Pamoja na Dodoma kuwa Katikati ya nchi lakini bado haikupaswa kuwa Makao Makuu

Watu wenyewe hawapandi miti,watu wananunua viwanja vya square meter 200-400 atapanda mti gani hapo
 
Ungeliongelea hisia za namna unavyotaka kuendesha maisha yako binafsi, lakini si kwa kukosoa maamuzi sahihi ya Serikali kuhamishia makao makuu pale.

Dodoma imo katika jiografia ya nchi, hauwezi kuitweza ama kuitenga na Tanzania kwa sababu yoyote ile.

Mengi ya sababu ulizoongelea zaweza kurekebishwa kwa kuboreshwa kwa miundo mbinu ya msingi tu na pakawa safi kabisa pa mfano.

Angalia maeneo mengine Duniani yenye jiografia yenye dhiki kuliko jiografia ya Dodoma, kwa mfano Dubai ya leo ama miji mingine iliyomo katika nchi za majangwani namna walivyoboresha miundo mbinu yao na jinsi wanavyo yafurahia maisha!

Ninadhani ungekuja na hoja namna ya kuligeuza Jiji la Dodoma liwe la kijani ili liweze kufaa zaidi kwa maisha ya binadamu.

Uwezekano wa kuvutwa maji baridi toka vyanzo vya kueleweka upo na ulikuwepo.

Maji kutoka Viktoria kuyafikisha pale Igunga, ajenda kuu ilikuwa ni kuyafikisha hadi makao makuu Dodoma ili kulifanya jiji lisitimke vumbi na liwe la kijani.

Uwezekano huo upo, sema labda mipango ndiyo inachelewa tu.

Mkuu, mawazo yako siku zote jaribu kuyaweka kutatua tatizo na si kusifia sehemu iliyokwisha boreshwa.

Dar es salaam unapopasifia, bila kuwekwa miundombinu ya maana, pangelifaa nini hapo, kwanza joto lililopo la kushinda na taulo mtu ukijifuta jasho, watu wengine hawawezi kupapenda.

Kwa hiyo jiografia ya kila sehemu yoyote hapakosi changamoto zake na uzuri wake pia.
 
mwamba anaongea kutoka moyoni duh , yaani balaa tupu eti kazeeka kisa maji ya munyu, sasa kama hupapendi siubakie unakopenda mzee baba ili uwe soft kama KE
 
Kwan mipango hio si ipo. Jiji hawakup kibal cha ujenz had upande mti.na mabati yasiwe tofaut.au ilikufa hio mipango na kunambi alivoondoka? Dom napenda sana ule mtaa wa vitumbua na mabajia. Kwa stend ya daladala ni vurugu tupu haijulikan yan hapaelewek. Ukiwa mjin pale mazingira saf tu.vumbi lipo tu kila eneo.ila nadhan singida ingekua ndio mji mkuu.singida haina ukame kama wa dodoma.unaweza ukaona utan ila ukabu wa singapoo sio sawa na dom
 
kalinganisha na dar hali ya hewe ya dar masikini na tajiri wote wote wanang,aa lakini domu hata utupwe kwenye tengi la siagi ukitolewe umepauka tiiiiii
Paka mafuta
 
Daaah!!! Nikiri tu kuwa JF kuna watu wachache sana waungwana na intelligent mmoja wapo ukiwa ni wewe. Umejibu kiungwana bila maneno ya maudhi, umeandika Kisomi na hoja zenye mashiko. Sikusifii bure lakini ndivyo unavyosomeka hivi.
Unajuwa humu tumezoea majibu ya hasira, povu, kejeli na matusi.
 
Dom kwenda magharibi huko Pana Hali ya hewa nzuri sana,hakuna joto la kiwaki,nimeishi Dom miaka miwili,kuhusu kunawiri mtoa mada muongo
Mpakani mwa Babati na kondoa ni pazuri sana
 
Mkuu nilipita na kutembea sana Dodoma kusema kweli lilikuwa wazo baya kabisa kuweka makao makuu kwa sababu uliyotaja na nyingine lukuki

Mji mkuu ungejengwa Tabora kama walivyofanya Wajerumani kipindi fulani
 
Sku ya kwanza kufika dodoma nilipaka lotion,,, nkavaa nguo,,, ile namaliza kuvaa tu najiangalia kwny kioo, ngozi kama ya kenge,,, khaaaaaa
 
Sasa kama hari ya hewa ya Dodoma inaumiza,vipi hari ya hewa ya Qatar,Dubai,kwenye jangwa?kwahiyo kwa mtazamo wako,eneo lisipo kuwa na hari ya hewa nzuri kama ulaya,halitakiwi kuendelezwa auxkupandishwa hadhi?!basi waarabu wasingejenga kwao kwa vile Kuna hari mbaya!!!
Bro usione vinaelea,vimeundwa,miji inajengwa,
Uarbuni Kuna joto na jua Kali,lakini michezo ya barafu huwa inafanyika,barafu snow,inatengenezwa!!
Umeishawahi kusikia man made lake?maziwa ya kutengeneza?
Binadamu wa Karne hii hatakiwi kuishi kwa kudra za Mungu,badilisha mazingira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…