Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Sasa kama aliaona anakaribia kukamuliwa mavi ulitaka abaki? Ushaambiwa alikuwa chini ya darubini kali! Tz ni nchi isiyo na ubaguzi, huwezi kuzuiwa ajira kisa una asili ya nchi fulani..., hii ni nchi huru
 
Kagame anawatishia KENYA ambao wamepeleka jeshi lao kupambana na waasi wa M-23.
Sisi tuliwatimuaga hao m23 wake chapu tu, mbona alinywea? Tukamalizia na oparesheni kimbunga..
 
Nionavyo mm pia Kaghame hajajuwa kuwa nimfupi ila anajiona mrefu. Swali rahisi angejiuliza ni nani anasumbua DRC? Na je ninani anachezesha huu mchezo. Akijuwa hili ataiponya nafsi yake ila asipo lijuwa hili Pagasus yake itakuwa ina mpa wrong taarifa. Ukiniuliza mm nitasema neno moja siku za Marais wa miasha wawili zina soma kama mshale wa saa. Keep silence u shall see maneno ya mtabiri wa kimataifa. Asante
 
Sasa si ndo vita inaendelea huko Mashariki mwa DRC mkuu? Au huna habari🤣
 
Eneo lenye maslahi makubwa kwa Tanzania ni jimbo la zamani la Katanga. M23 hawana nia yoyote ya kwenda hadi jimbo la Katanga.
Bidhaa tunazouza nyingi zinakwenda jimbo la Katanga kutumika katika shughuli za uchimbaji wa madini. Bidhaa nyingi za transit zinazopitia bandari zetu na kubebwa na magari ya Kitanzania na Kitanzania-Zambia, zinaenda katika jimbo la Katanga zamani. Siku hizi ni majimbo mawili.
Kwa uchache wa maslahi yetu mashariki mwa DRC ukilinganisha na Uganda, Rwanda na Kenya, sioni sababu ya kumwaga damu ya vijana wetu kwa ajili hiyo.
Sisi tukae macho, usumbufu wowote usitokee kusini na kusini mashariki mwa DRC. Sisi maslahi yetu yapo sana katika Copper Belt ya Zambia na DRC ambayo pia ina madini mengine lukuki.
 
Kuna makundi mengi sana ya kikabila yenye silaha mf Codeco ya walendu, maimai ya wabembe na vingine vingi tu.

Kupokonywa silaha ni muhimu kwa amani ya kudumu ya Drc
 
Hapana, sikubaliani nawe kamwe kwamba maslahi ya Tanzania yanaishia Katanga.

In fact, maslahi makubwa zaidi yapo huko kati na kaskazini mwa DRC. Kushindwa kwetu hadi sasa kutumia fursa isiwe sababu ya kutoendelea kutafuta fursa hizo.

Kwa nini uwepo wa Ziwa Tanganyika kati yetu ndiyo kiwe kikwazo kwetu badala ya kufanya kuwe fursa baina yetu?

Usinielewe vibaya, sichochei tujitumbukize kichwa kichwa kwenye mgogoro wa waKongo. Sisi tulishafanya kazi ya aina hiyo, ya kupigania wenzetu siku nyingi sana, na hakuna anayehoji heshima hiyo kwetu. Hiyo kazi tuliimaliza, wakati huu tusilaumiwe kwa kutojihusisha na maswala ya namna hiyo, lakini ni wajibu wetu mkubwa wa kujihusisha na mashirikiano ya kiuchumi baina yetu. Kama ni upatanishi, sawa; na kama hatuchokozwi, sioni sababu ya kwenda kupambana.

Ninakusihi, hebu chukua ramani tena, na angalia kwa makini sana tulipo (Tanzania) na ushiriki wetu katika eneo husika.
Tanzania ndio lango sahihi la kuingila Mashariki yote ya Congo, tusijirudishe nyuma kwa visingizio visivyokuwepo.
Halafu uje uniambie Mombasa achukue nafasi dhidi yetu? Sikubaliani nawe kabisa.
 
Huyo Kagame yeye alifanya nini baada ya kulijua shuka la kulalia la JK? 🤣🤣🤣, machocko wengine bhana...
 
Kuna makundi mengi sana ya kikabila yenye silaha mf Codeco ya walendu, maimai ya wabembe na vingine vingi tu.

Kupokonywa silaha ni muhimu kwa amani ya kudumu ya Drc
Kundi la Wakongo wenye asili ya Kitutsi M23 liingizwe kwenye Jeshi la Kongo halafu Nchi za jumuia za Afrika Mashariki tuli train Jeshi la DRC liwe kwenye Standard kama zetu ili visitokee vikundi vingine tena kutumia Ardhi ya Kongo kushambulia Majirani.
 
Hongera kwa kujibu kwa hoja. Una kiwango fulani cha maturity bila kujua umri wako.
Mimi na wewe tuna mawazo yanayofanana tukichukua concept na kuacha tofauti ndogo ndogo za kibinadamu.
Mfanano wetu uko hivi:
1. Sote tunataka kufaidika kutokana na kuwa jirani muhimu kwetu na kwa Ulimwengu yaani DRC kwa maana ya sisi kuuza na kununua kwao lkn pia na bandari yetu kuwa kama lango muhimu la kuingilia DRC na hivyo nchi yetu na watu wake hasa wafanyabiashara kufaidika.
2. Sote tunakubaliana kwa concept kwamba hatuna sababu ya kumwaga damu ya vijana wetu tena.
3.Nakubaliana na wewe kwamba hatutatakiwi kukaa kuegemea migongo kwenye viti bila kushirikia mchakato wa kutafuta amani mashariki mwa DRC. Hata mimi nashangaa Kenya wamekuwa mstari wa mbele huku sisi ambao ni marafiki wa DRC tukiwa waangaliaji tu, just watchers, not observers.
Lakini natofautiana na wewe juu ya kuangalia jiografia. Mashariki mwa Congo hakuna biashara ya maana kwenye eneo la consumption zaidi ya extraction ambayo ndio hiyo inapambaniwa. Vurugu tupu.
Bado nasisitiza kuwa asali kwetu as we speak ni kusini na kusini mashariki kwa DRC.
 

Sasa hivi tutarudia hii oparesheni!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…