Mkuu,
Mimi ninataka kujifunza jambo haswa kulingana na chimbuko halisi la dini ya Islam. Hii itatupa picha halisi bila kuwa bias ni nani walikuwa waanzilishi wa mwanzo kabisa wa hesabu katika karne nyingi sana zilizopita.
Sina shaka na Misri ya zamani maana mambo makubwa ya kihistoria yamefanyika huko, hesabu pamoja na maandishi ya kale pia.
1. Je, ni kweli Islam ilikuja baada ya Mtume Muhammad (saw) kuzaliwa?, au ni dini iliyokuwepo tangu awali hata kabla ya kuzaliwa kwa mtume?
2. Quran kama kitabu cha muongozo kwa Muslims, kiliteremshwa kipindi cha Muhammad (saw), au ni kitabu kilicho kuwepo karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa mtume?.
3. Mwisho kabisa, Islam kama dini ilianza karne ya ngapi, na hizi hesabu zinazo zungumziwa zilikuwepo Misri ya zamani na Mashariki ya mbali zilianza karne ya ngapi?.
Natanguliz shukran.
Nakujibu kama ifuatavyo
1) Uislam ulikuwepo kabla ya Mtume Muhammad ajazaliwa
Qurani 42:13
- Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.
Hapo mtume Muhammad anaambiwa hi dini ya uislam yeye sio wa kwanza mitume wote waliomtangulia walikuwa waislam
Na hapa wengi huwa mnachanganya Muislam wa kwanza Kwa wanao ifuata Quran ni mtume Muhammad
Ila waislam wa kwanza Duniani kabla ya Mtume Muhammad wapo wengi
2) Allah ameleta vitabu 4 hapa Duniani
Taurati amepewa nabii Musa
Zaburi amepewa nabii Daudi
Injili amepewa nabii Isa
Quran amepewa nabii Muhammad
Hivyo basi Muhammad Saw ndio mtume wa mwisho na Quran ndio kitabu Cha mwisho
3) Hesabu duniani zilikuwepo za aina nyingi hata mababu zetu wa hapa Tanzania naamini walikuwa na hesabu zao
Ila hasabu kuu hapa Duniani ni za aina 2 Yani za Kirumi na ndio hesabu za kwanza hapa Duniani na za Kiarabu Yani algebra
Hesabu za Kirumi zilifeli Kwa sababu hazinyumbuliki Yani hauwezi kutumia hesabu za Kirumi kufanya Calculation kubwa kubwa
Hesabu za Aljebra ndio zikafiti Kila sehemu na Kila aina ya Calculation hesabu hizi waanzilishi ni wasomi wa Misri Kwa msaada wa Quran katika miaka 830
The word "algebra" is derived from the Arabic word الجبر al-jabr, and this comes from the treatise written in the year 830 by the medieval Persian mathematician, Al-Khwārizmī, whose Arabic title, Kitāb al-muḫtaṣar fī ḥisāb al-ğabr wa-l-muqābala, can be translated as The Compendious Book on Calculation by Completion
Source website ya Cambridge university