Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

Kwanini ushoga usiruhusiwe tu? Maana watu wanaupenda sana
 
Msimamo wa Papa Francis nauelewa vizuri sana, hayupo mwenye dhambi anayetakiwa kutengwa, hata Yesu Kristu hakuja duniani kwa ajili ya wenye haki, alikuja kwa wenye dhambi ili wapate kuokoka...
"We cannot be judges who only deny, reject and exclude," he said.

He added, however, that the Church still considered same-sex relationships "objectively sinful" and would not recognise same-sex marriage.
 
Subirini Papa atakapoanza kumtukana YEHOVA-YESU waziwazi ndipo akili zitawakaa sawa.

Matusi na maneno ya makufuru si mnajua?

Hakuna hoja yoyote inayohalalisha wewe kuwa karibu na mwenye DHAMBI ambaye Hana mpango wa kuacha DHAMBI, hakuna hoja hiyo katika BIBLIA TAKATIFU.

1 Kor 6:9-11​

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa

Na tena...

2 Kor 6:14-18​

Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi
 
Ikumbukwe huyu Papa wa Vatican anaeongoza Kanisa la RC almaaufu Kanisa Takatifu la Mitume kama wanavyojiita wao ameamua kuwaburuza wenzake wafuate msimamo wake.

Baadhi ya mambo ambayo anataka Kanisa lake lifuate ni

- Kuwatambua Mashoga bila kukemea akisema wenye dhambi ndio wanatakiwa kwenda kanisani

- Kubariki Ndoa za mashoga

- Kufuhusu utoaji Mimba

- Kutambua watu Waliobadili Jinsia kinyume na maumbile Yao ya Asili

- Kuwa na msimamo legelege na kuficha taarifa za watawa wanaokumbwa na kashfa za kulawiti Watoto wadogo.

- Kufuhusu Baadhi ya Maaskofu wa RC huko Amerika ya Kusini kuoa kinyume na msimamo wa Kanisa lao Hilo la Mitume.

Haya wenye Kanisa lenu johnthebaptist mnaitwa huku 😁😁

======
Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa aliyeibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani alilokuwa akiliongoza .

Askofu Strickland ni mmoja kati ya sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.

Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.

Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

"Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema.

Kwa mujibu wa Vatican, uamuzi wa kumfukuza umefikiwa baada ya “ziara ya kitume katika Jimbo la Tyler iliyoagizwa na Papa mwezi Juni".

Vyombo vya habari vya Kikatoliki vinaeleza kuwa uchunguzi huo pia uliangazia masuala ya kifedha katika jimbo hilo.

Askofu Strickland, 65, aliteuliwa kuwa askofu mwaka 2012, wakati wa Papa Benedikto XVI.

Vatican imesema kuwa Jimbo la Tyler kwa sasa litaongozwa kwa mpito na Askofu Joe Vasquez wa Jimbo la Austin.

Hatua hii inafuatia hatua mahususi zinazochukuliwa na Papa ili kulifanya Kanisa Katoliki kuendana na wakati kwenye utawala wake.

Siku ya Alhamisi, Vatican ilitangaza kuwa watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa katika Kanisa Katoliki ilimradi kwa kwa kufanya hivyo hakutazua kashfa ama “mchafuko”.

Mwezi Oktoba Papa alisema kuwa Kanisa linaweza kukubali kubariki wanandoa wa jinsi moja, huku akiwaeleza makardinali kuwa "hatuwezi kuwa majaji ambao tunachofanya ni kukana, kukataa na kutenga tu".

Akizungunza katika mkutano wa Siku ya Vijana Duniani jijini Lisbon Papa alisema kuwa mgando wa fikra wa baadhi ya watu “hauna manufaa”.

"Kwa kufanya hivyo unapoteza utamaduni halisi na utategemea itikadi ili kuungwa mkono. Kwa maana nyingine, itikadi inachukua nafasi ya imani,” aliongeza kusema.

Mabadiliko ya tabianchi pia imekuwa ni moja ya ajenda kuu ya utawala wa Papa Francis - ambapo mwaka 2015 alitoa chapisho muhimu kuhusu mazingira ambalo lilionya kuwa dunia ilikuwa inaelekea hatua mbaya zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Papa pia amewashutumu vikali wale wote wanaokanusha mabadiliko ya tabianchi na anatazamiwa kuwa katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28 baadae mwezi huu huko Dubai.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuhudhuria toka mikutano hiyo ianzishwe mwaka 1995.

Chanzo: BBC
Tunajadili hoja za kisomi siyo za kidini kwa hiyo peleka dini yako mbali na huu mjadala

"We cannot be judges who only deny, reject and exclude," he said.
He added, however, that the Church still considered same-sex relationships "objectively sinful" and would not recognise same-sex marriage.
 
Abaki na misimamo yake.....neno lake lisiwe neno la kanisa
"We cannot be judges who only deny, reject and exclude," he said.


He (Pope Francis ) added, however, that the Church still considered same-sex relationships "objectively sinful" and would not recognise same-sex marriage.
 
Mimi ndio maana huwa nasema tatizo sio dini kuwa mbaya bali watu ndio wabaya. Hata kwa wenzetu waislam sidhan kama dini yao mbaya bali kuna maislam mapumbafu..ndio sawa na huyu papa mapumbu mpinga kristo.

Heko kwake padri Strickland hakubaliani na mausenge ya Papa mkubwa wake. Ukatoliki utabaki ila huyo papa ataenda zake na wenzake wanaokubaliana upotofu
 
"We cannot be judges who only deny, reject and exclude," he said.


He (Pope Francis ) added, however, that the Church still considered same-sex relationships "objectively sinful" and would not recognise same-sex marriage.
Sijui kizungu kaka
 
Mimi ndio maana huwa nasema tatizo sio dini kuwa mbaya bali watu ndio wabaya. Hata kwa wenzetu waislam sidhan kama dini yao mbaya bali kuna maislam mapumbafu..ndio sawa na huyu papa mapumbu mpinga kristo.

Heko kwake padri Strickland hakubaliani na mausenge ya Papa mkubwa wake. Ukatoliki utabaki ila huyo papa ataenda zake na wenzake wanaokubaliana upotofu
"We cannot be judges who only deny, reject and exclude," he said.
He added, however, that the Church still considered same-sex relationships "objectively sinful" and would not recognise same-sex marriage.
 
Back
Top Bottom