Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Ndugai alimkatalia wazi wazi kutomlipa hela za matibabu alimkatalia kwa misingi gani na wakati huo huo anaona Watanzania wanajichangisha mia mia atibiwe nani alihoji kuhusu hili...
Huo ni mhimili tofauti kabisa!
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
Lissu ndiye aliyefanyiwa unyama wakupigwa risasi mchana na watu hawajakamatwa,kibinadamu yeye ndiye anamachungu zaidi.Tuache kuchanganya siasa na utu.
 

Mtu anapopaza sauti ya msaada kwa boss Mkuu, maana yake wa chini walishamkwamisha!!!

Hapa kwenye jukwaa nimewahi kumsoma Mwanakijiji akiomba msaada wa kupata passport yake mpya,baada ya mwaka sasa kuzungushwa hapo USA.

Wote tuliona Mange Kimambi pia akipata passport baada kufanya kazi ya Mama ilihali zaidi ya mwaka hakupewa.

Kati ya hao watu wawili na ukiwaunganisha dhidi ya Lissu,yupi CCM hawampendi?!!
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Pep
 
Reactions: Pep
Duh! Kumbe alishajilipua. Lissu, alidhamilia kweli kubaki huko. Hivi, amemuonyesha Mama "lost report" ya polisi?
====
Swali lililo kwenye heading ya uzi huu lijibiwe.
 
Tundu Lissu ni msanii....utaratibu wa kupata passport kwa aliyepoteza unaeleweka.Anachokifanya ni kuficha aibu ya kula matapishi yake
 
Umeuliza Maswali ya maana kabisa, ila jiandae kwa Dhihaka na Matusi kutoka kwa Wafuasi wake ( wao ) wenye Uvivu wa Kufikiri lakini ni wepesi wa Kukurupuka.
 
Kwa nini uombe msaada wa Rais?
Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!

Wewe badoo hujaijua vizuri nchi yako. Ushajiuliza zile risasi alipigwa kuna sababu gani za msingi? Sembuse passport.

Wanataman afe kumuua ujerumani hawawezi, wameona bora waibe passport na wagome kumpa nyingine asikanyage tz.
 
Kwahiyo bila Samia kwenda Ubelgiji asingepat passport?
 

Kwenye hili Lissu kaibiwa au kapoteza kwa uzembe wake na anapaswa kuwajibika kwa uzembe wake huu!
Passport ni kama kitambulisho kinapaswa kutunzws kwa umakini mkubwa na anayepoteza hati ya kusafiria huchukuliwa kama mtu mzembe na asiyejali!
Lissu kwenye hili ameonesha udhaifu mkubwa sana kushindwa kutunza kitu muhimu kama hiki labda itaonekana sio mzembe kama ana ushahidi alivamiwa na kuibiww hiyo hati!

Pengine Sukuma gang wa ujeremani wamemuibia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ninachokiona hapo ni kuwa Tundu Lissu hakutegemea kama mama atakutana nae, alipoomba kukutana nae alikuwa katupa turufu na alishakuwa na jibu la kukataliwa kuonana nae kwa 100%, ili apayuke kisiasa. Mama kamziba mdomo na akawa hana la kusema hajui amwambie nini, akaanza kubwabwaja.
 
Inaweza kuwa kweli passport yake imeibiwa au imepotea, Hilo analijua yeye. Lakini kitendo Cha kukaa kimya bila kutoa taarifa Hadi alipokutana na Rais na kumuomba msaada amsaidie hakijakaa vizuri.

Vinginevyo angesema amepata vipingamizi Gani na akiba nani wanamkwamisha kupata passport yake.
 

Hao labda ni Sukuma gang wa ujeremani
 

Mwezi mchanga taratibu Bibie wa Mtaa Kipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…