Pamoja na hasara kubwa waliyoipata Hamas lakini Israel imeukosa ushindi

Pamoja na hasara kubwa waliyoipata Hamas lakini Israel imeukosa ushindi

Waisilamu na wakiristu bana utadhani wamebet kwenye hii vita ujinga mtupu
 
Hilo ndio tangazo la kushindwa vita kwa Israel.
Tujaalie hakuna mateka wa kubadilishwa kosa itakuwa ni la nani na Israel nayo itafanya nini baada ya kuporomosha majengo ya Gaza.Jee wataendelea kuuwa wapalestina waliobaki kwenye makambi au itachukua uamuzi gani mwengine?
Sasa kama hakuna mateka wa kubadilishana nao unategemea nini ? Ni hasira juu ya hasira ni mwendo na kichapo tu.
 
Jiulize na Israel imepata nini katika kuuwa watu zaidi ya 45000 na kuvunja majumba.
Mbona hawajaweza kuwamaliza Hamas.Zaidi imedhihirika kuwa Israel haina uwezo wa kupigana bila msaada wa mataifa makubwa na kwamba wapalestina wakiendelea kukomaa watarudisha heshima zao.
Acha kujipa moyo wewe hata miundo mbinu inapoharibiwa nayo ni hasara kubwa.

Mbona wewe unakaa kwenye nyumba ya kupanga, haukai kwenye magofu. Wenzake Gaza huko ndani hakukaliki wengine wanalala kwenye magofu.
 
Shida kubwa ni uelewa.

Kwa kiasi kikubwa kwenye vita hii walioathirika na kupoteza sana ni Hamas. Malengo ya Hamas, katika kufanya tukio la kigaidi dhidi ya Israel yalikuwa:
1) Kuamsha agenda yao ya kutaka kupatikana Taifa la Palestina

2) Kwa kushikilia mateka, walitaka Israel iogope kuwashambulia kwa hofu ya wao Hamas wangewaua mateka au mateka wangeuawa wakati wa mashambulio

3) Kutumia shambulio la ugaidi kuonesha wana uwezo wa kuwaua wayahudi kama endapo Israel haitaafiki matakwa yao.

Kikichotokea:
Hamas haikukipata hata kitu kimoja katika ilivyovitaka, ikaishia kusababisha vifo maelfu ya wapalestina; viongozi wake wote wakuu kuuawa, serikali yao kupotea, mfadhili wao mkuu Iran kupoteza nguvu za ulinzi wa anga na vifo vya askari wake, wasaidizi wake, yaani Hezbolla, serikali ya Assad, wote kupigwa vibaya na kupotezewa uwezo wa kiuchumi, na kuifanya Gaza nzima kuwa hoi kabisa kiuchumi na kihuduma.

Kwa upande wa Israel:

1. Wameweza kuisambaratisha serikali ya Hamas na kuwaua maelfu ya wapiganaji wa Hamas na viongozi wao

2) Wamepata mwanya wa kuwaadhibu na kuwatekeza mahasimu wao wakuu. Makamanda na viongozi wa Hezbollah wameuawa, makamanda wa Iran wameuawa, Hezbollah imeteketezwa ndani ya Lebanon na sasa wamepoteza udhibiti wa Serikali ya Lebanon.

3) Wamepata mwanya wa kuuondoa utawala wa Assad nchini Syria.

4) Wameweza kuteketeza kiwanda cha nuklia cha Iran na mifumo yake ya ulinzi wa anga.

5) Wameweza kutengeneza mazingira ya kuwalazimisha Hamas kuwaachilia mateka bila ya malengo yao ya kutaka Taifa la Palestina, kufanikiwa.

6) Israel imeweza kuzima sauti zozote zile za vita hii kuamsha mjadala wa kuundwa kwa Taifa la Palestina. Hata Hamas wenyewe wamebakia kuongelea tu kusimamishwa kwa vita, na siyo kuundwa kwa Taifa la Palestina

Kwa ujumla, Israel imefanikiwa zaidi hata ya ilivyokuwa imetamka, maana hayo ya kuuondoa utawala adui wa Syria, kuunyong'onyesha utawala wa Iran, kuwamaliza viongozi na nguvu za kijeshi za Hezbollah, havikuwepo kwenye malengo makuu, lakini wamefanya.

