Idd n,
Hawa magaidi hawana hoja...wanachokifanya ni kuleta kejeli, kuweka maneno ya kupumbaza, maneno ya kudumaza n.k
Mara nyingi huwa wanafanya hivyo kwa kuchangia, ni kundi au niseme ni genge, wana ma iD lukuki tu za kurusha vijembe maneno mengi n.k Lakini kikubwa ni Jumbe zao. Lengo kuu ni kudumaza Jamii tajwa....kwa kufanya kufanya Ugaidi wa matabaka. Ugaidi wa Tamaduni. Ugaidi wa Mila n.k
Kinachosikitisha ni pale vyombo vya habari, viongozi katika nyanja zao mbali mbali kuanza kuhemeka na kurudia ujumbe wenye lugha na misamiati ya Ukimbari. Ni aibu kubwa Kiongozi yeyote yule kutumia msamiati wa Panya Road. Ni faraja kubwa kwa hawa mabeberu na magaidi wa mtandao kwani huwa wanatumia vielelezo vyao kama haki kwao kuendeleza ugaidi huo...kuna mapungufu gani wakisema hao wanaofanya hivyo ni Majambazi?.
Viongozi wao wanaeleweka, nashauri TCRA wafanye kazi kweli kweli.
Idara zenye wajibu wa kuzuia Ugaidi wafanye kazi mara mbili ya hapa, sio kuweka usalama kwa Viongozi wa siasa bali Jamii nzima kwa Ujumla.
Tujifunze kuenda sambamba nao, wakibadilisha mbinu, spidi, jumbe(ujumbe) na misamiati yao...yaani tuende nao bega kea bega, kwata kwa kwata, risasi kwa risasi ....kwani Hawa ni maadui wa Taifa natu wachukulie hivyo.
Aluta Continua