Pata milioni 15 kwa mwezi kwa biashara ya bodaboda

Pata milioni 15 kwa mwezi kwa biashara ya bodaboda

Halafu hiyo elfu 10 kwa siku Ni mkataba ambao akimaliza piki piki inakuwa sio yako Tena Kama Ni Hamsini zote wakimaliza mkataba unabaki na piki piki sifuri unabaki na hela.
NI Sawa Tu kwani we umeingiza ngap
Kima cha Chini boda kukuletea NI elfu 10
Wengine wanaenda mpaka elfu 15
 
Kazi ya boda boda na bajaji ukitaka usiumize kichwa sana,japo changamoto zipo toa kwa mkataba,utakuwa na kazi ya kupokea hela na kuweka rekodi na kukimbizana na wavivu wanaochelewa kuleta hela,Kuna jamaa Ana maisha mazuri kupitia mikataba ya boda na bajaji...kwa Sasa anaweza kuwa na boda 100 na bajaji Kama 50...kila siku anakusanya pesa.
Ndio nachofanya
Mkataba na referee 3
 
Biashara ya bodaboda ilimfilisi GENTAMYCINE alikopa bodaboda mbili kwa mshahara wake wa ualimu zote zikapiga mzinga bunda mjini na hakuwa na insurance ya kueleweka
Hela ya bodaboda amekosa na benki kila mwezi WANAMKATA GENTAMYCINE


Biashara yoyote ni nzuri ukiwa anasimuliwa.
Akajipange tena
 
Wewe tangu umenunua gari umeweka pembeni pesa ngapi za ajali na traffic??
Kwanini ununue kitu uanze kuwaza mabaya mbeleni??
Madereva wa Boda Boda wengi wao awana akili ! So lazima njiani wasababishe ajali kwa wengine na wao pia hili haliepukiki
 
Madereva wa Boda Boda wengi wao awana akili ! So lazima njiani wasababishe ajali kwa wengine na wao pia hili haliepukiki
Asilimia nyingi Kwa sasa waendesha bodaboda wanajielewa
Kuna watu wazima wanaendesha bodaboda hawajui ajali NI nini
 
Hao watu wazima kuleta rejesho ni shughuli nyingine maana unakuta wanamajukumu makubwa
Mwulize bodaboda yeyote Kwa siku wanapata zaidi ya elfu 50
Sasa akuibie 10 ya nuni
 
Kuna mpumbavu hapa nchi jirani alishauriwa na wakwe zake aache kazi aliyokuwa anafanya kwenye shirika la umeme na kuchukua pesa zake zote ili afanye biashara kwasababu ajira ni utumwa. Baada ya kuacha hao wakwe zake ambao ni matajiri wa biashara ya daladala na mabasi wakamuuzia coaster mbovu. Mshkaji kwa sasa ni kama mtu aliyechanganyikiwa. Ana coaster mbili zote spana mkononi. Yaani anajuta kupokea ushauri wa wakwe zake.
 
Minimum unaletewa elfu 10
Unaweza ukaagizi elfu 15 Kwa siku vile vile
Jaman boda msinunue bongo agizeni ipitie zenji
Acha kuingiza watu chaka Penny, ukinunua boda ni vile unataka kumsaidia mtu na wewe upate kidogo ya chakula home.
 
Money Penny miaka kama 10 nyuma nilikuwa naishi nje ya Tanzania nilipokuja Tanzania, vijana wa kijijini kwetu wakanishikilia nifanye nao biashara ya bodaboda. Nikaenda Kariakoo nikaulizia bei, nikaona ubwete na yule mwenye duka akanambia ukilipia 30% zingine utalipa kidogo kidogo kama unachukuwa kuanzia 10.


Nikaona isiwe tabu, nikalipia 50% nikamwambia watakuja vijana kuchaguwa rangi na options wanazotaka. Nikanunuwa.

Wiki tatu za kwanza mambo yameenda vizuri kabisa. Nikaona hii ndiyo biashara, wiki ya nne, wawili hawakuleta pesa, mara mmoja ananipigia simu ananambia katekwa na majambazi, boda imekwenda, namuuliza, umeenda polisi? ananambia bado. Nikamwambia nenda polisi, hakwenda, nikaenda mwenyewe, kijana katoroka, kwao hayupo. Polisi akanambia huyo mjinga tunampata, wakaingia kazini siku mbili tu, boda ikapatikana na kijana akapatikana.

Polisi wakanambia hii kazi wazimu, nikasimamisha zile mbili ambazo hawajaleta pesa na ile ya tatu iliyorudi.

Nyingine zote nikamkabidhi mtu azisimamie. nilichoambulia ni kurudisha pesa za mtaji tu. Tena kwa kuwa huyo mtu niliyemwachia ni "mwaminifu". Nilipoona pesa zimerudi, nikampa yeye mbili, nikawacha nyumbani kijijini pale mbili, zingine nikawa naziuza kidogo kidogo mpaka zikaisha. Zile mbili zangu mpaka leo zipo, zinafanya kazi ndogo ndogo za pale pale nyumbani tu.

Kwa ufupi, hiyo ni biashara nzuri lakini inataka usimamizi wa karibu sana, saa zote 24/7.


Kama mtu hawezi kuzisimamia kwa ukaribu namshauri afanye biashara zingine.
 
Asilimia nyingi Kwa sasa waendesha bodaboda wanajielewa
Kuna watu wazima wanaendesha bodaboda hawajui ajali NI nini
Akili za Boda boda wote ni kama madereva wa daladala ,matatu au Taxi kule South Africa awe kijana au mzee
 

Attachments

  • IMG_7831.MOV
    1.3 MB
Back
Top Bottom