Pamoja na kulamba Asali, Mbowe alaani utitiri wa magari, msafara wa Rais hauendani na kubana matumizi

Alianza mwenda zake naona naye kaiga, msafara, mapadiri, mashekhe vyombo vyote vya ulinzi ,mpaka waimba mapambio Kila mtu na gari lake hapo lazima idadi ifikie 90 (V8)
Wanashida gani wakati awatoi mifukoni mwao
 
Mwigulu kukaa kimya bila kujibu hiyo meseji ya Mbowe hata sishangai, ina maana Mbowe hajui kama mwenzie anapenda kukusanya pesa ambazo mwisho wa siku haulizwi mapato ni kiasi gani, na matumizi yake ni yapi?

Mwigulu ana enjoy sana kuwa waziri wa fedha, naamini hata mifuko yake kwasasa inaendana na maana halisi ya yeye kuwa waziri wa fedha, kwa hii nchi yetu masikini mpaka wa fikra, kuwa waziri wa fedha halafu ufe kwa njaa ni ujinga wako mwenyewe.

Ila kuhusu hao makatibu wa Chadema bara na visiwani kutumia hilo gari moja kwa safari, nahisi sababu ni hali ngumu tu, siku Chadema wakibahatika kwenda ikulu nao ndio tutajua tabia yao halisi, now ni benefit of doubt.
 
Lile faili lipo, ni kuonesha tu nia ya kuendelea na case, sijui DPP anasubiri nini??? Ningekuwa mi ndiye DPP huyu Mbowr ningehakikisha namfunga maisha au hukumu ya kifo, hafai kabisa kwa demokrasia ni dikiteta na muuaji
Bahati nzuri hujapata hayo madaraka, Unafikiri mambo yako kirahisi rahisi hivyo? Fikiri kabla ya kudhihirisha jinsi ulivyo mweupe kuchwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi za nchi hii haziendi kuwasaidia wananchi..badi zinaenda kuliwa na wahuni wa lioko serikalini na kwenye chama..ndio mana wananchi hawana mwamko wa kulipa kodi.

#MaendeleoHayanaChama
Alafu Mtumishi wa Umma,anakuja kutukoga na kagari kapya kuliotokana na Kodi zetu!!!
 
Alianza mwenda zake naona naye kaiga, msafara, mapadiri, mashekhe vyombo vyote vya ulinzi ,mpaka waimba mapambio Kila mtu na gari lake hapo lazima idadi ifikie 90 (V8)
Na hii ndiyo maana ya kua Urais ni taasisi, team nzima lazima itimie, anae lipya na asiyelipwa wote ni muhimu sana kwa msafara wa Rais!!
 

..Mwigulu Nchemba alikuwa na msafara wa ma-V8 na mapikipiki siku aliyokwenda kusoma bajeti ya serikali.

..kwa sisi tuliokula chumvi nyingi tunakumbuka miaka ambayo mawaziri hawakuwa na misafara, na walitumia magari madogo kama peugeot 404, na 504.

..hapo utamuona Amir Habib Jamal waziri wa fedha ameshuka toka kwenye peugeot 404 anaingia bungeni kusoma bajeti.

 
Ni wapi alikolambia hiyo asali , weka ushahidi kabla hatujakufungukia zaidi .
 
Kuna wakati naona mindset ya viongozi wetu wa sasa ni ya kimasikini inayowaelekeza kwenye anasa [matumizi makubwa kupitiliza] huku wamezungukwa na raia wa kawaida wasio na kitu.

Wanajiona ili wao watofautishwe na member wengine wa hii society yetu, na viongozi waliopita, basi lazima wawe na magari ya bei mbaya kwenye misafara yao, na yawe mengi hasa, msafara ukiwa mdogo hauwasuuzi mioyo.

Huo ndio ukweli halisi ndio maana licha ya wao kila siku kusema wanabana matumizi, lakini bado yapo matumizi makubwa yaliyowazunguka kila siku kwenye utendaji wao ambayo hawataki kuyaacha.

Hawa ni walevi wa madaraka wanaotudanganya kwa uzalendo feki wa kuvaa tai yenye rangi za bendera ya taifa ili tuwaamini.
 
Asali imechanganywa na faru John tabu tupu. Haya magaidi sio ya kuyaamini kabisa.
 
Chenga tu hakuna lolote hapo anaacha kuongelea katiba anazungimzia utitiri wa magari kwenye msafara wa Raisi,Mbowe anajizima akili makusudi anajifanya hajui kuwa ujinga wote huo ni sababu ya katiba Mbovu tuliyonayo.Ili wenye AKILI tumuelewe arudi kwenye ajenda ya KATIBA MPYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…