PreGE2025 Pascal Mayala: Mateso ya kumuuliza swali Magufuli. "Niliumizwa, Kampuni yangu ilitolewa Sabasaba, Mikataba ikavunjwa. Sijapona hadi leo"

PreGE2025 Pascal Mayala: Mateso ya kumuuliza swali Magufuli. "Niliumizwa, Kampuni yangu ilitolewa Sabasaba, Mikataba ikavunjwa. Sijapona hadi leo"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sio dunia sema afrika, kwa mfano hspa kwetu sa100 amezungukwa na genge la propaganda balaa...na washamjulia anapenda kusikia nn wanatembelea mulemule, mbaya zaidi huku wanatafuna kodi za wanyonge!
SA100 hakubaliki kwa wananchi wa maisha ya chini...ni ulaghai tu mtupu.
Hilo ni swala la kidunia Mkuu, soma kitabu cha The Prince by Nicolo Machiavell (kama sijakosea jina) utaona.

Hata kwenye vitabu vya dini manabii wengi waliotumwa na Mungu kuwakemea na kuwapa habari wafalme walikuwa ni watu wa kuhadaa sana na kulaghai.

Ukiwa mhafidhina utapata wakati mgumu sana duniani, inatakiwa uwe grand au tuseme uwe na msimamo wenye liquid form.
 
Mayala akitaka kujua kuwa JPM alikuwa anahusika au hahusiki katika ishu yake akamuulize Anthony Diallo.

Diallo amewahi kuelezea kwenye clubhouse sakata lake la account zake za benki kuzuiliwa na TRA enzi hizo. Diallo alipompugia JPM, JPM akajifanya hajui kinachoendelea, ila alipowatafuta watu wa TRA baadae wakamwambia huyo JPM anayejifanya hajui pindi ukiongea nae, ndo huyohuyo anatoa maagizo kwa TRA wazuie pesa zake!.

JPM alimaster sanaa ya deception.
 
Nimesikitika sana kusikiliza Mahojiano ya Stanstaus Lambert na Pascal Mayalla.

Kwa ufupi, anadai kuwa baada ya kumuuliza Rais Magufuli maswali kuhusu jinsi anavyoingilia uhuru wa Mihimiki Mingine, Press card yake ilichukuliwa na Mamlaka.

Alikuwa na kampuni inayofanya consultants kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo 5 za Serikali ambapo alikuwa analipwa Mamilioni ya shilingi kila mwezi. Mwezi mmoja baada ya kuuliza swali lile Ikulu, alipokea barua 6 kutoka kwa kampuni hizo kumtaarifu zinavunja Mkataba naye, na zikasema hazimlipi fidia yoyote isipokuwa kampuni moja tu ndiyo ilimlipa.

Baada ya sakata hili, kampuni yake iliyoajiri watu 20, akilipa kodi ya ofisi ya zaidi ya Tsh. Milioni 3 kwa mwezi Ilibidi ihame ofisi na kwenda kupanga kijichumba kidogo, ikabidi abaki na watu 5 tu.

Haikuishia hapo, akapigwa pin kuonekana viwanja vya sabasaba, na alijua hili baada ya kwenda kama raia wa kawaida, lakini askari walimtaka asionekane pale tena.

Kwake yeye anasema alifanya juhudi za kumfikia Rais Magufuli ili aone nini hasa tatizo, akagundua hayakuwa maelezo yake isipokuwa watu wanaodhani wanamsaidia Rais kumbe wanamharibia.

Ameonya kuwa hata sasa kuna watu wanaodhani wanamsaidia Rais Samia lakini kiukweli wanamharibia, na si kila baya linalofanyika huwa na baraka za Rais. Rejea mfano wake wa wapambe wa Magufuli walivyomfanyia mabaya.

Kwasasa amerudishiwa press card yake, kaamua kuanza upya.



Swali alilouliza
 
Shetani hana Rafiki, Mayalla tulimuonya sana kuhusu ccm lakini akaweka pamba masikioni.

Asimlilie mtu
Magufuli alikuwa kama shetani. Lakini pamoja na ushetani wake, alikuwa wakati mwingine kuna maamuzi yake yalikuwa ni sahihi. Huyu Pasco ni mmoja ya watu wajanja wajanja na wanaojipatia fedha kwa ujanja ujanja. Kama hizo fedha alizokuwa analipwa na serikali zilikuwa ni mchongo wa kupiga fedha tu. Magufuli japo alisukumwa na hasira za kuulizwa swali, lakini ni kweli jamaa alikuwa anapiga fedha za serikali kwa ujanja.
 
Nimesikitika sana kusikiliza Mahojiano ya Stanstaus Lambert na Pascal Mayalla.

Kwa ufupi, anadai kuwa baada ya kumuuliza Rais Magufuli maswali kuhusu jinsi anavyoingilia uhuru wa Mihimiki Mingine, Press card yake ilichukuliwa na Mamlaka.

Alikuwa na kampuni inayofanya consultants kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo 6 za Serikali ambapo alikuwa analipwa Mamilioni ya shilingi kila mwezi. Mwezi mmoja baada ya kuuliza swali lile Ikulu, alipokea barua 6 kutoka kwa kampuni hizo kumtaarifu zinavunja Mkataba naye, na zikasema hazimlipi fidia yoyote isipokuwa kampuni moja tu ndiyo ilimlipa.

Baada ya sakata hili, kampuni yake iliyoajiri watu 20, akilipa kodi ya ofisi ya zaidi ya Tsh. Milioni 3 kwa mwezi Ilibidi ihame ofisi na kwenda kupanga kijichumba kidogo, ikabidi abaki na watu 5 tu.

Haikuishia hapo, akapigwa pin kuonekana viwanja vya sabasaba, na alijia hili baada ya kwenda kama raia wa kawaida, lakini askari walimtaka asionekane pale tena.

Kwake yeye anasema alifanya juhudi za kumfikia Rais Magufuli ili aone nini hasa tatizo, akagundua hayakuwa maelezo yake isipokuwa watu wanaodhani wanamsaidia Rais kumbe wanamharibia.

View attachment 3343264

Swali alilouliza

Hata wauaji pia hufiwa.
 
Back
Top Bottom