Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Siku ya leo Jumapili Januari 19 vita vya Gaza vinaingia hatua muhimu ambapo kutakuwa na usitishwaji wa vita kwa muda na ambao unaelekea kuwa wa kudumu baada vita vya zaidi ya mwaka mmoja.
Vita hivyo ni kati ya taifa kubwa kijeshi la Israel na washirika wake ambao ni mataifa makubwa dunia dhidi ya vikundi vya wanamgambo ndani ya Gaza vinavyoongozwa na Hamas.
Katika vita hivyo ambavyo huenda ndio vita vibaya zaidi kwa teknolojia za kisasa watu karibu nusu laki wameuliwa sambamba na majengo karibu yote ya ghorofa kuporomoshwa.
Hata hivyo Israel imeshindwa kuupata ushindi iliotangaza kuutafuta.
Vita vilipoanza Israel ilitangaza kutaka kuimaliza Hamas na kuwarudisha nyumbani mateka wote waliokuwa wakishikiliwa ndani ya Gaza.
Siku ya leo ni muhimu sana kwa pande zote zilizokuwa zikipigana. Israel kwa upande wake baada ya kushindwa kuwaokoa mateka wake itakabidhiwa baadhi yao kutoka kwa Hamas ambao watarudishwa nyumbani.
Kwa upande mwengine watu wa Gaza watapata nafuuu ya kuuliwa kwa kasi ya watu wasiopungua 100 kwa siku.
Kilichowazi kwa kila mfuatiliaji wa vita hivi ni kuwa Israel imefanya makubaliano na wale wale ilioazimia kuwamaliza na wasiwepo kabisa Gaza na kwamba mateka imebidi wawapate kwa njia za makubaliano na haikuwa wa kubebwa kibabe kama ilivyowahi kufanyika kuleta Entebe ambalo ndili lililokuwa lengo la awali.