PreGE2025 Pascal Mayala: Mateso ya kumuuliza swali Magufuli. "Niliumizwa, Kampuni yangu ilitolewa Sabasaba, Mikataba ikavunjwa. Sijapona hadi leo"

PreGE2025 Pascal Mayala: Mateso ya kumuuliza swali Magufuli. "Niliumizwa, Kampuni yangu ilitolewa Sabasaba, Mikataba ikavunjwa. Sijapona hadi leo"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Magufuli alikuwa kama shetani. Lakini pamoja na ushetani wake, alikuwa wakati mwingine kuna maamuzi yake yalikuwa ni sahihi. Huyu Pasco ni mmoja ya watu wajanja wajanja na wanaojipatia fedha kwa ujanja ujanja. Kama hizo fedha alizokuwa analipwa na serikali zilikuwa ni mchongo wa kupiga fedha tu. Magufuli japo alisukumwa na hasira za kuulizwa swali, lakini ni kweli jamaa alikuwa anapiga fedha za serikali kwa ujanja.
Mayala aligundua kuwa madhila yaliyomkuta hayakuwa maelekezo ya Magufuli.
 
Magufuli alikuwa kama shetani. Lakini pamoja na ushetani wake, alikuwa wakati mwingine kuna maamuzi yake yalikuwa ni sahihi. Huyu Pasco ni mmoja ya watu wajanja wajanja na wanaojipatia fedha kwa ujanja ujanja. Kama hizo fedha alizokuwa analipwa na serikali zilikuwa ni mchongo wa kupiga fedha tu. Magufuli japo alisukumwa na hasira za kuulizwa swali, lakini ni kweli jamaa alikuwa anapiga fedha za serikali kwa ujanja.
Ujanja ujanja,ingekuwa kila kitu kipo ki halali hasingeweza kufirisika kiasi hicho
 
Shetani hana Rafiki, Mayalla tulimuonya sana kuhusu ccm lakini akaweka pamba masikioni.

Asimlilie mtu
Nyie si ndio mlikuwa mnamjaza upepo kwa kumpa hongera baada ya kuuliza hayo maswali yake magumu. Tena wewe ulikuwa unasisitiza halijajibiwa 🐼
 
Nimesikitika sana kusikiliza Mahojiano ya Stanstaus Lambert na Pascal Mayalla.

Kwa ufupi, anadai kuwa baada ya kumuuliza Rais Magufuli maswali kuhusu jinsi anavyoingilia uhuru wa Mihimiki Mingine, Press card yake ilichukuliwa na Mamlaka.

Alikuwa na kampuni inayofanya consultants kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo 5 za Serikali ambapo alikuwa analipwa Mamilioni ya shilingi kila mwezi. Mwezi mmoja baada ya kuuliza swali lile Ikulu, alipokea barua 6 kutoka kwa kampuni hizo kumtaarifu zinavunja Mkataba naye, na zikasema hazimlipi fidia yoyote isipokuwa kampuni moja tu ndiyo ilimlipa.

Baada ya sakata hili, kampuni yake iliyoajiri watu 20, akilipa kodi ya ofisi ya zaidi ya Tsh. Milioni 3 kwa mwezi Ilibidi ihame ofisi na kwenda kupanga kijichumba kidogo, ikabidi abaki na watu 5 tu.

Haikuishia hapo, akapigwa pin kuonekana viwanja vya sabasaba, na alijua hili baada ya kwenda kama raia wa kawaida, lakini askari walimtaka asionekane pale tena.

Kwake yeye anasema alifanya juhudi za kumfikia Rais Magufuli ili aone nini hasa tatizo, akagundua hayakuwa maelezo yake isipokuwa watu wanaodhani wanamsaidia Rais kumbe wanamharibia.

Ameonya kuwa hata sasa kuna watu wanaodhani wanamsaidia Rais Samia lakini kiukweli wanamharibia, na si kila baya linalofanyika huwa na baraka za Rais. Rejea mfano wake wa wapambe wa Magufuli walivyomfanyia mabaya.

Kwasasa amerudishiwa press card yake, kaamua kuanza upya.

View attachment 3343264

Swali alilouliza

Hayo ni maelezo ya upande mmoja wa Mayalla. Hakuna uthibitisho wowote au kusikia upande wa pili.
 
Back
Top Bottom