TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Upumzike kwa amani mhandisi Mfugale umeacha alama zenye kuonekana.

Kule Mwanza ukimuelezea juu ya ujenzi wa daraja mheshimiwa Rais ikakutoka “Hapana” halafu ukagundua unaongea na bosi wako ghafla ukageuza shingo kumcheki kama aina fulani ya kuomba msamaha. Rais alilielewa somo.

Wasalimie wote mliokuwa mnajenga Taifa pamoja.
 
Wewe endelea kujifariji nakwambia kama hutamsamehe yeyote kati ya wabaya wako hata Mungu hatakusamehe. Na ninakwambia usipende sana kushadadia mambo yasiyokuhusu bibilia inasema cheka na wanaocheka na lia na wanao lia.
Biblia hiyohiyo inasema kuwa yeyote anayeua kwa upanga nae atakufa kwa upanga.
 
Nyerere hakupenda majina yake kutumika akiwa hai alisema ni uchuro.

Magufuli - Stendi, Daraja; Mfugale - tower, flyover; Kijazi - Daraja, Flyover.

Maneno ya Nyerere yanaweza kuwa na hoja.

Pale Dodoma napo pana soko nashauri jina kubadilishwa haraka.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kabadirishe
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mbona unaonekana una makasiriko sana na Mfugale? Una ugomvi nae binafsi Mkuu,tangu mwanzo unamsimanga tu,jamani tujivunze walau jinsi ya kudeal na stress zetu za maisha.Haya ameshakufa,unadhani itakupa ahueni ya maisha wewe binafsi?

Masimango unayasoma wapi mkuu? Unaweza nionyesha masimango hayo tafadhali? Kufa ni jambo la kawaida na kila mtu atakufa kwa wakati wake:


Au hupendi tuandike lolote ila wewe?

Hudhani labda ungejifunza walau jinsi ya ku deal na stress zako hasa unapoona maoni ya watu ambayo aghalabu ni haki yao?
 
Watu wanavyo comment humu utazani wao hawatakufa kabisa,jamani jamani Kila nafsi iliyoumbwa na Mwenyezi Mungu itaonja mauti,hebu tuwe na akiba ya maneno,maana katika msiba huu,teyari Kuna mtu amekuwa mjane,wapo watoto teyari mayatima wako wajukuu wamekosa babu n.k

Na unakuta ni watu wazima kabisa tena wenye kutegemewa kutoa busara katika familia na koo zao.Lakini wakiwa hapa akili zao wanaziweka pembeni wanakuwa vituko kisa tu wanatumia fake ID.
 
Atakuwa ameondoka na hii phase 3, watanzania tujifunze kustaafu umri ukisogea, toka 77 upo kazini kweli jamani hakuna watanzania wengine? angekuwa ametulia na wajuu haya yasingetokea labda

Na Prof Baregu yeye aliondoka na ugonjwa gani?
 
Nyerere hakupenda majina yake kutumika akiwa hai alisema ni uchuro.

Magufuli - Stendi, Daraja; Mfugale - tower, flyover; Kijazi - Daraja, Flyover.

Maneno ya Nyerere yanaweza kuwa na hoja.

Pale Dodoma napo pana soko nashauri jina kubadilishwa haraka.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Wave 3 soko la Dodoma kukamilisha set
 
Back
Top Bottom