Ndio yale yale tunayosema wajinga wa utopolo wanapinga. Jaribu kufikiria Yanga anacheza na Pamba mechi ya mwisho inayoamua Bingwa wa Ligi. Hizo hela anazojifanya kuwahaidi Pamba washinde si ndizo watakazopewa ili wafungwe! Hiyo fair game itatokea wapi hapo!? Ni mwendo wa kununua tu.
Haiingii akilini timu icheze dhidi ya Simba ihaidiwe mamilioni ili waifunge Simba, wakati ikicheza na timu nyingine haihaidiwi pesa, cha ajabu ukimfunga Simba na ukizifunga timu nyingine mfano KMC bado unapata pointi 3 zile zile, hapo hamuoni kuna shida sehemu.!? Huo ni upangaji matokeo wa wazi wazi kwani kuifunga Simba ni kumsafishia njia yule mpinzani wake akachukue ubingwa ndio maana wakicheza na timu nyingine tofauti hawahaidiwi fedha.