Paul Kagame: Ukiona wenye mali wanageuka kuwa ombaomba ujue akili zao haziko sawa

Kagame ana akili kwa kidogo Alichonacho ameonyesha nini maana ya kuwezekana kuleta maendeleo afrika .
 
Yeye ana akili au ni mbwa kama wewe tuu?
Akili anazo na ndio maana ameweza kuliona hilo tatizo na kuthubutu kulisema, na sio yeye tu mkuu watu wengi wa nchi zengine huwa wanatushangaa sana watanzania.

Nasikia Kikwete aliwahi kuulizwa kwa nini Tanzania masikini akajibu hata yeye hajui.
 
Huu ni ukweli wala hauniumi ila jambo linaloniuma ni kuwa huyu mtu anayomambo yetu mengi sana ambayo hatujui lini atayatumia kutudhuru. Kauli yake inamaanisha anajua kila kitu chetu hata jinsi tunavyotembeza bakuli huko nje. PK ana watu,tena wako ndani kabisa ya mifumo yetu.
 
Huyu anajua hadi mikataba ya kimangungo tunayoingia ambayo inahamisha rasilimali zetu bila sisi kunufaika ndiyo maana anatucheka ujinga
 
Japo simpendi ila katoa ujumbe sahihi.
 
Japo simkubaligi huyu jamaa ila hapa kaongea ukweli kabisa.
Kuhusu anaifanyia nini Rwanda ,Rwanda haina rasimali zozote.
Kashindwa kuweka lami nchi nzima yenye ukubwa wa nusu ya mkoa wa tabora!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…