Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Kwani mkuu wewe ni mgeni na Lissu aliamua kujilipua lakini ghafla ujio wa mama kabadili mawazo!
 
Afrika kuna ukiritimba.

Miguna Miguna alikua deported kwa madai ameishi Kenya kama raia wa Canada.

Inawezekanaje mtu aliyezaliwa Kenya na kuishi uhamishoni miongo miwili kwa kukimbia utawala dhalimu unasema sio raia?

Miguna alipoenda tofauti nao wakatumia loophole sasa kumfanyia deportation kwa madai ameukana uraia wa Kenya hivyo afanye kuomba upya.

Katiba mpya ya Kenya ya 2010 inaruhusu uraia pacha sasa kwanini hawamruhusu?

Katika majaribio yake 2 ya kurudi yamegonga mwamba kuanzia 2018 mpaka 2021, na mahakama zimeruhusu aingie ila serikali inakataa hii ndio Afrika na anaambiwa akiingia ataingia kwa tourist visa.

Kuomba hati ya kusafiria mpya inapopotea ya zamani inajulikaka , Lissu na Miguna Miguna ni wanasheria na raia halali wa mataifa yao na hatua hizo wanazifahamu ila watanyimwa tu mwisho wa siku

Tatizo kubwa wamawekewa ngumu sababu ni wakosoaji wakubwa na wa wazi kwa serikali na Africa taasisi zinanyenyekea serikali sio kufuata sheria.
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Kwani Ukiwa ULAYA HUIBIWI? Vitu vingine haviitaji kutumia Akili kubwa tumia hata Akili ya kuku
 
Ninachokiona hapo ni kuwa Tudu Lissu akutegemea kama mama atakutana nae, alipoomba kukutana nae alikuwa katupa turufu na alishakuwa na jibu la kukataliwa kuonana nae kwa 100%, ili apayuke kisiasa. Mama kamziba mdomo na akawa hana la kusema hajui amwambie nini, akaanza kubwabwaja.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Wew umekuwa mgeni na nchi mpaka unashangaa kumtumia rais ili aipate passport yake?
Au unadhani yupo kule kwa kupenda kwake?
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Lissu anafahamu taratibu zote na lazima ameshazifuata.

Picha ninayoipata hapa ni kwamba anapata usumbufu mahali either ubalozini au popote pale na ndio maana katumia nafasi hii kumwambia mwenye Mamlaka.

Hata Mange Kimambi alisumbuliwa sana kupata passport kwa miaka kadhaa mpaka akatumia nafasi ya kumuomba Rais Samia kupitia Wasaidizi wake ndio akatoa amri apewe passport.
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
Upo sahihi kabisa alichokifanya kundu ni mambo ya kitoto kweli kweli.
 
Ninachokiona hapo ni kuwa Tudu Lissu hakutegemea kama mama atakutana nae, alipoomba kukutana nae alikuwa katupa turufu na alishakuwa na jibu la kukataliwa kuonana nae kwa 100%, ili apayuke kisiasa. Mama kamziba mdomo na akawa hana la kusema hajui amwambie nini, akaanza kubwabwaja.
Ndo akamwomba na passport? 🤣🤣🤣
 
Lissu anafahamu taratibu zote na lazima ameshazifuata..
Picha ninayoipata hapa ni kwamba anapata usumbufu mahali either ubalozini au popote pale na ndio maana katumia nafasi hii kumwambia mwenye Mamlaka..
Hata Mange Kimambi alisumbuliwa sana kupata passport kwa miaka kadhaa mpaka akatumia nafasi ya kumuomba Rais Samia kupitia Wasaidizi wake ndio akatoa amri apewe passport.
Hivi ulikuwa na fununu ya kupotea paspoti kutoka 'space' yoyote ya wana'space' kabla ya jana?
 
Sasa afanye nini zaidi, hiyo turufu nyingine ili aulizwe kama ulivyouliza wewe, aanze kubwabwaja "tunaonewa" "hakuna chaguzi huru" "tunanyimwa passport tusirudi". Ni chambo tu cha kijinga kakiweka.

Aiseeeeee
 
Tuache siasa, hujui hata alisema atarudi lini. Waacheni wapinzani wahoji serikali, ambako kuhoji kwake waita kuropoka, uliyepo madaraka uwe waleta majibu sahihi.
We hukuona tweet yake akisema anarejea nyumbani, humu ndani vichaa wakapigiza kelele kuwa Lissu anarudi atamhenyesha Rais?? Tukawaambia hamjua nguvu ya Rais, leo kiko wapi?? Maombi ya Lissu na Zitto yana utofauti gani? Nyie ni vichaa
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.
Good point
 
Back
Top Bottom