Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Acha uwongo. Kati ya vitu nchi hii ni zero ni hiyo unayoita vetting.

Nchi hii, hata teuzi tu Rais huwa anapelekewa majina tu anateua bila kujua chochote.

Mimi Kuna watu nawajua wengi tu, siyo waTZ wamo kwenye system na siyo wabongo.

Kuna Mnyarwanda alisoma English medium fulani iko Karagwe, alivyomaliza La 7 akafaulu akapelekwa O-level Tarime sec, afaulu A-level akapelekwa Ihungo. Tayari akawa kwenye mfumo mpaka mkopo wa chuo na ajira.

Kati ya vitu Tanzania imekaa kizuzu ni Career development and recruitment.

Inategemeana tu na UCHAWA na connection, mtu yeyote anaweza akaokotwa tu akapewa uDED, RC au DC au hata Jeshini kicheo kwenda kusimamia watumishi waliokaa sehemu ya kazi kwa miaka 30.

Tena Kuna watu huwa wanateuliwa mpaka Rais anakuja kusaidiwa MITANDAONI, Mfano mzuri ni uliyekuwa uteuzi wa DG wa TPDC halafu akatumbuliwa baada ya masaa 2.

 

Attachments

  • EyMLpS9WgAg_gQI.jpeg
    112.5 KB · Views: 3
Kagame kamlenga yule Kubwa jinga wa Kinshasa, hajatulenga sisi Tanzania, sijui nyege tunazitoa wapi? sisi hatuna mgogoro wowote na Rwanda.
Kwa ujasusi kagame yuko vizuri🤷🏼‍♀️
 
Ninaelewa mkuu 'zitto junior', kuhusu hao M23 na uhusika wao na Kagame na Rwanda kwa jumla.

Swali la kujiuliza ni hilo: hawa M23 wasingekuwa na uhusiano wowote na Rwanda, kwa mfano utambulisho wao wa 'uTutsi' pangetokea tatizo kati ya DRC na Rwanda?
Mbona lile kundi jingine la 'kiHutu', Kagame analitumia kuwa sababu ya kujihusisha kwake kwenye mgogoro na DRC?

Hapana, DRC na wao sasa inaonyesha dhahiri wamekerwa na hivi viinchi vinavyojiingiza kwenye maswala ya nchi yao. Ni wao pekee watakaolimaliza hili swala, na ninaamini wameamua sasa kulimaliza.
 
Nijuacho mimi,Kagame amewekeza sana kwenye intelijensia kote Afrika mashariki kuliko unavyoweza kufikiri.

Anajiamini kwa kuwa anajua jinsi tulivyogawanyika na anaweza kupata wasaliti wengi sana kwa gharama ya pesa kidogo.

Anajua jinsi tulivyowekeza kwenye siasa za kujuana na kwa hiyo wale wasiojulikana wanaweza kufanya lolote kwani wanaona kama wametengwa.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kwa ujasusi kagame yuko vizuri🤷🏼‍♀️
Unajua Jamii ya Kitutsi imeishi kwa manyanyaso makubwa katika jamii za Kihutu sasa wameamua kujihami hata kwenye huu mgogoro wa sasa Watutsi ndio Victims lakini baadhi ya Serikali za Kibantu zimeugeuza huu mgogoro kuwa Watutsi mdio wa kuBlame.

Kama mimi ningepewa fursa nimgeumaliza huu mgogoro ndani ya Mwezi mmoja tu.
 
Unajua kiherehere cha Kenya kinatokea wapi?
Wana/walikuwa na 'project' yao, ambayo ilikuwa ni Tshisekedi, wakimchukulia kama 'client' wao.
Walitaka ku'impress', sasa wanajikuta mambo ni mazito kuliko walivyodhani.
 
Tatizo? Hao watutsi ndio walikomboa DRC kutoka Mukono ya Mobutu so wanaona Wana haki ya kugawana rasilimali kuliko Sasa ambako Kinshasa wanafuja Hela huku Goma sijui Bukavu njaa tupu ilihali madini ya kumwaga.

Unfortunately Kabila desire alikiuka makubaliano na kuwatimua watutsi wote pamoja na makabila ya "kitutsi" (Haya yalikuepo DRC miaka na miaka kama tu wahangaza huku Tz) kurudi Rwanda.

Kilichofuata ni kisasi Cha watutsi (Bila kujali Burundi, Kivu, Rwanda, UG au Tz) kupitia makundi kma RCD.... MLC... UPC n.k so hiyo vita haitaisha unless wapewe "mgao" wao wa "kuikomboa" DRC!!

Otherwise Kivu North pamoja na Ituri ziendelezwe miundombinu, pesa ikiwepo then malalamiko na uasi utaisha.
 
Bora umeongea ukweli mkuu, kwenye vetting Kuna walakini mkubwa otherwise Kuna baadhi ya watu wasingekuwepo sekta nyeti!!
 
Dah!
Hili tuliache. Umewapa ujiko mkubwa sana wasioustahiri.
Hawa watu walitumia udhaifu wa li nchi kubwa sana, lenye utajiri mkubwa kujitanua na kujipa umuhimu kupitiliza.
Inavyoelekea bayana kabisa sasa, makabila mengine yaliyoko eneo hilo, na wao sasa wamekuwa upande wa pili dhidi ya hicho kikundi cha M23.

Katika hali na namna hiyo, M23 itakuwa ikipambana katika eneo wasiloungwa mkono na jamii inayoishi humo. Kazi ya mapambano hayo itakuwa ngumu kwao.
 
Katika madhaifu yote ya nchi hii, hali yetu mbaya inayotukabili sasa inaanzia huko, kwa hawa waliopewa jukumu la kuhakikisha hatuingiliwi kipumbavu.

Sehemu hii ndiyo imesababisha kuenea kwa uozo kila sehemu nchini.
Hata marais sasa hatuna uhakika wanakotokea na ni watu wa aina gani
 
Makabila yapi? Hayo matatizo ya ukabila yamekuwepo tokea Mobutu sema tu alikua anawasaidia wahema na wanyamulenge wasivamiwe na wenyeji.

Yes hata Israel inapambana eneo isipoungwa mkono same to watutsi wa Burundi walikua 20% pekee ila waliitawala Burundi kwa tokea uhuru!! Kwani walikua wanakubalika? Hata uchaguzi haukuwahi fanyika pre 1990s.

Museveni ni Mtutsi pia ila anatawala Wagganda miaka 40 Sasa. So hiyo sio hoja kabisa.

3. Unasema Congo ni dhaifu so Wana take advantage?? Are u sure? Mbona hata hao wazungu na majeshi mengine ya Africa yanatumia mgongo wa vita kujinufaisha? Au ni halali Zimbabwe na Angola kuiba mafuta na Dhahabu ila Kwa Rwanda ni haramu? Au kuna double standards
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…