Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

Mheshimiwa punguza haraka basi andika taratibu ueleweke.
 
Habari WanaJF inaonesha huyu Pascal Mayala ni great thinker kiasi cha kushindwa kuelewa hoja zake......
PM anasema Tume ya Uchaguzi ni Huru kama ilivyo kwa Bunge na Mahakama kwa sababu vyote msingi wake ni Rais Sasa utata uko wapi hapo..?
 

Tupiganie katiba mpya mara 2? Aliyeikataa katiba mpya ni Magufuli mwenyewe maana hii mbovu anaitumia apendavyo na sio katiba itakavyo. Narudia tena, kama hujui kitu kaa kimya.
 
Ni tumehuru kwa CCM,kwa kuwa rais ni wao,hata mahakama na bunge vyote ni huru kwao,kwa kuwa vinapokea na kutekeleza maagizo ya CCM kwa uhuru,pasipo kuingiliwa na chama kingine zaidi ya CCM na serekali yake.
 
Tupiganie katiba mpya mara 2? Aliyeikataa katiba mpya ni Magufuli mwenyewe maana hii mbovu anaitumia apendavyo na sio katiba itakavyo. Narudia tena, kama hujui kitu kaa kimya.
Usijisahaulishe msingi wa hoja yetu tuliokuwa tunaijadili hapa mkuu.
Nilikwambia tume ni huru kwa mujibu wa katiba tulio nayo na nikakukumbusha nguvu ya Rais aliyopewa na katiba.

Sasa suala na Magufuli kuwa kakataa katiba mpya Kama unavyo dai wewe hilo ni jambo lingine na hata Kama yeye kakataa haimaanishi kwamba ndio tusiendelee kudai katiba mpya.
 

Mi nakataa mahakama na NEC siyo taasisi huru kwa sababu kuna mkono wa Rais kwenye teuzi. Fullstop
 

Hivi unajua unaloongea we dogo? Kuna mahali popote watu wamekaa kimya kuhusu madai ya katiba mpya?
 

Mi nakataa mahakama na NEC siyo taasisi huru kwa sababu kuna mkono wa Rais kwenye teuzi. Fullstop
 
Ni tumehuru kwa CCM,kwa kuwa rais ni wao,hata mahakama na bunge vyote ni huru kwao,kwa kuwa vinapokea na kutekeleza maagizo ya CCM kwa uhuru,pasipo kuingiliwa na chama kingine zaidi ya CCM na serekali yake.
Hiki unachosema ni sahihi 100% Ila ujue kuwa tusipopata katiba mpya hata Kama ATC/CHADEMA washike Dola bado hapatakuwa na tume huru sababu madaraka makubwa ya Rais yatakuwa pale pale na hivyo vyombo vitakuwa chini yake na si huru.
 
We nae ni zuzu tu, unakuwaje shabiki wa mtu ??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unajua unaloongea we dogo? Kuna mahali popote watu wamekaa kimya kuhusu madai ya katiba mpya?
Huwa nafurahiaga sana uwepo wa watu Kama nyinyi inapendeza Sana kwakweli ndio maana naipenda JF.
Hoja ya kuwa tume ni huru kwa mujibu wa katiba yetu umeielewa mkuu??
Unasababu yoyote ya kumsbambulia Pascal kwa alichokisema ??

Mkuu sikukwambia kuwa watu wapo kimya kuhusu kudai katiba mpya, hasha!!, bali nilikuwekea uhusiano wa KATIBA na TUME HURU (katiba tuliyo nayo inatuambia tume ni huru kitu ambacho si sahihi kwasababu katiba hii imempa madaraka Rais ya kuiweka tume chini yake.) Sasa ili tupate tume huru ya kweli nje na hii yenye uhuru wa bandia( japo ipo kisheria) katiba mpya ndio suluhisho.
 
Huyo low IQ Pascal mganga njaa ni Mwanasheria wa nchi gani? Kasajiliwa wapi kuwa Mwanasheria? Acheni kuwapa wajinga nafasi wasizokuwa nazo.
 
Huyu P. Mayalla ni mwandishi pekee kichwa aliyebaki. 100% Mahakama na bunge letu viko huru. That's why hata alipoitwa kuhojiwa na bunge Mahojiano yalikuwa wazi hata media ziliruhusiwa. Pia mahojiano yalipokisha P aliita mkutano na waandishi wa habari akawambia nini kilijili kwenye mahojiano na kamati ya bunge. Big up P. penye ukweli lazima useme.
 

Kuna tofauti ya chombo huru kIsheria na tume huru. Hata CAG na bank kuu ni chombo huru. Tume huru ni tume maalumu yenye wawakilishi mbali mbali kutoka vyama tofauti, wanaharakati na wana sheria. Lengo kubwa likiwa kuonyesha uwazi na uhakiki wa uchaguzi bila upendeleo. Hii tume sio lazima iwe idara inakuwa kama bodi ya kampuni. Hichi ndicho wanachokiomba kutokana na mienendo ya NEC.
 
Naomba kuuliza masuali yafuatayo.

1.Je, watu wanataka tume huru kwa vipi yaani iwe inajitegemea kivyake kuanzia fedha za kujiendesha mpaka bajeti yake ya kila mwaka?

2. Je, ikiwa tume huru nani anateua mkurugenzi wake na wasimamizi wa vituo vya kupiga kura?

3. Ikiwa ni tume huru itawajibika kwa nani, kwa katiba au kwa mahakama au kwa nani?

4..Je kuna mfano wa nchi yoyote duniani ambayo ina tume huru kabisa ambayo haina kamba kutoka serikalini au kwa vyombo vingine vya dola?

5. Je, naweza kupata mfano wa ni nchi ipi ambayo tume ya uchaguzi inaruhusu watu binafsi au taasisi fulani nazo zikusanye matokeo ya uchaguzi na kutangaza bila ridhaa yake?

6. Je Tume yetu ya NEC inafuata mfumo upi aana kuna mfumo wa executive ambayo ni hii ya Tanzania, independent yaani inakuwa na bajeti yake kabisa kila mwaka, sehemu ya serikali yaani branch, mchanganyiko au mixed ambapo kunakuwa na bodi inayosimamia idara maalum ambayo inashughulika na uchaguzi au chaguzi.

Au kuna judicialry yaani inasimamiwa na mahakama na mifano ya tume kama hizi ni kule Mexico, Brazil na Argentina.

Tunataka tume huru ya aina ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…