Kwanza, sodoma haikuangamizwa kwa sababu ya ushoga.
Ngoja nikuombe ombi moja juu ya kadhia hii. Nakuomba usiweke maoni yako bali weka andiko na marejeo.
Pili, nitakapo kuuliza maswali ujibu na mimi nina kuahidi nitajibu kila swali utakalo niuliza,ikitokea sijajibu nikumbushe.
Ushoga maana yake nini ? Je ni kumuingilia mwanume mwenzako kwa idhini yake huku wakifurahi jambo hilo au kinyume chake ?
Ubakaji tunaujua na ungekuwa ni ubakaji basi habari zingetufikia kwamba hilo lilikuwa linafanyika kwa Wanawake, lakini hilo lilikuwa linafanyika kwa wanaune wao kwa wao.
Anasema katika Qur'aan juu ya kisa cha nabii Luti na watu wake.
165. Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
166. Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!
167. Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!
168. Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu.
169. Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.
170. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
171. Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
172. Kisha tukawaangamiza wale wengine.
173. Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
174. Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
175. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. (Ashu'raa : 165 - 175 )
Sasa naomba unipe ushahidi wako unao onyesha ya kuwa watu hao waliangamizwa kwa sababu nyingine na si ushoga. Maana wale malaika walitumwa kwa ajili ya jambo hilo, na si wageni tu ilimradi ndiyo maana walimwambia nabii Luti, atoke katika ile miji na watu wake.