KERO Panel za usahihishaji mitihani ya kitaifa form two na form 4 - Waziri wa Elimu ziangaliwe upya, kuna ukabila uliokithiri

KERO Panel za usahihishaji mitihani ya kitaifa form two na form 4 - Waziri wa Elimu ziangaliwe upya, kuna ukabila uliokithiri

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Masuala ya mitihani na usahihishaji ni siri kichogo wewe. Kama unahisi hakuna usawa ungelipeleka malalamiko sehemu husika na sio mtandaoni. Kumbuka kiapo ulichokula. Mwakani nyote mlioteuliwa mwaka huu hamtaingia tena.
 
Ukweli tuliouanzisha tokea miaka ya 90 sasa unazaa matunda, sasa watu wanaanza kujua sio tu kulikua na upendeleo wa kidini, kumbe huu ushenzi umejikita mizizi mpaka kwenye ukabila....

Kwamba NECTA wanapendelea badhi ya Wanafunzi kwa kigezo cha UDINI na UKABILA?

Nitakuwa wa Mwisho kuamini hichi kitu.
 
Masuala ya mitihani na usahihishaji ni siri kichogo wewe. Kama unahisi hakuna usawa ungelipeleka malalamiko sehemu husika na sio mtandaoni. Kumbuka kiapo ulichokula. Mwakani nyote mlioteuliwa mwaka huu hamtaingia tena.

Uzuri pass record za Wanafunzi hua Zinaonekanaga Kuanzia first year mpaka mtihani wa mwisho wa NECTA.

Walio kua na Zero mitihani ya Ndani ndo hao hao, wanapata ZERO NECTA, sasa sijui anasema upendeleo gani.

Hata hivo, Muamko wa Elimu/Shule Kaskazini ni mkubwa kuliko sehemu nyingi
 
NECTA wao kama wao wapo vizuri sana na wako very fair tatizo ni hao wenyeviti wa panels.

1. Pia watu kwenda marking sijui wanatumia kigezo Gani Kuna watu wapo wanafundisha miaka 10 HAWAJAWAHI KWENDA MARKING LAKINI KUNA WENGINE KILA MWAKA WANAENDA TU. HAPA KUNA TATIZO..

2. Vile vile Kuna watu wakienda mara moja wanasubirishwa miaka miwili mpaka mitatu ila wengine ni special hakuna kupitishwa hata mwaka mmoja.

3. ukabila upo Tena sana tu wenyeviti wa panel wasipotoka Kilimanjaro basi atatoka mara.

Kama mnazungumzia ukabila wa kupeana uenyeviti wa Panels Sawa, Ila sio watu kutoa marks kwa ukabila.

Embu waalimu Nyoosheni Maelezo
 
Masuala ya mitihani na usahihishaji ni siri kichogo wewe. Kama unahisi hakuna usawa ungelipeleka malalamiko sehemu husika na sio mtandaoni. Kumbuka kiapo ulichokula. Mwakani nyote mlioteuliwa mwaka huu hamtaingia tena.
unamtisha nani mjinga wewe ?
take care niko busy nitakujibu tukimaliza paka shume wewe
 
Uzuri pass record za Wanafunzi hua Zinaonekanaga Kuanzia first year mpaka mtihani wa mwisho wa NECTA.

Walio kua na Zero mitihani ya Ndani ndo hao hao, wanapata ZERO NECTA, sasa sijui anasema upendeleo gani.

Hata hivo, Muamko wa Elimu/Shule Kaskazini ni mkubwa kuliko sehemu nyingi
Tatizo
Zote zinapikwa kidini, kikabila na kikanda
Ndio maana makampuni na mashirika ya kimataifa yanashaanga mtu ana digrii hajui hata alichosomea
 
Necta iweke wazi yafuatayo kwa wanaohusika. ikizingatiwa kazi ngumu sana

1.per script ni sh ngapi?

