Pamoja na kulamba Asali, Mbowe alaani utitiri wa magari, msafara wa Rais hauendani na kubana matumizi

Pamoja na kulamba Asali, Mbowe alaani utitiri wa magari, msafara wa Rais hauendani na kubana matumizi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Adai ni matumizi mabaya ya pesa za umma.

Mwigulu Nchemba auchuna.

Mbowe ahoji utitiri wa magari msafara wa Rais

=======
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema utitiri wa magari katika msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan hauendani na dhana ya serikali ya kubana matumizi.

Amesema, gharama za maisha zinatesa wananchi huku serikali ikionekana kutodhihirisha kwa vitendo mkakati wake wa kubana matumizi

Mbowe aliyasema hayo juzi mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia wanachama wa chama hicho katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA).

Alisema hivi karibuni alimwandikia ujumbe Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kumweleza kodi na tozo wanazotoza kwa wananchi haziakisi uhalisia na kuchochea umaskini miongoni mwao.

“Kodi hutozwa matajiri ili kuwasaidia maskini, unategemea nini kwa wananchi hawa unapowatoza kipato chao kidogo? Sasa wenzetu hawa hawaelewi, nilimuandikia barua Dk Mwigulu kuhusu hili mpaka sasa sijapata majibu” alisema

Alisema: “Gharama za kuendesha serikali kila siku zinapanda, Rais anatembea na msafara wa magari karibu 70 hadi 80 Land Cruiser za kazi gani? Hivi kweli nchi hii na umaskini wake unatumia magari yote haya, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais.”

Mbowe alitolea mfano Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Naibu wake wawili, Salum Mwalimu (Z’bar) na Benson Kigaila (Bara) wote watatu wametumia gari moja kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga ili kubana matumizi.

Kiongozi huyo wa upinzani ametoa kauli hiyo wakati Rais Samia akiendelea na ziara za kikazi mkoani Iringa akitokea Mkoa wa Njombe na Mbeya alikoanzia.

Lengo la ziara hiyo iliyoanza Agosti 5 mwaka huu ni kukagua, kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Chanzo: Mwananchi
 
Adai ni matumizi mabaya ya pesa za umma.

Mwigulu Nchemba auchuna.
Mbowe ahoji utitiri wa magari msafara wa Rais

=======
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema utitiri wa magari katika msafara wa Rais Samia Suluhu Hassan hauendani na dhana ya Serikali ya kubana matumizi.

Amesema, gharama za maisha zinatesa wananchi huku Serikali ikionekana kutodhihirisha kwa vitendo mkakati wake wa kubana matumizi

Mbowe aliyasema hayo juzi mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia wanachama wa chama hicho katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Alisema hivi karibuni alimwandikia ujumbe Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Chemba kumweleza kodi na tozo wanazotoza kwa wananchi haziakisi uhalisia na kuchochea umaskini miongoni mwao.

“Kodi hutozwa matajiri ili kuwasaidia maskini, unategemea nini kwa wananchi hawa unapowatoza kipato chao kidogo? Sasa wenzetu hawa hawaelewi, nilimuandikia barua Dk Mwigulu kuhusu hili mpaka sasa sijapata majibu” alisema

Alisema: “Gharama za kuendesha Serikali kila siku zinapanda, Rais anatembea na msafara wa magari karibu 70 hadi 80 Land Cruiser za kazi gani? Hivi kweli nchi hii na umaskini wake unatumia magari yote haya, waziri mkuu, makamu wa Rais.”

Mbowe alitolea mfano Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Naibu wake wawili, Salum Mwalimu (Z’bar) na Benson Kigaila (Bara) wote watatu wametumia gari moja kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga ili kubana matumizi.

Kiongozi huyo wa upinzani ametoa kauli hiyo wakati Rais Samia akiendelea na ziara za kikazi mkoani Iringa akitokea Mkoa wa Njombe na Mbeya alikoanzia.

Lengo la ziara hiyo iliyoanza Agosti 5 mwaka huu ni kukagua, kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Chanzo: MWANANCHI
Mbowe akicheleweshewa mgao wake kutoka Juu anakua mkali sana!!
 
Hizo V8 zina sound proof ya malalamiko ya matatizo yanayowakabili wananchi.

Wakishastaafu ndio wanakumbuka walichokifanya na kuandika vitabu..

Ila wakiwa madarakani hawawezi tuelewa tunaposema maisha magumu.
 
Lile faili lipo, ni kuonesha tu nia ya kuendelea na case, sijui DPP anasubiri nini??? Ningekuwa mi ndiye DPP huyu Mbowr ningehakikisha namfunga maisha au hukumu ya kifo, hafai kabisa kwa demokrasia ni dikiteta na muuaji
 
Back
Top Bottom