Ngoja niwaambie kitu kimoja pengine watu hawajui, binafsi nimekulia sana kitaa hao panya road ni wadogo zetu, kaka zao uo upuuzi tushauacha saivi tupo tunaendesha boda boda na wengine tunajishughulisha na shughuli zingine yani usela tushaacha wengine washaenda maisha ya mbele n.k wachache sana bado wapo ktk uhuni,
Panya road ni vijana wa miaka 16-24 wale wa 28-35 ndo baadhi kama viongozi na wengine ndo wanajiita matembo hawa hawafanyi uahalifu wao wanawatoa madogo chambo
Hawa madogo hawana roho ya huruma hata kidogo yani wametuzidi hadi kaka zao enzi zetu uhuni wetu haukuwa kiwango iki mpka tunawaogopa
Hawa watoto wamekulia katk uhuni wameanza kuvuta bangi mapema sana, wameshuhudia matukio mengi tofauti na umri wao, yani wamevaa roho za kishetani mapema sana, yani akikushikia kisu huwa ni nadra sana kirudi bila damu,
Sasa kilichopo ni kwamba wana hasira na wananzengo maana waidokoa wakidakwa ni kifo so na wao wakiingia sehemu watu lazima mchakae ,
Kwaiyo ni kisasi na wizi, hao wanaovamia bunju hawakai bunju unakuta wanatoka sehem za uswahilini, wanakinukisha kila mtu anarudi ktk shimo lake,
Hii trend itaenda watazoea damu za watu wataona kawaida watatamani kuona damu zaidi hapo ndipo mauaji yanapoanzia, polisi wakiwamata au raia wakiwauwa kisasi kinazid kuchochewa,
Kuwapata kwao au ukitaka kuwashuhudia mmoja auwawe alafu wamwache akazikwe na raia ndo utakapo waona panya road live , sasa kumjuwa yupi ni yupi ndo kazi ilipo ,wale ambao ni konki huwa wanakaa kimachale machale sana hata difenda zikija ni nadra sana wakamatwe wao, watakamatwa wavuta bangi tu ila panya wenyewe unakuta washa escape kitambo
Yani bora liwepo hata likiwanda linaloweza ajiri watu elfu tano wazolewe wakakae uko kama kambi wawe bize bila ivo
Shughuli ipo