🇰🇪 1. Vijana wameingia barabarani kupinga muswada wa sheria ya fedha (finance bill 2024) ambayo ilikiwa inakwenda kuongeza tozo na ushuru katika bidhaa mbalimbali.
🇹🇿 1. Tanzania, mawaziri wanalipa mazombi posho kusukuma hashtag na bungeni waziri anataja jina la Rais mara 40, bajeti inapita. Wabunge wanaruka sarakasi na miluzi.
🇰🇪 2. Maandamano ya kupinga muswada wa sheria yameratibiwa na wananchi wenyewe, hakuna chama cha siasa kilichoshiriki kuandaa. Hiyo inaitwa nguvu ya umma.
🇹🇿 2. Serikali ya Tanzania inapitisha tozo na kodi nyingi kwa watanzania, Waziri wa fedha anatoka hadharani anasema asiyekubaliana na kulipa tozo hizo ahamie Burundi.
🇰🇪 3. Baada ya kuingia barabarani, Rais William Ruto imebidi awaite wabunge wa upande wa Serikali (Kenya Kwanza) wajadili na kukubaliana kuondoa jumla ya tozo 14.
🇹🇿 3. Wananchi wanalalamika lakini wanaendelea kulipa. Baadae Rais anasema hajawahi kuona Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba anasifiwa. Ni kulaaniwa, apige kazi tu.
🇰🇪 4. Ruto amesema mapendekezo yameondolewa kufuatia zoezi la ushirikishwaji wa umma ambalo lilishuhudia Wakenya wakiibua upinzani dhidi ya mapendekezo hayo.
🇹🇿 4. Wananchi hata wakishirikishwa, hawaelewi nguvu zao, bado kuna wengine wanasema siasa haiwahusu, hawajui kuacha kushiriki ndiyo ahueni kwa serikali ya CCM.
🇰🇪 5. Awali Ruto aliwaita wabunge wa Kenya Kwanza, Ikulu ili kuwashinikiza kupitisha muswada huo wa sheria ya fedha, wabunge hao wamemkatalia baadhi ya tozo.
🇹🇿 5. Watanzania wao wanaamini ni wajibu na jukumu la CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe na Tundu Lissu kuwapambania kuhusu ugumu wa maisha yao.
🇰🇪 6. Wabunge hao wamemueleza Rais Ruto kwamba, watapitisha muswada wa sheria ya fedha ikiwa kelele za wakenya zitazingatiwa. Serikali imeondoa tozo 14 tata.
🇹🇿 6. Wabunge wa Tanzania wao kila linapotajwa jina la Rais wanapiga makofi, hawasomi vifungu vya bajeti, wanaunga kila hoja mkono na wanapitisha. Hawakuchaguliwa.
🇰🇪 7. Tozo zilizoondolewa; 16% ya VAT kwenye mkate na usafirishaji sukari, huduma za fedha na miamala ya kigeni, mafuta ya kula, bidhaa za ndani, kusajili biashara. Etc.
🇹🇿 7. Tanzania bado tozo zipo nyingi na katika bajeti ya 2024/25 zimeongezwa tozo nyingine na waliongezewa tozo na kodi hawana habari wao ili mradi wanapumua tu.
🇰🇪 8. Wananchi wa Kenya hawaogopi polisi, maandamano wameitisha wenyewe na wameingia barabarani hadi Rais na wabunge wake wamewasikiliza hoja zao.
🇹🇿 8. Pamoja na kwamba polisi wa Tanzania ni katili lakini hata katika maandamano ya ambayo yanalindwa na polisi vizuri watanzania wanapunga mkono kwa mbali.
🇰🇪 9. Kenya, unawaona vijana wadogo wa kike na wa kiume barabarani, wamebeba mabango yenye maandishi yanayotaka serikali iondoe muswada huo wa sheria ya fedha.
🇹🇿 9. Tanzania, wasichana na vijana wamejazana katika kumbi za starehe wanashindana kuvuta shisha hawajui kama bajeti ya nchi yao imepitishwa na tozo na kodi kibao.
🇰🇪 10. (GDP) ya Kenya ni $113.4 billion (2022). GDP per capita ni $2,099.30 (2022). Wananchi wa Kenya wameingia barabarani, uchumi mkubwa wa nchi, hauwagusi wananchi.
🇹🇿 10. GDP ya Tanzania ni $75.7 bilioni (2022). GDP per capita ni $1,192.77 (2022). Kenya wapo juu kiuchumi na wameingia barabarani, watanzania wanamwaga pongezi kwa Rais.
Martin Maranja Masese, MMM.