TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Alianza Eng wa Songoro marine amefuata Eng Mfugale! Watu wa miradi mikubwa wa Jiwe wanaondoka kwa staili moja!
 
Masimango unayasoma wapi mkuu? Unaweza nionyesha masimango hayo tafadhali? Kufa ni jambo la kawaida na kila mtu atakufa kwa wakati wake:

Au hupendi tuandike lolote ila wewe?

Hudhani labda ungejifunza walau jinsi ya ku deal na stress zako hasa unapoona maoni ya watu ambayo aghalabu ni haki yao?

Sasa kama unayajua yote haya,hayo maneno makali yanakutoka ya nini? Nikidhani wewe ni Immortal ndiyo maana unaongea kwa lugha ya majigambo kwa Marehemu
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
rest easy engineer
 
Nyerere hakupenda majina yake kutumika akiwa hai alisema ni uchuro.

Magufuli - Stendi, Daraja; Mfugale - tower, flyover; Kijazi - Daraja, Flyover.

Maneno ya Nyerere yanaweza kuwa na hoja.

Pale Dodoma napo pana soko nashauri jina kubadilishwa haraka.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Unasema ukweli
 
Namtafuta Mzee Mfugale kwenye hotuba za awamu ya sita simsikii, namtafuta kwenye vyombo vya habari simsikii tofauti na awamu iliyopita.

Je, amepotea na taaaluma yake yakudesign madaraja?
Nonsense,
 
Poleni kwa Msiba Mke na Watoto kwa Kumpoteza Mume na Baba yenu.

Pole nyingi kwa Familia kubwa ya Tanroads Nchi nzima kwa kumpoteza Mhandisi Mwandamizi na Wahandisi wote kwa Ujumla kwa msiba huu mzito.

Nchi imempoteza mtaalamu mbobezi kwenye nyaja ya Madaraja na Ujenzi kwa Ujumla.

Natumai kulikuwa na urithishaji wa taaluma yake kwa Vijana (Junior Engineers hapo Tanroads) kupitia yeye, whom they can fill the void that will be left by his absence.

Enda uwape salaam swahiba zako JPM na John Kijazi waambie Mama anaendelea kuupiga mwingi kwenye kuiendeleza Tanzania ya Uchumi wa Kati.

Pumzika kwa amani, ninyi mmetangulia sisi tuko nyuma yenu 😭😭😭😭😭😭
 
RIP Patrick Mfugale, Engineer aliyeboboea, mtu asiye na makuu, hakuwa na mdomo wa kubwabwaja kama ma CEO wengi.
Kwenye Elimu, sahihisha alienda Loughborough University of Technology, MidLands , Leicester UK.
Watu wanaandika kashfa kwa sababu tu alipendwa na Magufuli. Kusema ukweli mimi nilikuwa simjui na wala utendaji wake siujui lakini kwa kutumia hisia nadhani alikuwa mchapakazi na asiyependa kujikweza. Kwanini: Sijawahi kumsikia kwenye skendo au kujiona anajiweka mbele mbele kwenye media au mitandao au kuonyesha kwa namna yoyote kuwa ni msomi. Uzoefu unanifundisha kuwa watu wa aina hii huwa wachapakazi na wazalendo. Sijui huenda nimekosea lakini hisia zangu zinanituma hivyo.
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Hasara kwa Taifa Mungu akupe pumziko la milele.
 
Sasa kama unayajua yote haya,hayo maneno makali yanakutoka ya nini? Nikidhani wewe ni Immortal ndiyo maana unaongea kwa lugha ya majigambo kwa Marehemu

Nimekwambia unionyeshe masimango yoyote niliyoyaandika popote, kwenye uzi huu, humu JF au popote pale duniani. Hadi sasa umeshindwa.

Nakukumbusha tena, wapi nimetoa simango lolote achilia mbali masimango, popote?

If you are unable to show, please shut up!
 
Hiyo itakuwa ni BIP tu tokea kwenye lile wimbi.

Hebu leteni chanjo wajameni. Chanjo zenyewe si hiari?
Kijana na kilio cha chanjo, wake up, angalia aljeezera watu waliochanjwa wamelazwa kwa corona huko Russia. Uganda sasa wanaokufa ni wale waliochanjwa hata M7 amelazwa ingawa amechanjwa.
 
Katika kipindi chake hakuna madudu ndani ya TANROADS ambayo hata tetesi tumezisikia.
Barabara zimejengwa kwa mamia ya kilometa nchini kote.
Bw. Mfugale alikuwa ni mtu makini sana.

RIP Boss!
Ulitaka tetesi uzisikie wapi? nani angezisema kama hajaokotwa kwenye magunia kokobichi?
 
hawa ndi walikua chawa wa mwendazake na kwakua alikua kichaa aliona kama hawezi kazi yake kumpa mtu mwingine
Unavyoongea kama vile unamfahamu kwa karibu, kwa taarifa yako alishaomba kustaafu kitambo jamaa kachomoa
 
Yani jiji la Dodoma tangia lianzishwe umaarufu pekee lililo nao ni kuchinja chinja. Kama wewe ni mzee au kijana lakini una afya mbovu tafadhali sana epuka kwenda Dodoma.

Zingatia kisha unishukuru baadaye!
 
Back
Top Bottom