Pascal Mayalla alimtabiria Paul Makonda kuwa mgombea urais wa CCM 2025. Je, unabii wake utatimia?

Kwa trend hii ya sasa, by 2025 "mabeberu" watakuwa tayari washatuvuruga siku nyingi.... hapo itakuwa hakuna cha CCM wala Chadema!
 
CCM pamoja na madhaifu yao hawawezi kufanya huu ugoro. To even think and predict (prophesize in Rashid Gwajima’s World) kwamba Bashite anaweza kusimamishwa ni kuonyesha jinsi gani nafasi ya urais mnavyoidharau na hamjui msemalo

Urais ni taasisi nyeti na sio every Tom, Dick and Harry wanaweza kuutwaa. Kawaulizeni kina Malecela, Membe, Seif Sharif et al.
 
Ahaaa ahaaa, yeye aliweza kuwatabiria wenzake lakini akashindwa kutabiri kuwa atapata kura 2 za wajumbe?
Mkuu alipata kura 1 tu ya kwake! Mbwebwe zote za kura za maoni kuonyeshwa uhuru na uwazi na baadae wakaishia kuvuruga uchaguzi mkuu! watu hawa ni bure kabisa!
 
Kuna ugoro gani ambao hawajafanya mpaka sasa? Wala hili halitashangaza tena! Lengo lao hawa sio ustawi wa taifa na watu wake la hasha! Lengo ni wao kubaki kwenye madaraka tu at any cost!
 
Kwa nchi hii namna Rais ambavyo ni sheria na kila kitu hapa TZ, basi hata huo utabiri ingawa kwa wengi wataona ni "next to impossible" lakini inawezekana.

Hivi ni nani angeweza kutabiri kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, vigogo wote wa upinzani, akina Freeman Mbowe, Godbless Lema, Peter Msigwa, John Heche, Halima Mdee, Profesa Jey na Sugu, wote hao wangeanguka kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi huu?

Hata CCM wakisimamisha "Kuku" katika uchaguzi ujao, mbele ya Tume hii inayoongozwa na makada watiifu wa CCM, ni lazima CCM ishinde, tena kwa kishindo kikubwa sana.

Wapinzani wasipodai Tume huru, basi hakika kama wasemavyo wenyewe CCM kuwa chama Chao kitatawala milele na milele!
 
Uchaguzi umeisha tunawaza siasa, uchaguzi unakaribia siasa, uchaguzi unafika siasa.

NB: Siasa namaanisha siasa chafu.

Lini tutajadili kurusha rocket & satellite, kuunda vinu vya kurutubisha nuclear, kwenda mwezini na kuunda manowari?
Utawazaje kurusha rocket mkuu wakati huna uhakika wa kula
warusha rocket walishasahau matatizo madogo madogo kama tulio nayo
Huwezi kufika 10 kabla ya moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…