2.muda sahihi wa kufanya kazi niliwahi pita centa moja markers wengi walilalamika kama wapo guantanamo bay.Kufanya kazi mda mrefu ili kumaliza mapema kabla ya sikukuu ni jambo jema ila ufanisi wa kazi uwa uko chini.ukizingatia mtu atakuwa amechoka.Iwekwe ratiba sahihi ya kuanza marking na kumaliza form two.Na form hivyihivyo

3.transpot allowance iwekwe wazi kumekuwa na ubabaishaji mwingi wengine wakisema mpk usafiri kilomete 1300 ndio ulipwe night +transprt allowance.

4.mwisho necta ichuje majina ya wasahihishaji yenywe isiwaaachie wenyeviti wa pannels
 
,...hizo hoja Zina mashiko ..mengine porojo.

BTW...Kumbuka NECTA iko kwa Mzanzibar. Naibu waziri je!?? Utaelewa tu. Usitarajie ufanisi.
 
Pambaneni na hali zenu, kazi yenyewe kila mwaka wanaenda watu wale wale licha ya mke wangu kufanya kazi ya ualimu Kwa zaidi ya miaka 10+ lakini hajawahi kuitwa ila wenzie kila mwaka wamo
Achana na kazi ya kimasikini hiyoo
 
Masuala ya mitihani na usahihishaji ni siri kichogo wewe. Kama unahisi hakuna usawa ungelipeleka malalamiko sehemu husika na sio mtandaoni. Kumbuka kiapo ulichokula. Mwakani nyote mlioteuliwa mwaka huu hamtaingia tena.
Si kweli. Acha uovu uovuliwe.
 
Hivi ni kiasi gani kwa makadirio mwalimu huwa anapata baada ya kutoka kusahihisha mitihani. Mbona malalamiko ni mengi hivyo
 
Nimejaribu kufuatilia panel mbali mbali za usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne na chapili ambapo nilianza kuhudhuria kama miaka kumi iliopita kama external niliouagundua huko ni mengi lakini kwa haraka nitaeleza machache.

1. Ukabila uliopitiliza kama mwenye kiti wa panel akiwa kabila fulani atajaza watu wa kabila lake mfano nimeudhuria panel ya biology na chemistry geography ukabila umeshika kasi kuna mwenyekiti wa pannel hizoni wachaga kwa kwahiyo wamejaza wachaga wa kutosha katika vitengo vyote vya maamuzi. na wamescreen watu wengi kutoka uchagani ndo maaana mikoa yao lazima ifanye vizuri.

2. Uhuni na umalaya uliopitiliza kuna uhuni na umalaya uliptiliza pindi watu wanapokuwa kwenye mapumziko hususani wakati wa wikiend.

3. Kuletwa wa mama wajawazito sijui wanakuwa ni wake za viongozi wa panel wakati shughuli yenywe inakatza watu wajawazito wasiudhurie.

4. Viongozi wa panell kuwapunja stahiki zao wanaofanya shughuli hiyo izogatiwa shughuli hiyo ni ngumu kwani haijulikani per script ni sh ngapi? nauli zinalipwaje'?

MY note baraza la mitihani lifanyoe kazi malalamiko hayo ikizongatiwa kazi ydnyewe ni ngumu
my note.
Necta iweke wazi yafuatayo kwa wanaohusika. ikizingatiwa kazi ngumu sana

1.per script ni sh ngapi?

2.muda sahihi wa kufanya kazi niliwahi pita centa moja markers wengi walilalamika kama wapo guantanamo bay.Kufanya kazi mda mrefu ili kumaliza mapema kabla ya sikukuu ni jambo jema ila ufanisi wa kazi uwa uko chini.ukizingatia mtu atakuwa amechoka.Iwekwe ratiba sahihi ya kuanza marking na kumaliza form two.Na form hivyihivyo

3.transpot allowance iwekwe wazi kumekuwa na ubabaishaji mwingi wengine wakisema mpk usafiri kilomete 1300 ndio ulipwe night +transprt allowance.

