Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Si kweli hakuna baya lolote litakalotokea!
Acha uwoga wa kijinga kajikaka [emoji35]
 
Acheni kujipa moyo there is no way Rwanda akamkoromea Tanzania, Kenya na Uganda.

Hata DRC akiaamua kuitreat Rwanda kama magaidi anaipiga vizuri tu
 
Watu siwaelewi, eti Kenya itapigwa na Rwanda kisa wana experience ya kupigana vita ya ardhini.
Kwamba Kenya ije na Serbian Nora B-52K1 155mm self propelled howitzer among top in AfricaView attachment 2433410
Ije na American M118 105mm artilleryView attachment 2433411

Ije na F-5 fighters na Rwanda haina fighter jets kabisaView attachment 2433412
Ije na British Vickers MK3 tanksView attachment 2433414

Ije na various helicoptersView attachment 2433415

Na silaha nyingine nyingi tu ambazo ni superior in capabilities and number dhidi ya Rwanda kisha Rwanda iseme ilivyotuma wanajeshi mia tatu mia tatu Mozambique na wapi wapi uko hivyo wataishinda Kenya.

Hakuna anayetoa hoja za msingi kwa nini Kenya inaweza pigwa na Rwanda. Pointi zote nikiona zinanikatalia Rwanda kushinda, hisia tu za ukubwa wa Rwanda ambao haupo. Tofautisha mtu mwenye nguvu na mwenye fujo, Rwanda ina fujo za kudumu ambavyo hata Burundi wakitaka wanaweza anza leo after 20 years wakawa wasumbufu
Silaha kubwa kwenye Vita ni MORALE na COMMITMENT.

Hayo mavifaa huwa yanasaidia tu.

Iddi Amini alikiwa na vifaa vya kutisha na bado akawa na usaidizi wa Jeshi la Libya na Pakistan lakini hakushinda.
 
Rais Paul Kagame alikuwa anaapisha mawaziri wapya hapo jana mapema. Alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini baadae akahamia kwenye lugha ya Kiingereza na baadaye akatoa kitisho kizito kwa lugha ya Kiswahili. Wengi wetu tumeona hicho kipande chenye lugha ya kiswahili kikisambaa huko mitandaoni hasahasa kwa raia wa Tanzania na Kenya. Kitendo cha kusambaa mtandaoni kwa kasi hivi, inaonesha kabisa walengwa wa ujumbe ni watu gani.

Kwenye FASIHI njia moja kuu ya kufikishia ujumbe ni kuifahamu HADHIRA, lakini kubwa zaidi ni kufahamu lugha ambayo HADHIRA hutumia. Siku zote kimetumika Kinyarwanda na Kiingereza, lakini leo hii na Kiswahili juu, tena sehemu ambayo anatoa vitisho. Kwenye Dakika ya 27, ameanza kuwaliza mawaziri wake kama wanafahamu lugha ya kiswahili, wakamjibu wanelewa, ndipo akaanza kuzungumza kiswahili.

Huu ujumbe siyo wa wanyarwanda, wazungumzaji wakubwa wa lugha ya kiswahili wanafahamika, hivyo hicho kitisho ni ujumbe kwenu. Hajataja mhusika, mimi binafsi sitamtaja, lakini naamini walengwa mapema leo, watakuwa washafikiwa na huu ujumbe.

Alichokisema Rais Paul Kagame ni kwamba ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi. Kwamba Rwanda doesn't have the means, but they have the methods (ways). Hivyo kijiografia Rwanda ni nchi ndogo isiyo na rasilimali nyingi, lakini wao siyo migomba mifupi kama wanavyofikiriwa. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana.

View attachment 2433276
Kagame hawezi kupigana na Tanzania. Anachoweza ni kuua wanyarwanda wenzake na kuwavuruga wacongo. Kama anataka akimbie alipokaa, aanze kuigusa Tanzania.
Nafikiri anaamini DRC kuna wanaomvimbisha kichwa Tishikedi.
 
Acheni kujipa moyo there is no way Rwanda akamkoromea Tanzania, Kenya na Uganda.

