Pre GE2025 Pascal Mayalla amshauri Lissu kutumia jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati

Pre GE2025 Pascal Mayalla amshauri Lissu kutumia jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Pascal Mayalla mara nyingi kwenye midahalo ya kisiasa umekuwa ukijitambulisha kwamba wewe ni mwakilishi wa JamiiForums.

JamiiForums ipi unayoiwakilisha, ilihali wewe ni kada wa CCM? Je, JamiiForums, ina mrengo wowote wa kisiasa?

Kama unaenda kwenye midahalo hiyo, jitambuloshe kwa jina la taasisi yako ya PRRRR.

Iwapo ukaendelea kufanya utambulisho wa uakilishi wa JamiiForums, kuna watu watakaofanya mambo ya hovyo na kusema nao pia ni wawakilishi wa JF.

Tunaomba Maxence Melo akemee mara moja Jambo hili kwani linafanya JF ionekane ni Mali ya chama cha siasa
Tunaomba Jf huyu ndg apigwe ban ya mwaka mmoja.
 
Mwanachama mwenzetu akipata nafasi ya kutuwakilisha kwenye matukio makubwa na akipata nafasi ya kuchangia chochote ni vyema tukampongeza kwanza kwa ujasiri wa kujiweka public mbele ya kamera na watu wote hii si mara ya kwanza Paskal kujitokeza na kuuliza maswali magumu.

Haya maswali yake mara nyingi yamesababisha watu kulipukwa na moyo. Aliwahi muuliza swali JPM na ni hakika mpaka JPM anakufa hakuna mtu jasiri aliyewahi muuliza swali gumu na wengi wao walimpongeza na kumpa sifa...

Ila leo kisa kaulizwa Lissu, basi waliokuwa hawakupenda ule ushauri wa Paskali wamekuja juu zaidi ya Lissu aliyelengwa na lile swali..je ni wangapi wanaweza kujitokeza na kutaja id fake zao mbele ya kamera.....

wengi ni mahodari hapa kwenye vidole ujasiri mbele ya kamera au maandamano zero...

Muwache paskal atambe na ajinasibu na kujimwambafai na jukwaa lake pendwa mimi nimekubali kuwakilishwa....

Mnakataa udikteta kumbe baadhi yenu ni mqdokteta...paskal hongera na jf hongera kwa kutoa member smart na bright kutuwakilisha...

Paskal endelea na misumari ila mradi usivunje sheria ukaitwa kamati ya maadili kwa mara nyingine ...

Lissu ni nani asiulizwe? Tena ushauri mzuri tu apitie jukwaani kusoma hamuoni hata hayo mawazo yenu Lissu anaweza yasoma na kwenda kuyafanyia kazi!

Mnyika kafumua hoja ya kaka yangu mpaka nikaona huruma.
 
As
Naunga mkono Hoja kwa asilimia mia Moja. Paschal Mayalla amekuwa akituheshimisha sana wana Jamii Forum. Shida ya wana CHADEMA uwezo wao ni Mdogo sana kihoja. Kwa hiyo ukiwaambia hoja tofauti na uwezo wao wa kufikiri au vile walivyo karirishwa na kukariri wanaanza kupiga makelele kama walevi. Wao wanataka muda wote Taifa zima liwaze na kufikiri katika namna wanavyofikiria wao utafikiri tumekuwa manyumbu au mambumbumbu.
Ajitambulishe kama mwakilishi wa ccm sjui prrr nin sjui. syo et mwakilishi wajamii foram
 
Pascal Mayalla mzee mwenzangu umeumbuka maana wamekukataa humu kama walivyokukataa siku ile ya kura za maoni huko CCM. Huyu roho wa kukataliwa naona amekuandama baada ya kugeuka kutoka kwenye hulka yako ya kusimama na ukweli toka enzi zetu zile za KITIMOTO ambazo najua members wengi humu walikuwa hawajazaliwa au walikuwa vijana wadogo sana na hayo hayakuwa size yao.
Wengi wamependekeza upigwe ban ili liwe fundisho kwa wengine maana hii tabia kujivika uwakilishi imeanza kuota mizizi kwako, ila mie nakuomba tuu waombe radhi na uiache watakusamehe.
Unajua uzee na John Mtembezi sometimes vinavuruga.
Pia hicho chama ulicho amua kukitetea, hata mbinguni kisha kataliwa kwa matendo yake. Jiepushe nacho
 
Pascal ni mjinga baba yake alikuwa chawa wa Nyerere na mama yake pia
Hapana aisee, kwenye hili namtetea porti aiseee! Ina maana watumishi wa serikali wakati wa Nyerere walikuwa chawa? Hapana aisee wazee wa Pascal walikuwa wamesoma, shauri yako wewe kama ka baba kako wakati wenzie wanaenda shule kenyewe kanakimbizana na kayoga!
 
Back
Top Bottom