Patrick Mfugale katika umri wa miaka 71 alikuwa anafanya nini ofisi ya umma?

Patrick Mfugale katika umri wa miaka 71 alikuwa anafanya nini ofisi ya umma?

Peleka jukwaa la kimataifa...

hivi huko Marekani hakuna ma forum mengine mukamjadili Dr. Fauci na Wamarekani wenzenu ??????

mods ondoa huu uchafuzi wa mada hapa tafadhali...
Relax dada angu. Elewa kwanza mada na ujue Fauci amehusishwaje hapo.

Usikurupikie kila kitu mtoto mzuri kabla ya kuelewa mama angu utakuja kupigwa miti bila kujielewa.
 
Kwani hawawezi kumtumia kama consultant, yaani unavuka miaka 60 bado unakalia ofisi ya umma kama Chief Executive....huo ndo uroho wa madaraka tunaosema, watu wa design hii unaweza kuta wanatumia hadi ndumba....
Pengine alikuwa Consultant kwenye nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu.

Huko nyuma TANROADS ilishakuwa na watendaji wakuu maconsultant kutoka nje.
 
Kwa hiyo hatutakiwi kujadili watu... okay

na walio hai nao tusiwajadili ? Viongozi, ma Rais, mawaziri, ni sawa kuwajadili au pia ni kipoteza muda ?
Great minds discuss ideas. Small minds discuss people. Endelea kujadili watu.
 
Wamemuacha babu wa watu mpaka kashfa ya ripoti ya Kichere imemuua, alipohojiwa presha ikapanda. Ila Kichere nae kaitoa kama ilivyo Tanroad wamelipa mikataba mara mbilimbili January to March 2021.
Kama kuna ukweli flani vile
 
Great minds discuss ideas. Small minds discuss people. Endelea kujadili watu.
Tusijadili mtu aliyekula mshahara wa umma maisha yake yote kweli acha hizo mkuu,huwezi kuzuia kiongozi wa umma kujadiliwa
 
Umri sahihi wa kustaafu utumushi wa umma ni miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima, japo kanuni zinaruhusu kuendelea kutumikia umma kwa mkataba wa miaka miwili miwili, Mfugale hajawahi kustaafu na amekuwa akiongezewa mikataba juu kwa juu.

Madhara yake mnabana nafasi za ajira kwa wengine.

RIP Mfugale 1950-2021
Whaaaaat. Huhuhuhuhuhuuuuu. Dahhhhhhhh. Kweli ilikuwa ni conduit ya kupigia pesa. Hii inabidi iingie Giness Book.
 
Kuna wakati nilipomuona akiwa kazini anakagua mabarabara nilimuonea huruma kwa hali yake ya kiafya, nilijiuliza kwanini hapumzishwi au kwanini yeye haombi kupumzika? Maskini! hadi amefia kazini.

Hili ni fundisho pia kwa watumishi wengine wenye umri mkubwa au wana matatizo ya kiafya ni vyema wakaomba kustaafu kwa hiyari ili wapate muda wa kupumzisha miili yao kuliko kuifia kazini.

Kumbukeni kazi na afya, Afya yako/uhai wako ni muhimu sana kuliko kazi, ukifa leo kesho tunateua mwengine anashika nafasi yako.
wazee mnaotaka kuifia kazini pumzikeni, pisheni vijana nao wapige kazi.
Mbele ya JPM ungeanzia wapi.Ujui tu
 
Back
Top Bottom