4.mwisho necta ichuje majina ya wasahihishaji yenywe isiwaaachie wenyeviti wa pannels
Hii hoja ina hoja za msingi ndani yake japo kwa jicho la mbali ni kama mtoa hoja umekosa fursa uliyozoea kuitwa ila mwaka huu umeachwa hivyo unatema nyongo.

Hoja za msingi ninazo ziona ni:-

1. NECTA kuweka wazi vigezo wanavyotumia kuwapata wasahihishaji. Hata kama wanasema ni kazi maalumu na ya SIRI lakini haitoshi kusema uzoefu kazini, uadilifu, bidii ya kazi ndio vigezo vya msingi. Walimu ni kundi kubwa na wanafahamiana utendaji kazi wao. Fulani anapoitwa kila mwaka wakati huyo huyo wanamjua performance yake ilivyo kazini ndio huzua malalamiko kama haya. Kama wanavigezo vyao waviweke wazi waache kujificha kwenye kivuli cha usiri kwasababu tayari walimu wanajua hakuna VETTING inayofanyika ndiomaana unakuta mjamzito, mgonjwa, aliyehama kituo barua kwenda kituo cha zamani, na wale wenzangu na mimi kazini kwa manati, tabia binafsi za ulevi uliopitiliza (hii maana yake hawana taarifa za muhusika za hivi karibuni)

2. Kuweka wazi maslahi watakayo yapata. Hili lilitakiwa lisomeke kwenye barua zao za uteuzi hata halina mjadala. Huwezi kuitwa kufanya kazi wakati hujui hata utalipwa kiasi gani. Hii inatengeneza ukondoo kwa walimu na inashusha hadhi ya kada husika. Kwamba wako tayari kwa chochote watakacholipwa bila kuhoji kwasababu hata hawajui kwanini wamechaguliwa?! Nadhani hii nayo ni hoja ya msingi

3. Kama wanaochuja majina ni hao wenyeviti sijui wanapatikanaje lakini kama ni miongoni mwa wasahihishaji walioitwa kwa kipindi husika, upendeleo hauwezi kukosekana. Kwa vile walimu wako wengi na hakuna Mwalimu asiyejua kusahihisha, hakuna mwalimu ambaye hajawahi kusahihisha. Nashauri NECTA wangejiwekea utaratibu wa kufanya rotation kwa hawa walimu. Naamini NECTA inawafanyakazi wanaosimamia shughuli hizi kila mwaka, hawa watumike kuweka kumbukumbu za nani kaenda lini na nani ataenda lini. Data base ya walimu wanayo, kila mwalimu awekwe kwenye mzunguko! Apangiwe ratiba yake (hii inabaki kuwa siri yao) ili kila mmoja hatimaye ashiriki kazi hii kwasababu ni kweli kundi hili halina namna ya kupata posho ya ziada zaidi ya kazi hizi za mwisho wa mwaka. Pia hii itaondoa unyonge kwa baadhi ya walimu na wengine kujiona bora kuliko wengine. Walimu wote wawekwe kwenye ratiba isipokuwa wale wenye special cases! Kama anasahihisha mitahani shuleni, kwanini asiende kusahihisha huko kwenye vituo? Si ndio atajengewe na uwezo wa kujua aboreshe wapi katika ufundishaji wake maana atasahihisha karatasi za wanafunzi wengi waliofundishwa na walimu tofauti. Kuwaacha wapweke vituoni ni kuwadumaza zaidi.

4. Hili la watu kuvunja amri ya sita kwa sababu yoyote ile liko kila mahali na mtu mzima hachungwi kwanza linaongeza morali ya kazi. Waache watu waondoe uchovu na sumu mwilini ili kazi iende sawia! Haliepukiki hata watoto wadogo wakiwekwa sehemu moja haya mambo hutokea sembuse kwa waliozoea kuichezea kila siku!!
 
Back
Top Bottom