Hata hivyo, hakuna vita isiyo na hasara, Israel imepoteza mamia ya askari, na rasilimali mbalimbali kwenye vita hii, japo hiyo hasara ni justifiable.

Kwa njia za kigaidi, hakuna namna Hamas itaweza kuwaletea wapalestina Taifa huru. Kila mara wataishia kupoteza zaidi kuliko kupata.
 
Shida kubwa ni uelewa.

Kwa kiasi kikubwa kwenye vita hii walioathirika na kupotrza sana ni Hamas. Malengo ya Hamas, katika kufanya tukio la kigaidi dhidi ya Israel yalikuwa:
1) Kuamsha agenda yao ya kutaka kupatikana Taifa la Palestina

2) Kwa kushikilia mateka, walitaka Israel iogope kuwashambulia Hamas kwa hofu yawao Hamas wangewaua mateka au mateka wangeuawa wakati wa mashambulio

3) Kuwatumia shambulio la ugaidi kuwawana uwezo wa kuwaua wayahudi kama endapo Israel haitaafiki matakwa yao.

Kikichotokea:
Hamas haikukipata hata kitu kimoja katika ilivyovitaka, ikaishia kusababisha vifo maelfu ya wapalestina; viongozi wake wote wakuu kuuawa, serikali yao kupotea, mfadhili wao mkuu Iran kupoteza nguvu za ulinzi wa anga na vifo vya askari wake, wasaidizi wake, yaani Hezbolla, serikali ya Assad, wote kupigwa vibaya na kupotezwa uwezo wa kiuchumi, na Gaza nzima hoi kabisa kiuchumi.

Kwa upande wa Israel:

1. Waneweza kuisambaratisha serikali ya Hamas na kuwaua maekfu ya wapiganaji wa Hamas na viongozi wao

2) Wamepata mwanya wakuwaadhibu na kuwatekeza mahasimu wake wakuu. Makamanda na viongozi wa Hezbollah waneuawa, makamanda wa Iran wameuawa, Hezbollah imeteketezwa ndani ya Lebanon mpaka kupoteza udhibiti wa Serikali ya Lebanon.

3) Wamepata mwanya wa kuuondoa utawala wa Assad nchini Syria.

4) Wameweza kuteketeza kiwanda cha nuklia cha Iran na mifumo yake ya ulinzi wa anga.

5) Wameweza kutengeneza mazingira ya kuwalazimisha Hamas kuwaachilia mateka bila ya malengo yao ya kutaka Taifa la Pakestina kufanikiwa.

6) Israel imeweza kuzima sauti zozote zile za vita hii kuamsha mjadala wa kuundwa kwa Taifa la Palestina. Hata Hamas wenyewe wamebakia kuongelea tu kusimamishwa kwa vita, na siyo kuundwa kwa Taifa la Israel.

Kwa ujumla, Israel imefanikiwa zaidi hata ya ilivyokuwa imetamka, maana hayo ya kuuondoa utawala adui wa Syria, kuunyong'onyesha utawala wa Iran, kuwamaliza viongozi na nguvu za kijeshi za Hezbollah, havikuwepo kwenye malengo makuu, lakini wamefanya.

Hata hivyo, hakuna vita isiyo na hasara, Israel imepoteza mamia ya askari, na rasilimali mbalimbali kwenye vita hii, japo hiyo hasara ni justifiable.

Kwa njia za kigaidi, hakuna namna Hamas itaweza kuwaletea wapalestina Taifa huru. Kila mara wataishia kupoteza zaidi kuliko kupata.
Huijui Iran hata kidogo kaa kimya tuu nenda kachambue kanisani hizo hoja zako.
 
