Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Kampuni imekupa mkopo kwa mfumo ambao sio physically kwa maana haukufika ofisini.
Kwa taarifa yako hawa hawana ofisi kabisa.watu wametafuta ofisi wafike ili wahojiane vizuri na wanaotuma sms na kupiga imeshindikana kabisa,ni wahuni tu wenye hela.
HIyo ni njia inayowapa urahisi sana matapeli kutekeleza mipango yao ya kudhulumu pesa.
Hili sio kosa la mkopaji hata 0.1%.unampaje mtu mkopo kwa dhamana ya taarifa peke yake??πŸ™„πŸ™„πŸ™„,
Kwasababu kampuni haijui background zako kama wewe una rekodi za utapeli au ni mtu muungwana, na pia ukumbuke kampuni haijui wapi unaishi ili pengine waweze kukufuata ili hatua za huo ustaarabu zitumike.
Well,ktk makubaliano ya kabla ya kukopa,kuna sehemu tulikubaliana kwamba watajulishwa watu wote walioko ktk simu??
Unajua hilo ni kosa kubwa sana ndio maana hata wakitafutwa kwa mahojiano wanakosa nguvu ya kutoa ushirikiano hata utoe ahadi kwamba unakwenda na hela ya mdaiwa ukawape watagoma kabisa.
Hivi katika mazingira hayo unadhani njia ipi ilikuwa ni sahihi kama kampuni kuifanya ili kuhakikisha watu wanarejesha pesa bila kampuni kufilisika?
Swala la namna ya kurejesha,na namna ya kufanya ili kutofilisika halihusiani kabisa na uvunjifu wa haki za mteja,huu ni uhuni ktk kichaka cha mikopo.na ni kukosa dabu ktk fani za watu wa mikopo.
Kwasababu kwenye hiyo option ya kuweka namba 3 kumbuka upo uwezekano wa tapeli kutumia namba za watu ambao hawapatikani hewani au ni namba ambazo kazisajili yeye ili tu afanikishe jambo lake naada ya hapo line zinatiwa kapuni.
Hilo ni swala wanatakiwa wahakiki kabla hawajakupa mkopo muombaji.
Bank ukienda kuomba mkopo wa nyumba,utapewa mkopo 25% ya thamani ya nyumba,lakini kwanza sharti lazima watu wa tathmini wafike kuiona nyumba husika.
Huwezi toa hela nyumba hujaiona,itakuwa balaa.

Haya sasa jiweke wewe kwenye hiyo nafasi ya huyo anayekudai, umepewa namba 3 halafu zote ukipiga zimefungiwa na kuna namba nyingine unaziona utaacha kuzitumia?
Kwanza siwezi kifanya biashara ambayo inategemea huruma na utashi wa mteja mimi kulipwa.hii ni biashara kichaa sijwahi kuona.

Sijui ni nani alikuja na idea hii nahisi ni watu na pesa zao za kuzitakatisha.
 
Ukija me naitaka hiyo sticker πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hao hawatambuliki na bot,hata mwigulu aliwakataa,mkopo gani riba 52%
 
Hamna kitu,hao matapeli tu.ungeniambia songesha au nipige tafu sawa..ila hao wakina sijui branch au pesa x hakuna kitu na hawajasajiliwa popote hapa Tanzania
 
Wanakopaje rafiki? Nataka nichukue ya bia hapa ninywe nilale usiku huu nipate usingizi.πŸ˜…
 
Watu mnaenda nje ya mada na mnakuwa na mihemuko tu.Hivi unaelewa mleta mada anaongelea nini?? Yeye hajakataa kukopa au hajasema dhuluma ni mbaya - anawakomesha hawa wanaotumia app..wanao-access contacts zote kwenye simu ya mteja na wanawatumia sms watu wote kinyume na utaratibu.
Unafikiri hili suala ni sawa????
 
Acha uongo wako, nadaiwa mpesa 99k zaidi ya miezi sita na tigopesa 145k zaidi ya miezi miwili, mwezi uliopita nimekopa NMB na hawajaniuliza lolote kuhusu hiyo mikopo
acha uongo mkuu kila benki ikitaka kukukopesha lazima wafanye CBS check kwa kutumia NIDA yako na kama una mkopo watajua tu
 
Narudia tena dawa ya deni kulipa lipia deni la watu Hilo hamna vya bure duniani yaani unaweka namba ya nida halafu upate mkopo unachekesha wewd
Punguza ujuaji basi, hakuna benki itakataa kukupokesha kwa hicho kigezo chako. Unaelimishwa na bado umeshupaza shingo tu. Benki za biashara wana vigezo vyao, hivyo vikampuni vya mikopo kwa app ni uchwara tu.
 
Acha wenge. Hizo namba ni za kampuni na zinapigiaga simu kudai madeni. Hata mi zilinipigia hizo so hakuna kuingilia privacy ya mtu hapo.
Wewe ndio una wenge hiyo namba ninayo toka 2020 na haikuwa ya kampuni.
Ninaongea ninachokijua.Labda kama yeye alikosea kutumia private number kwa kazi lakini hiyo namba ni yenyewe.
 
Hapo unajiona mjanjaa kumbe zoba
 
Sawa kama hutarajii kukopa bank za tanzania maisha Yako yote sawa ila kama utahitaji kukopa Kaa ukijua hao jamaa washapeleka record zako sababu uliweka nida watanzania wengi hawajui hii kitu na hayo madeni yanapanda Kwa riba Kila mda mliokubaliana
Asa mtu empty kichwan kama mtoa maada atajulia wap...
 
Aliekuambia kampun Yao inategemea hyo elfu ishirini uliyozulumu kujiendesha nani..???

Umepunguza kijiko Cha chai kwenye pipa la maji afu unajisifia umemaliza maji kwenye pipa...wewe ni tapeli TU kama matapeli wengine hapa unatafuta uhalali wa ujinga wako...

Hela ndogo kama hyo huwez kuikomesha kampuni yenye mtaji wa billion na zaidi...zaid unajikomesha mwenyewe kujiingiza kwenye vifungo vya nafsi usivyovijua sabb kichwan upo empty!!!

Hao unaowajibu ni waajiriwa TU kwenye hzo kampun wanatimiza wajibu wao na mwisho wa siku wanalipwa mishahara Yao..ila kampun itabaki kustaw bila kujal loss ndogo kama hzo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…