TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Alikuibia pesa gani wewe masikini namna hiyo?

Ndio maana rais kawambia acheni porojo za katiba fanyeni kazi!

Vijana mtakufa koo zenu zikiwa zinaliwa na umasikini huku mkitumika kuwapandisha madaraja kina Mbowe!

Mfugale kaacha alama kwenye ukoo wake, wewe ukifa hapo ulipo utaacha nini zaidi ya ukurutu tu?

Alafu eti ametuibia! Amekuibia wew na nani?
Haa haa eti ukurutu jamani forum raha sana
 
Zingesi
Katika kipindi chake hakuna madudu ndani ya TANROADS ambayo hata tetesi tumezisikia.
Barabara zimejengwa kwa mamia ya kilometa nchini kote.
Bw. Mfugale alikuwa ni mtu makini sana.

RIP Boss!
Zingesikika Vipi wakati hakuna alieruhusiwa kuziona??

Barabara Nyingi ni Mbovu na zinatitia hata baada ya muda mfupi tu....Kuwa nazo Km nyingi finyu na mbovu sio sahihi.
 
Zingesi
Zingesikika Vipi wakati hakuna alieruhusiwa kuziona??

Barabara Nyingi ni Mbovu na zinatitia hata baada ya muda mfupi tu....Kuwa nazo Km nyingi finyu na mbovu sio sahihi.
Ya kwako isiyo titia ni ipi?

Makao makuu tu ya chadema ni kama banda la choo
 
Nyerere hakupenda majina yake kutumika akiwa hai alisema ni uchuro.

Magufuli - Stendi, Daraja; Mfugale - tower, flyover; Kijazi - Daraja, Flyover.

Maneno ya Nyerere yanaweza kuwa na hoja.

Pale Dodoma napo pana soko nashauri jina kubadilishwa haraka.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Unamaoni gani kuhusu daraja la Kikwete na kile kitengo cha moyo chenye jila lake.
RIP P. Mfugale.
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
RIP Eng
 
Unamaoni gani kuhusu daraja la Kikwete na kile kitengo cha moyo chenye jila lake.
RIP P. Mfugale.

Maoni yangu msingi wake ni maoni (au mausia) ya baba wa Taifa bila exception.

Au wewe unaona je ndugu yangu?

Apumzike kwa amani bwana Mfugale.
 
Duhhhh alikuwa genius wa ujenzi!...timu yooote ya Mzee inaenda chini kuanzia kina kijazi what is going on jaman!
 
Ya kwako isiyo titia ni ipi?

Makao makuu tu ya chadema ni kama banda la choo
[/QU

Chadema Hapa Imeingiaje..Zangu ndio hizo nililipia Kodi....unadhani hela Ni Ya kwenu ile....Ninalipa Kodi tulia kaa kwa kutulia...Barabara Nyingi zina shida viraka kila mara yawezekana unanufaika na mfumo huo.
 
Alikuibia pesa gani wewe masikini namna hiyo?

Ndio maana rais kawambia acheni porojo za katiba fanyeni kazi!

Vijana mtakufa koo zenu zikiwa zinaliwa na umasikini huku mkitumika kuwapandisha madaraja kina Mbowe!

Mfugale kaacha alama kwenye ukoo wake, wewe ukifa hapo ulipo utaacha nini zaidi ya ukurutu tu?

Alafu eti ametuibia! Amekuibia wew na nani?
Umeona ee
Wanakera sana
Kazi kufuata mkumbo wa kisiasa tu
 
Nawakumbusha....Ripoti ya ukaguzi maalum wa BOT itakabidhiwa kesho. Presha inapanda presha inashuks
 
Daraja la Kijazi.... Daraja la Mfugale.... huku sio kuchuriana? Wazee wa maeneo husika wamekasirika! Turudishe majina ya asili ya maeneo husika! Daraja la Tazara, Daraja la Ubungo, stendi ya Kuu ya Mabasi Mbezi Louis!
Hivi jina la Kijazi si lilitolewa akiwa kashafariki? Labda la mfugale lakini sio hoja maana kuna daraja la Kikwete pia.
 
Back
Top Bottom