Kwa taarifa yako hamas hard kwenye utawala Gaza ndio makubaliano na Israel anatoa jesh maeneo maalum ya watu sio Gaza. Huu ujinga ni kama ule mnaolishana kwamba hezbollah ameshinda wakati alipigwa mande kila mahali mpaka akakubali kunyoosha.mikono
upofu sio kutokuwa na macho tu
 
Siku ya leo Jumapili Januari 19 vita vya Gaza vinaingia hatua muhimu ambapo kutakuwa na usitishwaji wa vita kwa muda na ambao unaelekea kuwa wa kudumu baada vita vya zaidi ya mwaka mmoja.

Vita hivyo ni kati ya taifa kubwa kijeshi la Israel na washirika wake ambao ni mataifa makubwa dunia dhidi ya vikundi vya wanamgambo ndani ya Gaza vinavyoongozwa na Hamas.

Katika vita hivyo ambavyo huenda ndio vita vibaya zaidi kwa teknolojia za kisasa watu karibu nusu laki wameuliwa sambamba na majengo karibu yote ya ghorofa kuporomoshwa.

Hata hivyo Israel imeshindwa kuupata ushindi iliotangaza kuutafuta.

Vita vilipoanza Israel ilitangaza kutaka kuimaliza Hamas na kuwarudisha nyumbani mateka wote waliokuwa wakishikiliwa ndani ya Gaza.

Siku ya leo ni muhimu sana kwa pande zote zilizokuwa zikipigana. Israel kwa upande wake baada ya kushindwa kuwaokoa mateka wake itakabidhiwa baadhi yao kutoka kwa Hamas ambao watarudishwa nyumbani.

Kwa upande mwengine watu wa Gaza watapata nafuuu ya kuuliwa kwa kasi ya watu wasiopungua 100 kwa siku.

Kilichowazi kwa kila mfuatiliaji wa vita hivi ni kuwa Israel imefanya makubaliano na wale wale ilioazimia kuwamaliza na wasiwepo kabisa Gaza na kwamba mateka imebidi wawapate kwa njia za makubaliano na haikuwa wa kubebwa kibabe kama ilivyowahi kufanyika kuleta Entebe ambalo ndili lililokuwa lengo la awali.
Huu ni ujinga mnaoendelea kulishana misikitini na madrasa,Hamasi October 7,2023 walianzisha vita lengo kuiangamiza Israel,Israeli ikaingia mzigoni ikawapiga Kona zote mpaka wamesalia kwenye mashimo utawala wa Hamas Gaza umeangushwa hakuna wanapotawala zaidi ya mashimo waliomo ambamo namo Kila saa wanawindwa kukubali kurudisha mateka ni kusalimu amri kwa Hamas maana Trump Alisha waambia ikifika 20 Januari hawajaachia mateka atawafanya kitu mbaya ndo unaona wanasalim amri,uwe unatumia akili kobasi
 
Wao wakishangilia Israel wanaumia nini? Kwann wanawapiga mabomu? Ama kweli nani mshindi sasa kama wameshinda kwanini wanaua Watu wanaoshangilia kushindwa?
 
Kwanini nyie watu mnapenda sana kuona wenzenu wakiuwawa

Yaan wewe badala ushukuru kwa mola kwamba vita imeisha wewe unaanza kutafuta mshindi tena

Ivi unajua mateso wanayopitia watu wa Palestine kweli wewe
 
Dah Waduwanzi wameua watu kibao,lakini wameshindwa kushinda vita..Wameshwindwa kuwarudisha mateka,na wameshindwa kuwamaliza Hamas.
 
Jiulize na Israel imepata nini katika kuuwa watu zaidi ya 45000 na kuvunja majumba.
Mbona hawajaweza kuwamaliza Hamas.Zaidi imedhihirika kuwa Israel haina uwezo wa kupigana bila msaada wa mataifa makubwa na kwamba wapalestina wakiendelea kukomaa watarudisha heshima zao.
Hiv hujui Israel mpaka muda huu imepatana nini mkuu au umekuwa kipofu ni sawa. Golan height imeondoka yote. Pale west bank wale masetler wameondoka na vijiji kibao. Na kwasasa hamas harud kutawala gaza cjui kama unaelewa au umelewa
 
Hamas wasiwepo kiasi kwamba angeingia mitaani tu kuunda serikali isiyo na Hamas na ingekuwa ni tusi kuwaomba Hamas msaada wa kuwapata mateka
Hamas ni watu
Wasiwepo maana yake wote wafe?
 
