Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Maisha yanaenda kasi kweli kwahiyo kwa SasaTundu ni shwahiba wa Suluhu.
 
Inaweza kuwa kweli passport yake imeibiwa au imepotea, Hilo analijua yeye. Lakini kitendo Cha kukaa kimya bila kutoa taarifa Hadi alipokutana na Rais na kumuomba msaada amsaidie hakijakaa vizuri.

Vinginevyo angesema amepata vipingamizi Gani na akiba nani wanamkwamisha kupata passport yake.
Watu wajuajiaji unauhakika kuwa Lissu wajawahi toa taarifa kwenye mamlaka husika, he is not stupid as you think ndugu

Leagal documents inapopotea hatua ya kwanza ni kitoa taarifa polisi na taasisi husika, anajua madhara iliwa pass hiyo itaingia mkononi mwa watu wabaya.
 
Mpaka Rais anakubali kuwa atalifanyia kazi swala la passport ni wazi amepewa details za kutosha za nini hasa kimemkwamisha kupata passport.

Rais siyo mjinga asingepewa maelezo ya kutosha angemwambia aende aifuate sehemu husika.

Lissu na Samia wameongea zaidi ya saa Moja, clip ya summary Kwa umma ni dk 7, hivyo Kuna details na mengine mengi wameongea hatujaambiwa, tumepewa summary tu ya kilichozungumzwa.
 
Unapojadili jambo linalomhusu Lisu lazima uangalie siasa za Tanzania tangu 2015 hadi leo. Unahitaji kuangalia utendaji wa vyombo vya dola, taasisi za serikali, tabia za wateuliwa,fikra zao, matendo yao dhidi ya viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.
Hata humu humu kwenye mjadala huu mawazo hayo hayo ya kibaguzi kwa ukaburu wa kivyama yanajitokeza.
Rais Samia amevunja fikra hizo za kikaburu, Lisu ametumia nafasi hiyo kujieleza na kutoa changamoto anazokumbana nazo ikiwemo hiyo ya passport.
 
Mie nahisi kaipoteza passport makusudi ili aendelee kuhifadhiwa huko ubelgiji apate kisingizio, au kwa kuwa alishaahidi atarudi mwezi march tz na aliongea kisiasa bila dhamira yake kumtuma hivyo akaona aje na style ya kupoteza passport, kupoteza passport kwa mtu maarufu kama TL na isipatikane nadhani ni vigumu sana
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie

Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Kazi ya wale vijana wakijani ili asirudi nyumbani. 🤔
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.

hata mimi miaka ya nyuma kabisa nilipokuwa nchi moja kule ulaya ilikuwa kazi kubadilisha passport , mpaka nilipokutana na balozi mwenyewe mahali nje ya ubalozi nilipomweleza ndio nilipokwenda ubalozini nikafanyiwa passport kwa haraka.
 
Taratibu za kupata passport mpya kama uliyokuwa nayo imepotea, zipo wazi.

Kwa nini uombe msaada wa Rais?

Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!
Mbona unaonekana ni mwelewa na una exposure kubwa tu.sasa wewe usichoelewa ni nini.inawezekana kaibiwa na watu wasiotaka arejee nchini kaenda ubalozi kanyimwa.pia ki protocol passport ni ID ya mtanzania ukiwa nje kwahiyo kama huna passport ya Tanzania wewe sio Mtanzania inaonekana umejilipua.kwahiyo kama ingekuwa mama anaonana na jumuiya ya diaspora wa kitanzania huko Brussels Lissu asingeruhusiwa kwenye huo mkutano.Busara imetumika yeye kukutana na Prezidaa.
 
Back
Top Bottom