Mcanada
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 982
- 1,942
Kwanza kabisa lazima tukubaliane kimsingi kuwa panya road ni school drop out hasa shule ya msingi na secondary, lakini wengi pia ni wale waliolelewa Kwa style ya single mothers hii nimeongea sio kukejeli lakini ni kutokana na mahojiano waliyofanya wenzao kituo Cha polisi.
Jana Tarehe 11.02.23 siku ambayo Simba ilifungwa huko Ugenini, Panya road walifanya matukio ya uvamizi na uporaji katika maeneo ya Bunju B.
Mimi najiuliza kwanini Hawa vijana wamekuwa wakatili kiasi hiki, yaani wakifanya uvamizi lazima wakuchororonge mapanga hata kama utakuwa mtiifu na kuwapa wanachotaka tofauti na majizi mengine.
Wao wakikufikia wanaanza na panga Halafu ndo wanadai Hela , simu, etc, pia wakishindwa kuchukua kitu wanakiharibu either Kwa kukipiga nyundo au kukikatakata.
Pia katika video hii hapa chini utaona Bado kuna Watanzania wachache wanakaa na hela ndani , mfano mmoja kuna mtu kakutwa na laki sita ndani, sijui ilikuwa ya matumizi ya kawaida sijui.
Pia najiuliza Hawa vijana walitumia mbinu gani kuweza kujikusanya wengi vile na kuunda timu yaani genge la wahalifu, hiyo sio kazi ndogo, huyo Kiongozi wao ana upeo fulani wa kipekee. Tunaita team building skills
Kwa jicho langu la kiusalama: Panya road ni kikundi cha kihalifu kinachofanya shughuli za ujambazi kwa low scale.. lakini pia baada ya kusikiliza hii clip nimechambua maelezo ya wahanga kwa jicho la usalama nimegundua kuwa hawa panya road ni biashara inayosukumwa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu kuwakomoa wananchi kwa kile kinachodaiwa kuwa wananchi wamekuwa wazito au kukataa kulipa hela ya ulinzi shirikishi..
Nashauri: Wananchi washinikize kazi ya ulinzi shirikishi irudishwe kwenye mtaa wao pia wao kama wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa kuhakikisha wanatoa michango yote inayohitajika na taarifa zote zinazohitajika hiyo itakuwa ni njia pekee ya kugundua nani anawatuma panya road na kumwajibisha kiongozi/viongozi wa mtaa huo kama matukio hayo bado yatakuwa yanaendelea .. waswahili wanasema Mchawi mpe mwanao akulelee, mwanao akifa tu ujue mchawi ndio kamuua..