Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Hujui pickpocteting ipo hata huko nchi za magharibi?

Pia, pickpocteting sio kwa ajili ya manufaa ya kupata pesa au mali tu, bali ni njia mojawapo ya kukusanya taarifa!
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Mkuu Nyani Ngabu umeuliza maswali ya msingi sana.

Naamini kama Tundu Lissu angekuwa amekutana na Rais mwingine kama Magufuli au Waziri Kabudi au Lukuvi asingethubutu kutamka hayo. Maana majibu yangemchefua.

Hii ni dalili kuwa Mama anaponya Taifa mpaka waliomuita Dikteta mwanamke wanampelekea personal problems awatatulie.

Hongera Rais SSH
 
Umeuliza Maswali ya maana kabisa, ila jiandae kwa Dhihaka na Matusi kutoka kwa Wafuasi wake ( wao ) wenye Uvivu wa Kufikiri lakini ni wepesi wa Kukurupuka.
Swali la aliyeiba ni nani, hata mhusika hawezi jua. Imagine umepanda mwendokasi na kuibiwa simu...unaweza kujua aliyeiba ni nani?

Kwa nini amuombe Rais, je una hakika kama mamlaka husika hazijamuwekea vizingiti? Kumbuka kuna baadhi wanamuona msaliti tangu awamu ya tano...je ni rahisi watu hawa kutoa hati ya kusafiria kwa msaliti?
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Unavyobwata sasa utafikiri mtu kuibiwa ni kitu kigeni.
 
Kupoteza ni bahati mbaya always,

Hii inaonesha walio nje wengine wanapata shida kupata even ku renew their passports, hata yule dada mange alifanikiwa kupata / renew yake alipoenda kule.

Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa.
 
Unajuaje kama hakutoa taarifa

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app

Si ndio maana hii thread imeanzishwa?
Hayo mambo yote inabidi yajulikane..unakumbuka yule mama alienda Kwa Rais na madai yake akaambiwa akae na kutulia jambo lake litashughulikiwa?

Lengo ni kama Kuna watu wamekwamisha mchakato wa upatikanaji wa gari na wenyewe wawajibishwe. Isiishie TU upatikanaji wa hati.

Lakini pia kama tayari alishatoa taarifa na jambo lake linashughulikiwa, hakukua na sababu ya kuliibua Kwa Rais, ni jambo dog sana kumpelekea Rais kama halina konakona ambazo ndio tungependa kujua ni zipi?
 
bila kufanya hivyo, balozi yoyote ambaye angejaribu kumpa passport Lissu angefunguliwa kesi ya uhaini + uhujumu uchumi…….
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Mpigie atakueleza mwenyewe
 
Kwenye hili Lissu kaibiwa au kapoteza kwa uzembe wake na anapaswa kuwajibika kwa uzembe wake huu!
Passport ni kama kitambulisho kinapaswa kutunzws kwa umakini mkubwa na anayepoteza hati ya kusafiria huchukuliwa kama mtu mzembe na asiyejali!
Lissu kwenye hili ameonesha udhaifu mkubwa sana kushindwa kutunza kitu muhimu kama hiki labda itaonekana sio mzembe kama ana ushahidi alivamiwa na kuibiww hiyo hati!

Pengine Sukuma gang wa ujeremani wamemuibia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kama hujawahi kukutana na hiyo hali ya kupoteza/kuibiwa huwezi kujua. Hata kama una chuki na huyo Bwana, bora ungekaa kimya.

Tukifuatilia maisha yako umepoteza simu mara nyingi tu ntingine kwa uzembe (gross negligence)nyingine kwa kutokujua. Lakini hakuna aliyekusimanga kama hivi. Usimfanyie mwenzio kile usichopenda kufanyiwa (golden rule)
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.

Atakuwa alifanyiwa figisu kwenye njia ya kawaida ndio maana kaamua kumwambia rais.. mbona rahisi tu kuelewa..
 
Kama hujawahi kukutana na hiyo hali ya kupoteza/kuibiwa huwezi kujua. Hata kama una chuki na huyo Bwana, bora ungekaa kimya.

Tukifuatilia maisha yako umepoteza simu mara nyingi tu ntingine kwa uzembe (gross negligence)nyingine kwa kutokujua. Lakini hakuna aliyekusimanga kama hivi. Usimfanyie mwenzio kile usichopenda kufanyiwa (golden rule)
Watanzania watu wa ajabu sana wanashangaa kupotea passport 😁😁😁
 
Tundu Anthipas Lissu ni mwanasheria na msomi. Sina wasiwasi kuwa alishafuatilia taratibu zote, lakini mamlaka zinazohusika haziwezi kufanyia kazi maombi yake kwa hofu iliyojengwa na watawala hasa utawala uliopita wa ile awamu ya giza.

Waliomwibia Lissu passport yawezekana walitumwa kumdhuru na/au kumwibia nyaraka mbalimbali anazofanyia kazi. Nina imani kuwa hizo nyaraka na passport zipo Tanzania zimekaa tu mezani kwa mtu.

Kwa mazingira hayo, ilifaa Lissu apeleke ombi lake kwa Rais ambaye anaweza kutoa tamko tu na wahusika wakaondoa hayo mambo machafu yanayoendelea kuiweka Tanzania katika zama za ujinga na giza.
Sijui Mataga na CHAWA Kama watakuelewa.
 
Nani sasa anayemkatalia na anamkatalia kwa misingi gani?
Kwanini alipigwa risasi, kwanini alifukuzwa bungeni, kwanini alinyimwa mafao yake, kwanini alimyimwa matibabu.. ukiyajibu hayo utakuwa umepata jibu la swali lako...
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.
Na kwa mtu ambaye hana connection na amepoteza pasport utaratibu ukoje?
Je wanaopoteza pasport wote huwa wanaenda kumuomba raisi awasaidie kuzipata au ya kwake ni special?
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Huku kunaitwa kutafutiana sababu......mama asipolitekeleza iwe ooh! ooooooh!
 
Back
Top Bottom