Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Taratibu za kupata passport mpya kama uliyokuwa nayo imepotea, zipo wazi.

Kwa nini uombe msaada wa Rais?

Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!
Namba zake huna umuulize?
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Alikumbuka ya Kashogi passport ilikuwa chanzo cha mwisho wake.. so yupo sawa kumueleza Rais ili wasije mla kichwa
 
Mb
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
O
Tundu Anthipas Lissu ni mwanasheria na msomi. Sina wasiwasi kuwa alishafuatilia taratibu zote, lakini mamlaka zinazohusika haziwezi kufanyia kazi maombi yake kwa hofu iliyojengwa na watawala hasa utawala uliopita wa ile awamu ya giza.

Waliomwibia Lissu passport yawezekana walitumwa kumdhuru na/au kumwibia nyaraka mbalimbali anazofanyia kazi. Nina imani kuwa hizo nyaraka na passport zipo Tanzania zimekaa tu mezani kwa mtu.

Kwa mazingira hayo, ilifaa Lissu apeleke ombi lake kwa Rais ambaye anaweza kutoa tamko tu na wahusika wakaondoa hayo mambo machafu yanayoendelea kuiweka Tanzania katika zama za ujinga na giza.
Hivi Lissu ni chama gani? Ukimsikiliza vizuri alivyo kuwa anaelezea mazungumzo yake na Rais Samia, utafikiri yeye ni CCM! Mara alipo anza kuzungumzia issue ya Mheshimiwa Mbowe, utafikiri ni ACT WAZALENDO! Sikusikia alipojieleza kama mkamanda! Anawadanganya CHADEMA - inaonekana kama zile point zake 6 kaandikiwa na Ndugai!
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.
Wasiojulikana ndo walio mwibia ,Yani mh Lissu amepitia Mengi,ila amejua kuinyosha serikali za CCM, namanisha from Mkapa,kikwete,mwendazake, SSH japo alikua ajamjua vizuri labda na kupata history yake tangu tawala tajwa hapo juu,
Lissu penye kujenga hanaga shida, ila pale unapotaka kuvunja haki za watu,ndo utamjua vizuri
 
Afrika kuna ukiritimba.

Miguna Miguna alikua deported kwa madai ameishi Kenya kama raia wa Canada.

Inawezekanaje mtu aliyezaliwa Kenya na kuishi uhamishoni miongo miwili kwa kukimbia utawala dhalimu unasema sio raia?

Miguna alipoenda tofauti nao wakatumia loophole sasa kumfanyia deportation kwa madai ameukana uraia wa Kenya hivyo afanye kuomba upya.

Katiba mpya ya Kenya ya 2010 inaruhusu uraia pacha sasa kwanini hawamruhusu?

Katika majaribio yake 2 ya kurudi yamegonga mwamba kuanzia 2018 mpaka 2021, na mahakama zimeruhusu aingie ila serikali inakataa hii ndio Afrika na anaambiwa akiingia ataingia kwa tourist visa.

Kuomba hati ya kusafiria mpya inapopotea ya zamani inajulikaka , Lissu na Miguna Miguna ni wanasheria na raia halali wa mataifa yao na hatua hizo wan

Tatizo kubwa wamawekewa ngumu sababu ni wakosoaji wakubwa na wa wazi kwa serikali na Africa taasisi zinanyenyekea serikali sio kufuata sheria.
Hayo yote yalitokea Kenya ambayo ni mfano bora wa democrasia kwa mujibu wa chadema?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Taratibu za kupata passport mpya kama uliyokuwa nayo imepotea, zipo wazi.

Kwa nini uombe msaada wa Rais?

Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!
Acha ujinga wewe! Hujui katika mazingira aliyonayo na uoga wa maafisa wa serikali hizo taratibu za kupata passport mpya zaweza kuwa ngumu?
Unatambua hata hiyo aliyoibiwa aliipataje kama sio kwa msaada wa Ubalozi wa Germany baada ya uchafuzi mkuu 2020 na akaondoka kwa msaada wao?
Lissu anajua kuzicheza vyema hesabu zake
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
Kwamba usalama wake sio jambo la msingi! hii nchi imebeba mapumbaavu yaliyoshindikana nyie ndio wanufaika wa migogolo na safari hii mtakuuuunya povu!!
 
Kama mtu kaibiwa begi lenye vitu vyake ikiwepo wallet yenye passport anapaswa kutumia lugha gani kuwasilisha??

Wenzako wanabeba box begani wewe unabeba box utosini ndiyo maana akili zimegadamizwa.
Lisu angeibiwa hivyo huko twitter kusingekalika kwa mijadala lukuki toka kwa wana space

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
Wewe nawe upo tu , kwamba katika hoja zake 6 alizowasilisha sio za msingi? Zile hoja 6 mkianza kujadili, utachukua mwaka,

Tatizo CCM kwenu Mambo ya msingi kwenu ni kusifia tu na kujipendekeza pata teuzi ,taifa badae tumbo kwanza
 
Back
Top Bottom