Panya road 100 wakamatwa Temeke

Panya road 100 wakamatwa Temeke

Ropoka tu..siku mdogo wako alie kutembelea kwako akidakwa akapewa kesi ya mauaji ndio utajua umhimu wa The Rule of the Law & PGO
Listen bro km unafanya uhalifu wewe hata km ni ndugu yangu mimi nitakua mtu wa kwanza kukureport kutuoni waje wakuchukue... Usituletee ujinga hapa,
 
Huo ni uonevu. Ukamataji wa hovyo bila uchunguzi. Polisi ilikuwa wapi miaka zaidi ya 10 sasa? (Toka ile Clip ya Wanaume wa Dar es Salaam- Sauti ya mtu wa MARA).
Huwezi kurupuka uka kamata watu hovyo hovyo tu.
Dah umenikumbusha mbali sana. Ilkua 2014 au 2015 kama sikosei. Ile sauti ilikua inachekesha balaa.
 
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema ndani ya siku mbili zaidi ya wahalifu 100 wamekamatwa wakiwemo vijana wanaojiita ‘panya road’ ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo mbalimbali vya uhalifu wa kuvamia nyumba na kupora mali pamoja na kuwajeruhi watu

Source:

#EastAfricaRadio

MY TAKE :Najua wanatumia ule utaratibu wa general to specific kwamba unakamata wengi ila Target yako ni specific people ,Rai yangu kwa polisi upelelezi ufanyike haraka wapelekwe mahakamani ili wataokutwa na hatia sheria ichukuwe mkondo wake na wataokutwa Innocent waachiwe mara moja

View attachment 2358822
Keyser Söze
 
Wewe umejuaje km sio panyaroad? Emu acha polisi wafanye kazi yao usijifanye kujua mkuu ukipigwa panga kesho wewe ndio wa kwanza kuwarushia matusi polisi, ndugu yako akipigwa panga usiku wa leo wewe ndio wa kwanza kuwalilia polisi hawafanyi kazi... Waache polisi wafanye kazi yao
Unajifanya umetoka sayari ya Mars leo siyo? Hujui ufanyaji kazi wa polisi wa Tanzania. Kwa mtu anayetumia kichwa chake vizuri atajua kabisa huwezi kukamata panya road 100 kwa kipindi kifupi namna hiyo. Walifanya uchunguzi saa ngapi mpaka wakawajua. Hakuna mtu anayependa panya road lakini wakati mwingine hao polisi wanaweza kuwa hatari kuliko hao panya road.
 
Hakuna mtu anayependa panya road lakini wakati mwingine hao polisi wanaweza kuwa hatari kuliko hao panya road.
Sawa mkuu umeeleweka na unachokisema kina maana ila nao wana namna yao ya kufanya kazi waache polisi wafanye kazi yao, nakwambia leo ukivamiwa ukapigwa mapanga kesho uko Muhimbili kilio chako namba moja kitakua polisi hadi mimi napigwa walikua wapi? Kwa hio kaa kwa kutulia acha kuwatetea wahalifu acha polisi wafanye kazi wanajua wanachokifanya usiwafundishe kazi mkuu
 
dawa Yao ni moto tu...
magenge ya wavuta bangi yote yateketezwe maana hayo ndio mazalia ya uhalifu.
tunaliomba Jeshi letu la Polisi kusafisha vijiwe vya wavuta bangi,
 
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema ndani ya siku mbili zaidi ya wahalifu 100 wamekamatwa wakiwemo vijana wanaojiita ‘panya road’ ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo mbalimbali vya uhalifu wa kuvamia nyumba na kupora mali pamoja na kuwajeruhi watu

Source:

#EastAfricaRadio

MY TAKE :Najua wanatumia ule utaratibu wa general to specific kwamba unakamata wengi ila Target yako ni specific people ,Rai yangu kwa polisi upelelezi ufanyike haraka wapelekwe mahakamani ili wataokutwa na hatia sheria ichukuwe mkondo wake na wataokutwa Innocent waachiwe mara moja

View attachment 2358822
Waliotaka jela ni kuua kabisa hao.
 
Ndio uache kua panyaroad sasa wewe unatakaje watu waendelee kupigwa mapanga au wewe unataka nini muachwe muendelee kuua watu mtaani na kuiba na kujeruhi watu? Wewe km sio panyaroad unaogopa nini?
Nataka sheria na taratibu za kukamata zifuatwe.
 
Nataka sheria na taratibu za kukamata zifuatwe.
Sawa mkuu, sheria utazijua vizuri ukiwa ushadakwa kwani wakati unawapiga watu mapanga ulitumia sheria zipi au sheria unazijua baada ya kudakwa? Acha polisi wafanye kazi yao
 
Hao wahalifu wasishike group la vijana wadogo pekee kwa vile walikovamia wanasema wapo mpaka watu wazima na wazee na wamama wanaochora raketi hivyo wote wanaohusika washikwe Ili kuondoa mizizi yote.
Kazi ipo it seems Mtandao wao mkubwa na pengine kuna watu behind wanao wadefend in one way another
 
Tahadhari kivipi mkuu?
Kuna msako wa chini kwa chini dsm umeanza, hasa usiku kwenye maeneo ya starehe,mitaani hasa hii mitaa yetu ya kawaida, watu wamemwagwa si vizuri kutembea hovyo au kuwa karibu na watu au company usiyoifahamu hasa usiku mwingi, Kuna vijana tayari washachanganywa tena wengi tu.
 
Back
Top Bottom