Panya road wanauawa kwa risas. Je, wezi wa mabilioni ya kodi za Watanzania wanabakije salama?

Tena huwa wanasifiwa kuwa ni Wajanja !!
 
Watu weusi tuna ila kichwani mkuu!
 
Mkuu ushasikia fisadi amekata mtu mapanga? Au kumuua mtu live kisa aibe hela. Hii story ndo headline ya panyarodi., yani wakikushika lazima wakutie kilema.
 
Kwa kweli kwa matukio niliyoyashuhudia ya hawa vijana wanaoitwa panya road Sina huruma nao hata chembe na hata siwezi kumuombea adui yangu kukutana nao.....

Ukitazama kwa jicho la kibinadamu ni kama wanafanyiwa ukatili lakini ukishuhudia matukio yao na wahanga wa hayo matukio nafsi yako inabadilika hapo....

Kwa kifupi ikitokea umekutana nao ni tukio la kufa au kupona........

Haki na ustawi kwenye jamii ni pamoja kila mmoja kuheshimu haki na usalama wa wengine.....

Najaribu kulaani vitendo vya polisi lakini nikivaa viatu vya wahanga na majeraha wanaoyouguza naishiwa nguvu kabisa.....
 
Bokoboko mabapa mixer mabanzi ila pilau kwa kua lina viungo vingi unakatwakatwa .Jamaa yangu alikutana nao akachagua pilau aisee usiombe.Halafu hawa chupi sijui wanasema nini hawa.
Hahahahahah dah kmmmk walai,
 
Reactions: EEX
Bokoboko mabapa mixer mabanzi ila pilau kwa kua lina viungo vingi unakatwakatwa .Jamaa yangu alikutana nao akachagua pilau aisee usiombe.Halafu hawa chupi sijui wanasema nini hawa.
🤣🤣🤣 kumbee ndo inamaanisha hivi. Bora umetuambia siku nikukutana nao bora nichague bokoboko.

Mamæ zao panya road
 
Sawa mkuu!

Je hawa wanaoiba pesa zetu za kodi ambazo zingesaidia kununua vifaa Tiba ili kuondoa vifo vya watoto, wajawazito na wagonjwa mbalimbali wanaokosa huduma mahospitalini, watu hawa sio wauwaji.?
 
Wangekuwa wanaua watu live story ya fisadi isingekuwepo.
Sawa mkuu!

Je hawa wanaoiba pesa zetu za kodi ambazo zingesaidia kununua vifaa Tiba ili kuondoa vifo vya watoto, wajawazito na wagonjwa mbalimbali wanaokosa huduma mahospitalini, watu hawa sio wauwaji.?
 
Acheni kutetea ujinga, hao wezi wa mabilioni wamemshikia nani panga, hao wezi wa mabilioni wamembaka nani?? Hujasiki mama na mtoto wakibakwa na hao panya road??.. pesa zinatafutwa lakini uhai wa mtu haupatikan popote ukishapotea, hao unaosema wezi wa mabilioni si unaona wanakufa na kuyaacha tunaanza kung'ang'aniana Tena. Panya road wafe TU hao wezi wa mabilioni tutajua namna ya kudili nao tu
 
Hayo mabilioni wangetumia kuwapa watu Maisha mazuri usingewaona hayo wakata mapanga.
Good!

Majizi mengine huwa yanatengenezwa na mifumo mibovu ya serikali,

Hayo mabilioni yanayoibwa, kama yangelitumika kuboresha huduma, mishahara ya wafanya kazi n.k

Mambo mengine hupotea tuu automatically
 
Wote wachapwe shaba tuu! Hakuna cha aliye nafuu hapo

Kwani hujui pia hao wezi wa mabilioni nao ni wauwaji?
 
Kuna kundi linajinasibu sana kila siku sijui tozo zinaibiwa, sijui serikali ni wezi lkn siku ukiwadaka walete ushahidi utaskia nilisoma jf,

Siku nimeamini wanasiasa ni wabaya sana ni baada ya kelele za lowasa ni fisadi apoapo wao wakamchukua waliokunae nao wakamuita fisadi wakatuahidi watafungua na mahakama spesho kwa ajili ya watu wa aina yake lkn mpaka sasa hivi ile mahakama imeishia vichochoroni na lowasa anatesa tu mtaani, pengine hakuwahi hata kuiba sh 10 ya mtu

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Wote wachapwe shaba tuu! Hakuna cha aliye nafuu hapo

Kwani hujui pia hao wezi wa mabilioni nao ni wauwaji?
Akiingia kwenye rada zako mpe Shaba tu, ila sijui kwenye hilo nani atapona Maana watanzania asilimia kubwa ni wezi, unaweza kumnyooshea huyo anayeona anaiba nyingi unajisahau wewe unayemuibia muhindi, fundi ujenzi anamuibia boss wake kwa kutaja bei kubwa ya vifaa tofauti na Bei halisi, muuza duka naye atamuibia boss wake na boss wake naye anamuibia boss wake, sisi tumeanza na wanaotumia mapanga na kutudharirisha
 
Sawa mkuu!

Je hawa wanaoiba pesa zetu za kodi ambazo zingesaidia kununua vifaa Tiba ili kuondoa vifo vya watoto, wajawazito na wagonjwa mbalimbali wanaokosa huduma mahospitalini, watu hawa sio wauwaji.?
Kosa halishindanishwi na kosa bali kwa kutatuliwa.......uharaka wa kushughulika kosa unatokana na madhara ya kosa kwa muda huo......wezi wa mabilioni ni watu wabaya sana na wa kuangamiza lakini madhara yake yanakwenda kwa process kuweza kuyaona......lakini unakutana nae hapo anakukata mkono na kuchukua kilicho chako......hawa wote ni waharifu lakini wanashughulikiwa kwa namna tofauti......

Kwa mfano mwanasiasa anaweza akahujumu mradi leo na kujipatia mamilioni.....baada ya mwaka unapita uchunguzi wa mkaguzi mkuu wa serikali na kubaini na baadae inaundwa tume kuchunguza kwa kina inayochukua miezi kadhaa alafu waandae mashtaka.......

Lakini kibaka panya road anashika kisu anakuchoma wakati unagala gala kwenye dimbwi la damu ukipigania pumzi yako yeye anachukua Mali zako na kukimbia je watu Hawa wanapaswa kufananishwa.......???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…