Money Penny miaka kama 10 nyuma nilikuwa naishi nje ya Tanzania nilipokuja Tanzania, vijana wa kijijini kwetu wakanishikilia nifanye nao biashara ya bodaboda. Nikaenda Kariakoo nikaulizia bei, nikaona ubwete na yule mwenye duka akanambia ukilipia 30% zingine utalipa kidogo kidogo kama unachukuwa kuanzia 10.
Nikaona isiwe tabu, nikalipia 50% nikamwambia watakuja vijana kuchaguwa rangi na options wanazotaka. Nikanunuwa.
Wiki tatu za kwanza mambo yameenda vizuri kabisa. Nikaona hii ndiyo biashara, wiki ya nne, wawili hawakuleta pesa, mara mmoja ananipigia simu ananambia katekwa na majambazi, boda imekwenda, namuuliza, umeenda polisi? ananambia bado. Nikamwambia nenda polisi, hakwenda, nikaenda mwenyewe, kijana katoroka, kwao hayupo. Polisi akanambia huyo mjinga tunampata, wakaingia kazini siku mbili tu, boda ikapatikana na kijana akapatikana.
Polisi wakanambia hii kazi wazimu, nikasimamisha zile mbili ambazo hawajaleta pesa na ile ya tatu iliyorudi.
Nyingine zote nikamkabidhi mtu azisimamie. nilichoambulia ni kurudisha pesa za mtaji tu. Tena kwa kuwa huyo mtu niliyemwachia ni "mwaminifu". Nilipoona pesa zimerudi, nikampa yeye mbili, nikawacha nyumbani kijijini pale mbili, zingine nikawa naziuza kidogo kidogo mpaka zikaisha. Zile mbili zangu mpaka leo zipo, zinafanya kazi ndogo ndogo za pale pale nyumbani tu.
Kwa ufupi, hiyo ni biashara nzuri lakini inataka usimamizi wa karibu sana, saa zote 24/7.
Kama mtu hawezi kuzisimamia kwa ukaribu namshauri afanye biashara zingine.