hazijamwajiri mtu basi nao hupita huko Credit reference bureau kutazama usafi na uaminifu wa mwajiriwa tarajiwa. Wakikuta hulipi huko MPAWA basi hawakuchukui.
 
izo ni shida zake kama aliajiriwa asumbue watu mimi hayanihusu mana alitambulisha namba kama ya kampuni 😁😁
Wewe ndio una wenge hiyo namba ninayo toka 2020 na haikuwa ya kampuni.
Ninaongea ninachokijua.Labda kama yeye alikosea kutumia private number kwa kazi lakini hiyo namba ni yenyewe
 
Back
Top Bottom