Jiulize na Israel imepata nini katika kuuwa watu zaidi ya 45000 na kuvunja majumba.
Mbona hawajaweza kuwamaliza Hamas.Zaidi imedhihirika kuwa Israel haina uwezo wa kupigana bila msaada wa mataifa makubwa na kwamba wapalestina wakiendelea kukomaa watarudisha heshima zao.
Huwezi jua labda lengo lao ilikuwa kuua watu zaidi ya elfu 45 na kubomoa majumba
 
Nyinyo
Thamani ya waisraeli 33 ni sawa na wapalestina 1890??!!!.Hii nimeona kwenye deal la kubadilishana wafungwa!!!
Nyinyi mazwazwa kazi kupotosha watu lkn mtawapotosha mazwazwa wenzenu tu waislamu vichwani wako oky wanaelewa ukweli huu muisrael m 1 anasamani yoyote mbele ya .waislamu 1 ata ktk mapigigano waisrael wawe 10 kwa muislam 1 tu na anawakalisha!! Ona kwann nawaita mazwazwa ona akili zenu za kitoto na propaganda zenu za kitoto nije kwenye mada yako kwanini muisrael 1 kwa wapalestina 50 jibu lake ni ili tu bisha zwazwa ww waisrael ndio Magaid OG wao wameteka wapalestina wengi sana wamewafungia uko Israel ata kabla ya 7octb waliwateka wapalestina zaid ya 10000 wakiwemo watoto ivo uvamizi wa Hamas iyo 7octb ilikuwa na lengo moja tu kuwachukua waisrael kama mia300 ili wawatumie kuwakomboa wapalestina wenzao waliojaa ktk jela za Israel ndio maana baada ya 7octb Hamas wakaitangazia dunia kuwa wao awataki vita ila wanataka tu Israel iwaachilie wapalestina wanaowashikilia uko kwao Israel lengo la HAMAS awakuona Sababu ya kuwachukua waisrael 10000 lkn awa awa mia300 watawalazimisha waisrael iwe kama ivo unaona sasa 1 kwa 50 manake waisrael 20 wapalestina 1000 waisrael 100 wapalestina 5000 lengo tu kuwatoa wapalestina kwenye mikono ya magaid ya Israel hii misheni waisrael waliikataa mwanzo wakaona waingie vitani baada kuona vita avikuweza kufanikisha kupata waisrael nawao kupoteza wanajeshi wengi kupata ulemavu wakudumu na asala zengine chungunzima Netanyahu na waisrael kwa ujumla wameona watiii amri ya Hamas ndio mana duniani nzima wanajua waisrael wameshindwa vita ndio mana sasa wanakula matapishi yao waliokataa mwanzo kwann ili lasasa wasikubali tangia mwanzio lingeepusha vifo vya wapalestina wasionatia lkn pia lingeokoa wanajesh wa IDF elf kadhaa waliokufa na kuifanya Israel kiuchumi iyumbe sana kwasasa kwaiyo hii kusema eti muisrael 1 samani yake sawa na wapalestina 50 kichekesho cha mazwazwa wengi wamechafukwa na ushindi huu wa wapalestina niwatakie asubui njema jumatatu njema watetezi wa haki wote pamoja n mazwazwa wetu.
 
Huu ni ujinga mnaoendelea kulishana misikitini na madrasa,Hamasi October 7,2023 walianzisha vita lengo kuiangamiza Israel,Israeli ikaingia mzigoni ikawapiga Kona zote mpaka wamesalia kwenye mashimo utawala wa Hamas Gaza umeangushwa hakuna wanapotawala zaidi ya mashimo waliomo ambamo namo Kila saa wanawindwa kukubali kurudisha mateka ni kusalimu amri kwa Hamas maana Trump Alisha waambia ikifika 20 Januari hawajaachia mateka atawafanya kitu mbaya ndo unaona wanasalim amri,uwe unatumia akili kobasi
Tumia akili vyema kuona kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom