Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Sahihi kabisa Off-sir
 
Sawa kama hutarajii kukopa bank za tanzania maisha Yako yote sawa ila kama utahitaji kukopa Kaa ukijua hao jamaa washapeleka record zako sababu uliweka nida watanzania wengi hawajui hii kitu na hayo madeni yanapanda Kwa riba Kila mda mliokubaliana
Hakuna benki itamnyima mkopo mteja wake kisa hawa wapuuzi. Acha uzwazwa dogo.
 
😂😂😂
 
Acha wenge. Hizo namba ni za kampuni na zinapigiaga simu kudai madeni. Hata mi zilinipigia hizo so hakuna kuingilia privacy ya mtu hapo.
 
si namba zao za ofisi ukitaka kukopa wacheki
Mi kuna siku niliona tangazo la app ya pesa X. Nikadownload ile app, then nikaingiza namba yangu ya simu alafu nika iunstall baada ya kujua kuwa ni kampuni za kukopesha.

Baada ya muda naona nimepokea 4750 toka Dex nini sijui. Ikabidi niisearch hiyo kampuni, nikawatambua so nikaamua niwatafute kwenye mitandao yao ya kijamii.

Huko nikawaambia naona mmenitumia pesa wakati sijaomba. Niwarudishie pesa yenu wakauchuna. Baada ya wiki simu zikaanza na deni juu. Sijawahi lipa ile pesa yao hadi leo.
 
Hiyo mikopo si huwa ina terms?

Na hizo namba si uliweka wewe?

Usingependa hizo disturbances usingechukua mkopo.

Pengine huo mkopo ungeweza kuupata kwa mtu wako wa karibu na ukawa umeepuka hizo kero.
namba sijawapa na sio za wadhamini niliowaweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…