Panya Road wavamia Bunju Magengeni, maduka yafungwa kwa kuhofia usalama

Yaan momepita hapo Bunju B Kama do 10 zilizopita, nimeona heka heka, defender na police wengi, aisee... Amani ni kitu muhimu Sana.
Hivi kumiliki Bastola masherti yake ni yapi?
"Amani haiji ila kwa ncha ya upanga"; walisema wahenga.
 
Kila mkoa kwa sasa una panya road sio rahisi kuwazibiti hao madogo nikama maroboti hawaogopi kabisa kifo
 
KhaKhaKhaa; Polepole jamani. Huyo alikuwa anainusuru nafsi yake kwanza. Gari si atanunua nyingine ila sio roho yake. Panya rodi wapo pia wanawake au ???.
Wakati ananijibu hakufikiria mara mbili usalama wa watu wengine,kwani nilishindwa kuchukua gari na kuondoka,ndio maana simu niliiacha kwa kuwa kukimbia naweza kuangusha simu.
 
Hivi hawa ni panya road au kuna kikundi cha uhalifu kikubwa kinapoozwa kwa kuitwa 'panya road'? Kwa ninavyojua mimi, sidhani kama kuna kijana wa kitanzania ambaye wataji organise wawe na mapanga bila nguvu ya kundi kubwa la kihalifu nyuma yao.
Kweli kabisa. Huo uthubutu haupo kwa vijana wa ki-Tz.
 
Dawa yao hao ni kuwauwa tu washenzi hao
 
Aaaah! Mjomba, Mpaka uje kuimiliki hiyo bastola kwa urasimu uliopo; hao panya watakuwa wesha sepa. Ww anza hata na panga, rungu, nondo, mshale, gobore n.k. twanga wapuuzi hao.

Usiwe na ‘Gobore’ utaenda jela wewe.
 
Kataa wahuni, piganieni ipatikane KATIBA MPYA ndio mwarobaini wa migogoro yote hii. Huwezi kutumia ASILIMIA 90 ya bajeti kwenye ANASA tu, na kwenye maendeleo upeleke pesa kiduchu halafu utarajie mambo yatakuwa sawa tu.
Bila katiba mpya PANYA ROAD wataendelea kuongezeka maelfu kwa maelfu hadi akili zitakapowakaa sawa..


 
Mnalipa kodi halafu hamlindwi na mali zenu na roho zenu zinachukuliwa

Hivi hamna uchungu? Na mtakuwa hivyo wa hewala mpaka lini
Hayo ndio madhara ya KATIBA DHAIFU, watawala wamelala tu hakuna uwajibikaji. Acha panya road waendelee kuwapelekea moto labda akili zitakuja
 
Unalipa kodi serikali inashindwa kukuhakikishia usalama halafu unaona sawa, puumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…