Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Kuibiwa passports kwenye hizo trains za Europe kitu cha kawaida sana. Kuna Waturuki wengi tu wanaiba bags hasa za laptop na ukiweka passport humo inakwenda.

Sasa Lissu kaenda kuomba passport mpya na wanamzungusha tu. kumbuka huyo Sokoine alipoteza cheo kwa kwenda kumuona Lissu hospitali .
Lissu kasema ameomba passport mpya na wamemzungusha?

Halafu, kama ulichodai ni kweli, kwa nini haya yanatokea chini ya Samia?
 
Mwendazake aliamrisha awindwe auliwe. Mtu anayepaswa kuuliwa kama ngedere anaweza kupewa passport?

Jaribu kutumia akili zako vizuri utaelewa.
Hiyo aliyokuwa nayo ambayo imepotea, aliipataje?

Alipewa? Aliiokota? Alijitengenezea mwenyewe?
 
Lisu angeibiwa hivyo huko twitter kusingekalika kwa mijadala lukuki toka kwa wana space

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo unadhani Rais hawezi kuwa na ufahamu kwa jambo kama hilo? Anao watu wakuweza kumpa ukweli ndani ya serikali.
Chama chenu pekee ndicho chenye washauri hopeless lakini serikalini wapo wenye weledi na ndio hao wamemshauri atenge muda mchache wa ziara yake kuongea na Lissu
 
Huu Uzi umenifanya niwafahamu watu upeo wa akili zao,nilidhani wana akili ni ma great thinker kumbe hata Ku reason kitu kidogo hiki wameshindwa![emoji848][emoji848]
Kwanini madame?
 
Unyamaze kuhoji vitu ambavyo huwezi kuvielezea unapoulizwa, huna utofauti na mashahdi wa michongo kazi kujikojolea wanapoulizwa na kujifanya wagonjwa.
Nafanya chochote kile ninachotaka kufanya na huwezi kunifanya kitu!
 
Tundu Anthipas Lissu ni mwanasheria na msomi. Sina wasiwasi kuwa alishafuatilia taratibu zote, lakini mamlaka zinazohusika haziwezi kufanyia kazi maombi yake kwa hofu iliyojengwa na watawala hasa utawala uliopita wa ile awamu ya giza.

Waliomwibia Lissu passport yawezekana walitumwa kumdhuru na/au kumwibia nyaraka mbalimbali anazofanyia kazi. Nina imani kuwa hizo nyaraka na passport zipo Tanzania zimekaa tu mezani kwa mtu.

Kwa mazingira hayo, ilifaa Lissu apeleke ombi lake kwa Rais ambaye anaweza kutoa tamko tu na wahusika wakaondoa hayo mambo machafu yanayoendelea kuiweka Tanzania katika zama za ujinga na giza.
Naunga mkono hoja, dhumuni lilikuwa ni kudhibiti safari zake
 
Siasa za Africa wapo watu wanazuia wengine kupata haki yao Rais ndio mwenye maamuzi juu ya vikwazo hivyo...

Haya masuala hayako Africa tu ni Global mzee baba. Tena afadhali huku Africa, lakin kwa mtu aina ya TAL (uzalendo ulipungua, kutaka Tanzania kushitakiwa Na kuzuiliwa ama kushikiliwa kwa mali za Taifa nyakati za Makinikia Na Acacia)ingekuwa ni kwa baadhi ya nchi kama za magharibi pengine asingekuwepo Duniani akipumua au kupata nafasi ya kuzungumza Na Mh Rais kama aliyoipata. Ni agharabu sana.
 
Nafanya chochote kile ninachotaka kufanya na huwezi kunifanya kitu!
Ninaouwezo na sema SUU hapo ulipo uangalie nitakachokufanya unaona tumo humu kwa bahati mbaya tu kwasbaabu tunaandika jumbe. Ila uache upuuzi wako nitakachkufnya usijekujakulia humu.
 
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
Hajamuomba Rais amsaidie, amesema amehakikishiwa kuwa atapata hati ya kusafiria... hajasema ataipata kwa namna ipi
 
Inaelekea watu bado wanafanya kazi kama awamu iliyopita...zama zile kutoa passport kwa mtu kama Tundu Lissu ni kujitafutia kutumbuliwa tu....taratitu zinaaply kwa wananchi wa kawaida tu...
 
Duh! Kumbe alishajilipua. Lissu, alidhamilia kweli kubaki huko. Hivi, amemuonyesha Mama "lost report" ya polisi?
====
Swali lililo kwenye heading ya uzi huu lijibiwe.
Hujui hata maana ya kujilipua?

Unajilipua kama nchi unayoenda hawajui kiukweli unatoka wapi. Kwa mfano Mtanzania anajilipua na kuwa mkimbizi wa Rwanda.
Suala la Lissu linajulikana Kwahiyo hana haja ya kutupa passport yake ya Tanzania. Wanaompa ukimbizi wanajua yeye ni mtanzania na ana passport ya Tanzania
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.
Maandishi yanayojibu hoja na zaidi.
Mjadala huu sasa ufungwe rasmi maana majibu yote yapo hapa kwenye maandishsi haya ya ndugu tutafikatu .
Kongole kwako tutafikatu .
 
Ninachokiona hapo ni kuwa Tudu Lissu hakutegemea kama mama atakutana nae, alipoomba kukutana nae alikuwa katupa turufu na alishakuwa na jibu la kukataliwa kuonana nae kwa 100%, ili apayuke kisiasa. Mama kamziba mdomo na akawa hana la kusema hajui amwambie nini, akaanza kubwabwaja.
Naona mna hasira kwelikweli,,
 
Back
Top Bottom