Hata DRC akiaamua kuitreat Rwanda kama magaidi anaipiga vizuri tu
Kabisa. Atakuwa mpumbavu akiamua kupigana na Tanzania. Ndio siku atakimbilia ulaya kuwa mkimbizi
 
Ujumbe wa Jemadari Paul Kagame umefika kwenye yale Mafuvu magumu ya Kinshasa loud and clear.

qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
qRI8Gs7.gif
 
Kabisa. Atakuwa mpumbavu akiamua kupigana na Tanzania. Ndio siku atakimbilia ulaya kuwa mkimbizi
Na nyinyi akili yenu maharage tu, vita ni lazima nchi iweke mizinga mpakani? Kwa nini mnamchagulia wakati hajasema..
 
Wanyarwanda wamejipenyeza karibia kila sekta hapa nchini. Intelligence wako busy tu na issues za Chadema, uchawa na uchaguzi wa 2025. Kale kajamaa kaliwahi mkoromea msoga akaufyata kimya. Wenzetu wanaoperate kwenye viwango vingine kabisa sisi tumelala.
Acha kamba wewe..
 
Sas kosa kubwa waliliolifanya congo Ni kuruhusu uganda Kama moja wa wana operation Ni kosa San kitakacho watokeaa jeshi la waKenya mtaonaa

Ni full uzaliti
Ndio maana museveni alimtoa dogo jeshi la ardhini ili asilete mkosi
 
Kagame anawatishia KENYA ambao wamepeleka jeshi lao kupambana na waasi wa M-23.
Hao naawaambie ukweli kwa sababu wanapenda kimbelembele hata kama hawajachokozwa. Wengine kama Tanzania asijaribu kuchokoza.Awaulize Malawi wakati wa Joyce Banda.
 
Mama kamuweka BASHUNGWA wizara ya Ulinzi hakika atavuna alichokipanda kwa Mnyarwanda huyu
Kuna wizara ukiwekwa ni formality tu, huwezi agiza au kuamrisha chochote, wewe ni kuwasikiliza hao wataalam na kupeleka kunakohusika wanachotaka. Umewahi sikia Waziri wa ulinzi anafoka kwa majenerali?
 
Kagame anawatishia KENYA ambao wamepeleka jeshi lao kupambana na waasi wa M-23.

President Kagame Speaks out on Rwanda-DRC Crisis​


Source : IGIHE
Hujamuelewa naona katumia Kiswahili ili kuongea na wakongomani wa kunako uwanja wa mapambano maana wanazungumza Kiswahili cha ‘kwa fasi ya’



KT PRESS
www.ktpress.rw
President Kagame Points Out Double Standards In Dealing With ...


2 days ago — President Paul Kagame says that the insecurity problems that have dogged the Democratic Republic of Congo (DRC) for the past three decades ...
rw times Paul Kagame speaks on Congo crisis December 2022 from www.ktpress.rw

https://www.theeastafrican.co.ke/te...crisis-to-delay-drc-poll-4039136?view=htmlamp
 
Mama kamuweka BASHUNGWA wizara ya Ulinzi hakika atavuna alichokipanda kwa Mnyarwanda huyu
Kuna mambo hii nchi yetu inaweza kuwa imelala..ila sio kila jambo.

Kuwa tu Incharge kwenye Hospitali zetu kubwa mfano JKCI kuna vetting ya hatari inapitishwa..itakuja kuwa Wizara ya ulinzi?.

Na jambo jingine Waziri pale WU anampelekea tu Rais maombi ya Jeshi na bajeti zao..hakuna lingine la maana analoweza kuingilia na kuinfluence lifanyike kama Jeshi halitaki.
 
Na wewe usiwe mjinga,Tanzania haijalala kiasi hicho japo hatujafanya vya kutosha naona Kama unahemka kwa vijimaneno vya mfa maji hapo juu..

Tungekuwa hatufanyi kitu Leo hii tusingekuwa na urali wa biashara kuwazidi wote EAC yaana balance of trade yetu na majirani wote Ni surplus in terms of quantity and value licha ya changamoto zote..
Na balozi wa tz kule ruanda ni generali
 
Back
Top Bottom