Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Wala hujajibu swali nililokuuliza.Kwanza ni lazima uelewe vita haipendwi na wengi isipokuwa ni viongozi ndio huichochea na kuihamasisha sasa tujiulize viongozi hao hawaendi kanisani na je wakienda kanisani papa hawaambii livelive kwamba haifai haifai haifai kumwaga damu za askari wetu badala yake papa ndo anaweza kwenda kuwaombea na kuwatakia heri katika vita..
Swali jingine. Umeshawahi kusoma Agano la Kale? Kule ni vita tupu kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mbinguni kwenyewe shetani alikiwasha na aliposhindwa ndo akatupwa duniani pamoja na wafuasi wake. Duniani hapa tumo katika vita kati ya wema na ubaya. Hata kinafsiya tunapambana na vita. Vita (ukinzani) - hasi na chanya ndiyo muundo wa ulimwengu!
Vita vya pili vya dunia ilikuwa lazima vitokee hata kama Papa angefanya nini. Sasa unamlaumu Papa kwa Italy kuingia katika vita utafikiri Papa alikuwa kiongozi wa Italy wakati hakuwa/hana usemi wo wote huko.
By the way Vatican haikuunga mkono vile vita bali wali-adopt siasa ya kutokuunga upande wo wote (neutrality) hasa ukizingatia kuwa Adolf Hitler alikuwa anawakoromea hapo hapo Rome mpaka Bennito Mussolin alipoamua kujiunga naye....
Hitimisho: Hata kama una chuki na upapa hii hoja eti kwa vile Italy iliunga mkono vita basi somehow Vatican inapaswa kulaumiwa haina mashiko.
Kwa heri!